Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Simba, Yanga zawindana usajili

Elie Mpanzu Elie Mpanzu

DAR ES SALAAM

Na Mwandishi wetu

Klabu za soka za Simba na Yanga zimeanza kutegeana kuhusiana na kuweka wazi mipango yao ya usajili katika dirisha dogo lililofuguliwa Desemba 15 mwaka huu.
Licha ya tetesi za hapa na pale, timu hizo zimeonekana kuwa na siri kubwa kuhusiana na kile wanachoendelea kukifanya katika kipindi hiki cha usajili, huku kila moja ikitegeshea mwingine aweke mambo hadharani.
Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe, alisema kuwa kwa sasa hawezi kuweka wazi wachezaji waliowanyakua na wale wanaopanga kuwatoa kwa mkopo katika kipindi hiki, isipokuwa anachofahamu ni kwamba kuna mchezaji mmoja wataachana nae katika kipidi hiki.
“Nilipata fursa ya kuwasiliana na Mtendaji Mkuu wa Klabu na akanionyesha jina moja la mchezaji ambaye hatokuwa sehemu ya kikosi cha Yanga baada ya dirisha dogo kupita.Na siwezi kumtaja mchezaji huyo kwa sababu zilizo nje ya uwezo. Tusubiri dirisha lifungwe,”alisema Kamwe.
Hata hivyo, Tumaini Letu linafahamu kwamba Yanga ina mpango wa kumsajili kiungo mkabaji mmoja, mshambuliaji mmoja, na beki wa kati mmoja.
Kwa upande wake Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Simba, Ahmed Ally naye ameonekana kufinyanga maneno kuhusiana na usajili wao huku akisema kwamba hadi sasa hakuna mchezaji yeyote waliyemnasa, na hata anayetolewa kwa mkopo, hakuna.
“Sisi zaidi ya Elie Mpanzu ambaye tumeanza kumtumia kipindi hiki, hatuna mchezaji yeyote yule tuliyemsajili.Hayo mengine ni maneno tu ya watu wa pembeni.Kama ikitokea tuna jambo jipya, tutawafahamisha,”alisema Ahmed Ally.
Vigogo hao wa Simba na Yanga wamekuwa na tabia za kutangaza wachezaji wapya, huku wakiweka muda maalum wa kuwatangaza kwenye mitandano yao ya kijamii.
Simba imekuwa na utaratibu wa kutambulisha wachezaji wake saa saba mchana, huku Yanga wakijiwekea utaratibu kama huo katika majira ya usiku.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.