Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Waaswa kukataa kuyumbishwa Kiimani

Baadhi ya Waimarishwa wakiwa katika maandamano kuingia kanisani Parokia ya Mtakatifu Cesilia, Kisarawe ll, Kigamboni, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam. (Picha na Yohana Kasosi) Baadhi ya Waimarishwa wakiwa katika maandamano kuingia kanisani Parokia ya Mtakatifu Cesilia, Kisarawe ll, Kigamboni, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam. (Picha na Yohana Kasosi)

DAR ES SALAAM

Na Mwandishi wetu

Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Henry Mchamungu amewataka Waamini kutokubali kuyumbishwa kiimani.
Askofu Mchamungu alitoa wito huo hivi karibuni katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Sakramenti Takatifu ya Kipaimara iliyofanyika Parokia ya Mtakatifu Cesilia -Kisarawe ll, Kigamboni.
Askofu Mchamungu alisema waamini wanatakiwa kuitangaza Injili kwa watu wote ili wamjue Mungu wa kweli.
“Ndugu zangu, tushike Maandiko Matakatifu… hayo ndio yatatusaidia kuona utukufu wa Mungu,”alisema Askofu Mchamungu.
Kwa upande wa Waimarishwa wa sakramenti hiyo, aliwataka kutambua majukumu yao sis i kuwasimamia watoto hao, bali hata kuwasaidia na kuwaongoza katika misingi thabiti ya kimaadili.
Askofu Mchamungu aliwataka waamini wa parokia hiyo wajenge Kanisa kwa sababu kanisa la sasa ni dogo.
Naye Paroko wa parokia hiyo,Padri Roger Kamuzinzi, aliwaomba waamini kumpa ushirikiano ili aweze kutekeeleza vyema majukumu yake ya kitume.
Padri Kamuzinzi alimshukuru Askofu Mchamungu kwa kuwapatia vijana 31 Sakramenti ya kipaimara.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Parokia hiyo, Geofrey Lyungu alisema parokia hiyo bado changa kwani ina muda wa miezi sita tu tangu ilipotangazwa na Askofu Mkuu Mhashamu Sana Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, kuwa Parokia Kamili.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.