Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Tanzania, Uingereza kuinua Sekta ya Madini

DODOMA

Na Mwandishi wetu

Serikali ya Tanzania imeihakikishia Serikali ya Uingereza kuendeleza ushirikiano kwenye Sekta ya madini, hususan katika kujengea uwezo Watu wake.
Mpango huo unakwenda sanjari na kubadilishana uzoefu, uongezaji thamani madini, na kuwekeza kwenye kufanya utafiti mbalimbali ili kukuza Sekta hiyo na kupanua mnyororo wa thamani,i kuongeza ajira na kuchangia ukuaji Pato la Taifa.
Hayo yalielezwa na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde (pichani), Jijini Dar es Salaam alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza hapa nchini, Mh. Marianne Young.
Katika mazungumzo hayo, Tanzania na Uingereza zimekubaliana katika kuwajengea uwezo Watu wake na kubadilishana uzoefu, hususan katika Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini nchini, Gst.
Aidha, itashirikiana na British Geological Survey, Bgs, ya Uingereza, ili kuwajengea uwezo Watanzania kwa kuwa na ujuzi stahiki katika masuala ya uendelezaji wa Sekta ya Madini.
Mavunde alisema, Uingereza pia imeonesha utayari katika kushirikiana na Tanzania katika eneo la mnyororo mzima wa uongezaji thamani madini, mkakati ambapo Tanzania imejipanga kuhakikisha inavutia uwekezaji mkubwa wa ujenzi wa viwanda vya kuongeza thamani madini hapa nchini.
Naye Balozi Marriane Young, alipongeza jitihada kubwa za kukuza Sekta ya Madini zinazofanywa na Serikali ya Tanzania chini ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, na kuahidi kuimarisha ushirikiano mkubwa baina ya nchi hizo, hasa katika kubadilishana uzoefu na kujengeana uwezo kupitia Taasisi za madini za nchini Uingereza na Tanzania.
Balozi Young ameunga mkono mpango wa uongezaji thamani madini nchini, na kuahidi kwamba Uingereza itashirikiana na Tanzania kwa ukaribu ili malengo hayo yatimie.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.