Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Wenyeheri wapya watangazwa DRC

VATICANCITY, Vatican

Baba Mtakatifu Fransisko amekumbusha Wenyeheri wapya, Wamisionari Waxaveri wa Kiitaliano waliotangazwa kuwa wenyeheri Agosti 18, mwaka huu, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC.
Baada ya Sala ya Malaika wa Bwana, Baba Mtakatifu Fransisko alisema kuwa kutangazwa kwa Wenyeheri hao kutakuwa kitulizo cha vita nchini DRC,
“Kifo chao cha kishahidi kilikuwa kilele cha maisha yaliyotumiwa kwa ajili ya Bwana, na kwa ajili ya ndugu zao…mfano wao na maombezi yao yatie moyo njia za upatanisho na amani kwa manufaa ya watu wa Congo,”alisema Baba Mtakatifu Fransiko.
Baba Mtakatifu Fransisko alikumbuka tukio la kutangazwa Wenyeheri wapya katika nchi ya Afrika na kueleza kwamba:
“Huko Uvira  katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Luigi Carrara, Giovanni Didoné na Vittorio Faccin, Wamisionari Waxaveri wa Kiitaliano, walitangazwa kuwa Wenyeheri, pamoja na Albert Joubert, Padre wa Congo, waliouawa katika nchi hiyo Novemba 28, 1964.
Baba Mtakatifu aliendelea kutazama hali halisi ya ulimwengu wa vurugu kama kawaida yake, alisema: “Na tunaendelea kuomba kwamba njia za amani ziweze kufunguliwa katika Mashariki ya Kati - Palestina, Israel - na vile vile katika Ukraine inayoteswa, Myanmar na katika kila eneo la vita, kwa kujitolea kwa mazungumzo na majadiliano na kujiepusha na kujibu kwa vitendo vya vurugu.
Aliwaasalimia Waamini wote kutoka Roma na Mahujaji waliotoka Italia na nchi mbalimbali. “Hasa ninawasalimu wale wanaotoka Jimbo la Mtakatifu Paulo nchini Brazili; na pia Masista wa Mtakatifu Elizabeth.
“Ninatuma salamu zangu na baraka zangu kwa wanawake na wasichana waliokusanyika katika Madhabahu ya Maria wa  Piekary Šlskie huko Poland, na ninawatia moyo kushuhudia Injili kwa furaha katika familia na katika jamii.”
Aidha, Baba Mtakatifu Fransisko aliwasalimu watoto wa Parokia ya Moyo Safi wa Bikira Maria kutoka Roma. Hatimaye amewatakia Dominika njema, huku akiwaomba wasisahau kumuombea. Mlo mwema, mchana mwema na kwaheri ya kuonana.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.