Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Kuhani atahadharisha siasa zisiwagawe Wananchi

Paroko Msaidizi wa Parokia ya Bikira Maria Mshindaji, Jimbo Katoliki la Kigoma, Padri George Muhanuka, akisimika Msalaba kwenye kaburi la marehemu Theresia Nicholaus Massawe. (Picha na Yohana Kasosi) Paroko Msaidizi wa Parokia ya Bikira Maria Mshindaji, Jimbo Katoliki la Kigoma, Padri George Muhanuka, akisimika Msalaba kwenye kaburi la marehemu Theresia Nicholaus Massawe. (Picha na Yohana Kasosi)

MOSHI

Na Mwandishi wetu

Watanzania wametakiwa kutoruhusu Vyama vya Siasa viwagawe na kuwafanya watengane kwa itikadi hizo, kwani sifa kubwa ya Taifa hilo, ni kuwa na amani.
Hayo yalisemwa na Paroko Msaidizi wa Parokia ya Bikira Maria Mshindaji, Jimbo Katoliki la Kigoma, Padri George Muhanuka wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya kumuombea marehemu Theresia Nicholaus Massawe, iliyofanyika Parokia ya Bikira Maria Mpalizwa Mbinguni – Kibosho- Singa, Jimbo Katoliki la Moshi.
Aidha, Padri huyo aliwasihi Waamini kuwa wamoja, huku wakiachana na tabia ya ubinafsi katika imani yao.
“Waamini, tujitahidi kuwa wamoja, tuachane na tabia ya ubinafsi katika imani. Lakini pia Vyama vya Siasa CCM, CHADEMA, au chama chochote kile, visitugawe katika umoja wetu tukiwa Watazania wenye amani,” alisema Padri Muhanuka.
Padri Muhanuka aliongeza kwa kusema, “Ndugu zangu Waamini tujiandae, hatujui muda wala saa tutakapoitwa na Mungu, maana tunakuwa Waamini wa Jumapili tu, wala hatupo kama Waamini wa kuwa na Mungu karibu.”
Padri huyo alisema pia kuwa Theresia Massawe enzi ya uhai wake, aliuishi Ukristo wake kwa imani moja ya Kanisa Katoliki, ambaye pia alikuwa mwanashirika la Moyo Mtakatifu wa Yesu, na alijiunga pia na Shirika la Mtakatifu Anna.
“Je, wewe Mwamini umejiunga na chama gani cha Shirika la Kanisa? Jitathmini Ukristo wako unaoishi kwa sasa, Mungu ametuleta hapa duniani ili tumtambue na tumtumikie, ili siku ikifika, tuwe mahali pa wokovu. Huyu mama aliishi kiukamilifu bila shaka lolote,” alisema Padri huyo.
Alibainisha pia kuwa Waamini wengi hawauishi Ukristo wao kikamilifu, kwa sababu ya kutangatanga katika Makanisa mbalimbali kutafuta miujiza.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.