Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Maliasili na Utalii ni nguzo muhimu ya Uchumi -PM

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa

AUSHA

Na Mwandishi Maalum-PMO

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa, amesema kuwa Sekta ya Maliasili na Utalii ni chanzo kikubwa cha mapato ya Taifa kwa kuwa inahusisha shughuli nyingi za kiuchumi.
Waziri Mkuu Majaliwa alisema kuwa Serikali itaendelea kubuni mikakati ya kuimarisha sekta ya Maliasili na Utalii kwa kuwa sekta hiyo ni nguzo muhimu kwa uchumi wa Taifa.
Alisema hayo wakati alipozindua Tuzo za Uhifadhi na Utalii katika Ukumbi wa Hoteli ya Mt. Meru, jijini Arusha.
“Sekta hii peke yake inachangia asilimia 21.5 katika pato ghafi la Taifa ambapo asilimia 17.2 ni utalii, asilimia 4.3 ni misitu na nyuki,” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.
Aidha, alisema kuwa Sekta hiyo inachangia asilimia 30.9 ya mapato ya fedha za kigeni, ambapo asilimia 25 yanatokana na utalii na asilimia 5.9 ni kutoka misitu na nyuki.
Katika hatua nyingine, Majaliwa alisema kuwa juhudi za dhati na maono makubwa ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika kuiendeleza Sekta ya Maliasili na Utalii, yamesaidia kuongeza idadi ya watalii wa kimataifa kwa asilimia 96 kutoka watalii 922,692 mwaka 2021 hadi watalii 1,808,205, mwaka 2023.
Waziri Mkuu Majaliwa aliiagiza Wizara ya Maliasili na Utalii kuhakikisha inaweka vigezo vya wazi na vinavyojulikana vya uteuzi na upokeaji wa tuzo.
Naye Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dk. Pindi Chana alimpongeza Rais Dk. Samia kwa namna anavyojitoa katika kuhakikisha Sekta ya Maliasili na Utalii inaendelea kukua kwa kasi.
Aliongeza kuwa Wizara hiyo imekuwa na mikakati mbalimbali ya kuimarisha uhifadhi na kuendeleza utalii, ikiwemo kutumia teknolojia mbalimbali pamoja na kuendeleza Programu ya Tanzania – “The Royal Tour” na kuibua mazao mapya ya utalii ili kuongeza idadi ya watalii na mapato yatokanayo na shughuli za utalii.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.