DAR ES SALAAM
Na Paskazia Nestory
Jamii ya siasa kwa hivi tuna mambo mengi yanayotuzunguka, mathalan harakati nyingi, mipango mingi shughuli nyingi na zinatufanya tukose muda wa kuongea na Mungu hasa katika sala kusoma Neno la Mungu, na kutafakari.
Hali hii inapelekea kuwa na mikwamo kila mahali kwenye familia, jumuiya, vikundi vya sala Kanisa na Taifa.
Kiongozi yeyote anahitaji kuombewa ili aweze kuongoza vyema sehemu anayokuwa amesimamia.
Madhara yanaweza kujitokeza kwa kukosa kuwaombea viongozi. Biblia inahitaji sehemu mbalimbali kuhusu maombi kwa ajili ya viongozi, Esta, 4:16 Esta anakubali ushauri wa mjomba wake Modekai anaamua kufunga kusali na kuomba kwa ajili ya (Wayahudi) Taifa la Israeli, na kumwomba Mungu ampe kibali cha kuingia kwa mfalme.
1.Tuanzie kwenye familia:
Kiongozi wa nyumba (baba na mama) akiyumba, nyumba yote inafarakana. Malezi ya watoto yanakuwa hafifu na matarajio ya familia yanapotokea.
2. Kanisa Kiongozi wa Kiroho akiyumba, Kanisa lote linakosa msimamo. Waamini wanakosa imani na Kanisa lao na kiongozi wao, na kondoo wengi wanatangatanga, Efeso, 6:18 Mtume Paulo anakazia jambo hilo kwani ni himizo kwa kila Mkristo kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho Mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea Watakatifu wote.
Kwa mambo mengi tuliyonayo sisi, tumewachosha viongozi wetu wa Kanisa. Tunawapelekea mizigo mizito ili waitatue, lakini wao wanashindwa kutatua migogoro yetu, hatuwaombei, nao hawana nafasi ya kutosha kujiombea wenyewe.Tunapowachosha huduma zao zikaenda ndivyo sivyo, tunawanyooshea vidole.
Kama wewe ni Mkristu Mkatoliki, nakuomba usifanye hivyo kama kiongozi wako wa kiroho akikengeuka. Kitu cha kwanza mwombee bila kuongea chochote, maana ukifanya hivyo, Mungu yupo tayari kusamehe. Lakini kama unaona kuongea kama watu wengine wa mataifa kama biblia inavyotaja, kutakusaidia utajidanganya na utabeba dhambi yake na yako. Tukumbuke hawa ni wapakwa mafuta (makuhani) yatakupata yaliyompata. Aroni na dada yake Miriam, Mwenyezi Mungu anatafuta mtu mmoja tu kujenga mahali palipobomoka Ezek, 22:30.
Hawa ni ndugu zetu, watoto wetu, kaka zetu na jamaa zetu. Tunawapenda na kuwathamini ili huduma yao iwe nyepesi.
Viongozi wa Nchi:
Tusipowaombea Viongozi wa nchi jua kazi kubwa iko kwetu. Tusisubiri kwenye ibada za Jumapili, shetani muda wote yuko kazini.
Uongozi ni mzigo na kama ujawahi kuwa kiongozi mahali popote hata kuwa kaka au dada wa darasa, huwezi kufahamu jambo hili.
Ukimwona mjumbe wa mtaa anaboronga, usipambane nae mwombee tu, Mungu wetu si mwanadamu anashughulika naye. Vile vile Muheshimu amebeba dhamana kubwa.
Viongozi wakubwa, wanakutana na mambo makubwa wanapambanishwa na mambo mengi. Hata wa Dini wakipata madaraka makubwa, kiburi kunaweza kuinuka ndani yao na kuanza kutoa amri kama wanavyotaka wao, bila kufuata sheria kanuni, na miongozo husika. Upinzani unaanza machafuko na mafarakano yanaanza kati ya kiongozi na waongozwa.
Tuombe neema ya kutubu:
Ee Bwana kumbuka yaliyotupata, utazame na kuona aibu yetu, urithi wetu umegeuka kuwa mali ya wageni wa nyumba zetu kuwa mali za makafiri Maomb, 1:5,1-2 Kiongozi wa nchi akifanya yasiyompendeza Mungu, Taifa lote linaingia hatarini, haijalishi maskini, tajiri wala mwenye cheo, Tuombeane ili Mungu atusaidie katika madhaifu tuliyonayo.
Kama hawa Viongozi tunawapelekea shida zetu ili wazitatue, je, shida zao wao wanazipeleka kwa nani?
Sisi ndio tunapaswa kupeleka chngamoto kwa Mwenyezi Mungu ili awape nguvu ya kutenda kazi yake.