Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Ishini Neno la Mungu kwa ukamilifu - Padri Kisoka

Paroko Msaidizi wa Parokia ya Kristo Mfalme – Tabata, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Padri Bonaventure Kisoka, akimbatiza mtoto wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Sikukuu ya Somo wa Jumuiya ya Mtakatifu Fabiano, parokiani hapo. (Picha na Yohana Kasosi) Paroko Msaidizi wa Parokia ya Kristo Mfalme – Tabata, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Padri Bonaventure Kisoka, akimbatiza mtoto wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Sikukuu ya Somo wa Jumuiya ya Mtakatifu Fabiano, parokiani hapo. (Picha na Yohana Kasosi)

Dar es Salaam

Na Mwandishi wetu

Wanajumuiya wametakiwa kulishika na kuliishi Neno la Mungu kwa ukamilifu bila kuwa na hofu yoyote katika maisha yao ya kila siku.
Wito huo ulitolewa hivi karibuni na Padri Bonaventure Kisoka, Paroko Msaidizi wa Parokia ya Kristo Mfalme – Tabata, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Sikukuu ya Somo wa Jumuiya ya Mtakatifu Fabiano, parokiani hapo.
“Waamini muwe watu wa kusali kila mnapokutana, kwa sababu ninyi ni Wakrito, mnapoishi kwa umoja msije mkatengana, endeleeni kusali pamoja kama hivi leo mnaposherehekea Sikukuu yenu mmeungana kitu kimoja, hivi ndivyo inavyotakiwa Wakristo,”alisema Padri Kisoka na kuongeza,
“Tambueni kwamba Jumuiya ni kanisa ndogo la nyumbani, mnakuwa Wakrito wenye umoja. Endeleeni kusali pamoja kama hivi kila wakati, mfuateni Mtakatifu wenu wajumuiya, Mtakatifu wenu alikuwa mtu mwema ambaye alimsikiliza sana Mungu, na ninyi muwe watu wema.”
Aidha, aliwasihi kuungana kwa pamoja ili waweze kuwa na furaha katika Jumuiya yao, Kanda, pamoja na Parokia yao ya Kristo Mfalme, kwa ujumla.
Padri huyo aliwasihi Waamini wenye tabia za kujilimbikizia uongozi, waache kufanya hivyo, akisema kwamba baadhi yao wakipata uongozi, wanajiona ndiyo wameshafanikiwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo ya Mtakatifu Fabiano, Alfred Kunambi alisema kuwa kwa sasa Jumuiya yao ni changa ina miezi michache tangu Paroko wa Parokia hiyo awatangaze, bali wanaishi Ukristo wao kwa furaha.
Kunambi aliongeza kuwa mwaka huu mpya, Jumuiya yao imejipanga vyema, hasa katika mavuno ya Parokia na Jimbo, pamoja na kushiriki katika michango mbalimbali wanayoambiwa na Parokia yao.
Hata hivyo, aliwaomba Viongozi wa Vyama vya Kitume kila Parokia na Parokia Teule, kumuunga mkono Askofu Mkuu wa Jimbo hilo, Mhashamu Sana Jude Thaddaeus Ruwa’ichi kwa kutoa michango yao ili kukamilisha ujenzi wa Kanisa Kuu Mbadala la Gezaulole.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.