Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

UKWAKATA wakoleza Utume

Mwenyekiti wa Utume wa Kwaya Katoliki Tanzania (UKWAKATA), Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Cassian Kahimba (kulia), na viongozi wengine wakiwashukuru Wanakwaya wa jimbo hilo kwa kuhudhuria Adhimisho la Misa Takatifu ya Jumatatu ya Pasaka iliyoadhimishwa Parokia ya Mtakatifu Bonaventura, Kinyerezi. (Picha na Yohana Kasosi) Mwenyekiti wa Utume wa Kwaya Katoliki Tanzania (UKWAKATA), Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Cassian Kahimba (kulia), na viongozi wengine wakiwashukuru Wanakwaya wa jimbo hilo kwa kuhudhuria Adhimisho la Misa Takatifu ya Jumatatu ya Pasaka iliyoadhimishwa Parokia ya Mtakatifu Bonaventura, Kinyerezi. (Picha na Yohana Kasosi)

DAR ES SALAAM

Na Celina Matuja

Utume wa Kwaya Katoliki Tanzania (UKWAKATA), Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, wametajwa kuwa ndiyo wamekuwa wakikoleza Uinjilishaji kupitia tungo na nyimbo zao za Injili.
Kutokana na kuifanya kazi hiyo kwa bidii na kwa sifa na utukufu kwa Mungu, Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Stefano Musomba amewapongeza Wanakwaya hao, alisema kuwa wanafanya kazi kubwa licha ya dosari chache zinazojitokeza ambazo zikirekebishwa mambo yatakuwa mazuri zaidi.
Askofu Musomba alisema hayo katika sherehe ya UKWAKATA Jimbo, iliyofanyika Parokia ya Mtakatifu Bonaventura, Kinyerezi wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Jumatatu ya Pasaka, ambayo mwaka huu ilikuwa na kauli mbiu “ Tumwimbie Bwana, katika Roho na kweli.”
Alisema kuwa kuimba na kumtangaza Kristo Mfufuka ni jambo muhimu ambako linatakiwa kwenda sambamba na matendo namna ya kuishi kwao, unyenyekevu, utii, moyo wa ibada na
uchaji kwa kufanya hivyo ili kila anayewaona aseme kweli hilo ni tanganzo la Kristo mfufuka.
Aidha Askofu Msomba aliwataka Wakatoliki kuiga mfano wa wanawake waliokwenda kulitazama Kaburi, alimozikwa Yesu Kristo na kupewa Habari kuwa amefufuka, aliendea mbio kuwapasha habari wanafunzi wake ila walipo kutana na Yesu walianguka chini na kumsujudia na kumwabudu.
Alisema sio vema kuishi kwa mazoea kwa kuwa wakati mwingine mazoea yanapotosha na kupelekea watu kutozingati misingi ya Imani na kupokea EkaristiTakatifu kwa mazoea.
Aliwasihi waamini hao kuhakikisha kutojiongelesha mezani pwa Bwana na kuonyesha hali ya kuabudu na kwa unyenyekevu katika kuonyesha heshima kwa Mungu.
“Ni suala la kujiuliza kila mmoja wetu, hasa anapokwenda kushiriki Ekaristi Takatifu …utaona kuhani anamwambia mtu mwili wa Kristo anakutazama tu, ni kama hajawahi kusikia na kuhani akirudia mwili wa kristo, basi hapo atadhani anasalimiwa na kujibu milele amina hajui nafanye nini,’’ alisema Askofu Msomba.
Akiwageukia waimbaji ambao ndio ilikuwa siku yao, Askofu Musomba, alisema wote wanatakiwa kuonyesha ushirikiano kati ya walimu na wanafunzi wao, ili kuondoa majivuno, kwani wapo baadhi hawaimbi kama Utume, bali hupenda kujionyesha kuwa bila yeye hakuna mwingine anayeweza.
Kwa mujibu wa Askofu Musomba, ingawa wapo wanaotumikia vema utume wao, wapo baadhi wanaimba kwa kiburi na kuwakwaza hata wenzano, wengine wameshindwa kabisa kuimba na kucha kazi hiyo, akiwataka kutambua kwamba kipaji cha uimbaji kimetoka kwa Mungu.
Alisema si vema mwanakwaya kujigamba kwa namna yoyete ile, kwani wakati mwingine baadhi ya wanakwaya huleta fujo kwa kutofautiana na Makuhani hasa wanaporekebishwa ana kukosolewa.
‘Niwaombe msimruhusu adui shetani kutawala bali wamtangulize Mungu daima, ili maisha ya utume wa uimbaji yawe mazuri na kuwafikisha katika uzima wa milele, tumeumbwa ili tumjue Mungu na tuchochee karama zetu na za wengine ili kauli mbiu yenu iendane na kile mnachofanya,’’ alisema Askofu Musomba.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Utume wa Walei Jimbo, Padri Vitalis James Kassembo aliwapongeza WanaUKWAKATA na kuwataka wajibidiishe katika elimu ya mambo ya Uchumi yaani elimu endelevu, ambayo itawasaidia kujikwamua kiuchumi.
Aliwaomba Viongozi wa Halimashari za Walei ngazi zote kuhakikisha wanasaidia baadhi ya wanakwaya, ambao hawana elimu juu ya Uchumi ili waipate kama kikundi.
Naye Dekano wa Dekania ya Segerea Padri Cornelius Mashale ambaye pia Paroko wa Parokia ya Kristo Mfalme Tabata, alikazia kuhusu wale Wanakwaya wanaoishi kama mume na mke kwa muda mrefu kuhakikisha wanarekebisha maisha yao, wka kutoka kuishi giza na kuukaribisha mwanga kwa kufunga ndoa Takatifu.
Padri Mashale alisema maisha hayo hayatafsiri vizuri maisha ya mkristo anayejua nini maana ya kuishi Sakramenti ya ndoa na uimbaji wao ama uinjilishaji wanaoufanya.
Alibainisha kwua haina maana pale wanakwaya wanapoomba barua au kibali cha kwenda kuinjilisha parokia Fulani, halafu nusu ya kikundi chote cha kwaya unapofika muda wa komunio wao ndio wa kwanza kutoshiriki.
Naye Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Bonaventura, Kinyerezi Padri Francis Hiza, aliwapongeza wanaUKWAKATA Jimbo, kwa kuadhimisha siku yao hiyo.
Akisoma risala mbele ya Askofu Katibu wa UKWAKATA, Jimbo, Paulina Abias alitaja mafanikio katika utume wao kuendelea kuimarika, kutokana na semina za kiroho na kwamba wanayo mipango mingi ya kufanya ikiwemo kuwa na studio yao ya kurekodi nyimbo jimboni.
Sherehe hizo zilikwenda sanjari na utoaji vyeti vya kuhitimu muziki Mtakatifu kwa wahitimu 24 katika madaraja manne na walitakiwa kujitokeza kujifunza muziki mtakatifu ili kutekeleza zoezi la kuutunza muziki huo.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.