Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

‘Dumisheni Injili ya Uhai’

VATICAN

Baba Mtakatifu Fransisko amewataka Waamni kusimama kidete kulinda na kutetea Injili ya uhai dhidi ya utamaduni wa kifo, akiwasisitiza kupokea zawadi ya uhai kwa moyo wa upendo, shukrani na ukarimu.
Aliyasema hayo wakati wa Dominika ya Nne ya Majilio, Mwaka ‘C’ wa Kanisa, ambapo pamoja na mambo mengine, Baba Mtakatifu alisema, “Bikira Maria ambaye baada ya kupashwa habari kuwa atakuwa ni Mama wa Mungu, anakwenda kwa haraka kumtembelea binamu yake Elizabeti, ambaye katika uzee wake, alikuwa ni mjamzito.”
Aidha, aliwaalika Waamini pamoja na watu wote wenye mapenzi mema, kusimama kidete kulinda na kutetea zawadi ya uhai tangu pale mtoto anapotungwa mimba, hadi mauti ya kawaida yanapomfika, kadri ya mpango wa Mungu.
Sambamba na hayo, Baba Mtakatifu anakaza kusema kwamba Kanisa linataka kujitosa kuwahudumia kwa ukarimu na upendo watoto wadogo ambao bado hawajazaliwa zaidi ya wengine wote, kwani hao ni watu wasio na ulinzi wala hatia.
“Wanawake hawa walikuwa na kila sababu ya kufurahia kutokana na miujiza iliyotendwa ndani mwao, mwaliko ni tafakari ya kina kuhusu uwepo wa Mungu kati ya waja wake na kwamba, huruma na upendo wake unamwandama mwanadamu kwa njia ya zawadi ya maisha, kwa kila mtoto anayebebwa tumboni mwa mama yake, kama ilivyo kwa wanawake wengi na kati yao kuna wale ambao wanatazamia kwa imani na matumaini, kuzaliwa kwa watoto wao,” alisema Baba Mtakatifu.
Vile vile, aliwaalika Waamini kupokea zawadi ya uhai kwa moyo wa upendo, shukrani na ukarimu, akisema, “Hata watoto ambao hawajazaliwa, wameumbwa kwa sura na mfano wa Mungu. Jamii isipojifunza kuwalinda na kuwatunza watu dhaifu, sheria ya mwenye nguvu mpishe, itatawala Dunia. Maskini wanao upendeleo wa pekee mbele ya Mwenyezi Mungu. Wao ni walengwa wa kwanza wa Habari Njema ya Wokovu, ni amana na utajiri wa Kanisa. Wao ni dira na ufunguo wa kuingilia mbinguni.”
Alisema pia kuwa inasikitisha kuona kwamba katika baadhi ya Nchi, utamaduni wa kifo unalindwa kisheria, jambo linalokwenda kinyume cha haki msingi za binadamu, utu na heshima yake.
Aliongeza kwamba maisha ya binadamu ni Matakatifu, hivyo yanapaswa kulindwa na kuendelezwa, akisema kuwa utoaji mimba si kitendo cha maendeleo, bali ni ukiukwaji wa haki msingi za binadamu.
Pia, alibainisha kwamba Kanisa linapenda kuwasaidia wanawake kutekeleza vyema dhamana na wajibu wao wa kulea na kutunza vyema watoto, ambao ni zawadi kubwa kutoka kwa Mungu.
Alisema kuwa katika kipindi hiki cha Sherehe za Noeli ambapo sehemu mbalimbali zinapambwa kwa taa na muziki wa Noeli, Waamini na watu wote wenye mapenzi mema, wanapaswa kuonesha furaha pale wanapokutana na wanawake wajawazito, au wale wanaowabeba watoto wao, tayari kumwimbia Mungu utenzi wa sifa na shukrani, kama ilivyokuwa kwa Elizabeti, akisema “Umebarikiwa kuliko wanawake wote, na mzao wa tumbo lako amebarikiwa.”
Alisisitiza kwamba hii inatakiwa iwe ni fursa ya kushukuru na kuwabariki watoto wote wanaozaliwa sehemu mbalimbali duniani.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.