Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Makatekista Pugu wapewa mwelekeo Maisha ya Kiroho

Mlezi wa Makatekista wa Dekania ya Pugu, Padri Pius Thomas -MSFS (katikati mstari wa nyuma), ambaye ni Paroko wa Parokia ya Bikira Maria Mama wa Huruma, Mji Mpya Relini, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam akiwa katika picha ya pamoja na Makatekista baada ya Misa Takatifu ya Shukrani kwa kuelekea kumaliza Mwaka 2024. (Picha na Laura Chrispin) Mlezi wa Makatekista wa Dekania ya Pugu, Padri Pius Thomas -MSFS (katikati mstari wa nyuma), ambaye ni Paroko wa Parokia ya Bikira Maria Mama wa Huruma, Mji Mpya Relini, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam akiwa katika picha ya pamoja na Makatekista baada ya Misa Takatifu ya Shukrani kwa kuelekea kumaliza Mwaka 2024. (Picha na Laura Chrispin)

DAR ES SALAAM

Na Laura Chrispin

Makatekista wa Dekania ya Pugu, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, wameaswa kuishi maisha ya utakatifu ili wawe mfano bora kwa wengine.
Wito huo ulitolewa hivi karibuni na Paroko wa Parokia ya Bikira Maria Mama wa Huruma Mji Mpya Relini, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Padri Pius Thomas -MSFS, ambaye ni Mlezi wa makatekista wa Dekania hiyo.
Padri Pius  alisema hayo katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Shukrani ya Makatekista wa Dekania ya Pugu, kumshukuru Mungu kwa kuumaliza salama mwaka 2024, na kuukaribisha mwaka 2025, iliyofanyika Parokia ya Mtakatifu Thomas Mtume-Chanika, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam.
“Kila Katekista inampasa atembee zaidi Kisinodi akiufuata mfano bora wa maisha ya Mama Bikira Maria, ambaye mara zote anawasaidia kutenda kazi za uinjilishaji, kwani ninyi mliitwa na mkaitika kwa kazi ya Mungu,”alisema Padri Pius.
Aidha, alisema kuwa hata Mama Bikira Maria alikubali maagizo aliyopewa na Malaika kwani aliitika na kusema,  ‘Mimi mjakazi wa Bwana, nitendee kama ulivyo nena,’ aliendelea kusema Maria alitambua kuwa ile ilikuwa ni kazi ya Mungu, na siyo ya malaika.
Padri Pius aliwataka Makatekista hao kutambua kwamba Bikira Maria, alikubali kila mtu aige mfano bora wa maisha yake kwa kutazama zaidi fadhila za Kimungu.
Kwa mujibu wa Padri Pius Makatekista hao wanatakiwa kufahamu kuwa Kipindi cha Majilio, kila mtu anatakiwa kutafakari na kujiuliza, je anawajibika kama Bikira Maria? Na kumshukuru Mungu kwa kuhitimisha mwaka 2024 na kuomba baraka na neema kwa mwaka ujao 2025.
Aidha, Padri Pius alitoa wito kwa Makatekista hao kutambua kwamba wao ni mzizi wa imani wa Kanisa Katoliki hivyo, hawatakiwi kuwa kikwazo kwa wengine, au chanzo cha kuwapotosha watu katika imani ya Kanisa Katoliki.
Aliwasihi Makatekista hao, kumkabidhi maisha yao Bwana Mungu, ili waweze kupata fadhili zake, wakiendelea kufundisha habari njema kwa watu, wakiliongoza Kanisa, kwani wao ndio wenye kumkuza mtu katika imani tangu kuzaliwa hadi kufa.
“Bikira Maria anafundisha unyenyekevu na utii, na huo huo unauona hata kwa Yesu kwa kutii na kukubali kunywa kikombe cha mateso, na unyenyekevu huo unang’aa ndani yake,”alisema Padri Pius.
Alitumia nafasi hiyo, kuwataka Makatekista kumshukuru Mungu na kumwomba Mama Bikira Maria, kama mwombezi wao, hata katika wakati mgumu pasipo kukata tamaa.
Naye Katibu wa Makatekista Dekania ya Pugu, Katekista Gerald Shukuru, aliwashukuru Makatekista kwa ushirikiano wao.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.