Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Nyota wa zamani NBA amsifu Papa Fransisko

NEW YORK, Marekani
Mchezaji wa zamani wa NBA na mwanaharakati wa haki za binadamu Enes Kanter Freedom, amesema kuwa Baba Mtakatifu Fransisko ni zaidi ya kiongozi wa kiroho duniani na ishara ya matumaini na amani.
Mchezaji huyo wa Kiislamu alieleza kuwa alianzisha uhusiano wa maana na kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki, jambo ambalo lilimpa msukumo wa kuanzisha kambi ya mpira wa kikapu mjini Vatican, na kuwaleta pamoja watoto wa imani tofauti.
“Michezo huwaleta watu pamoja. Haijalishi historia yako, dini yako, rangi yako, yeyote yule,” Freedom aliiambia NewsNation.
“Tulileta watoto wa Kiislamu, watoto wa Kikristo, watoto wa Kiyahudi, na tulikuwa na wakati mzuri.”
Freedom alikumbuka ushirikiano wake na Papa, ikiwa ni pamoja na wakati ambapo Baba Mtakatifu alipomuomba asimame, ili aone urefu wa mchezaji wa mpira wa vikapu.
“Kila wakati ninapomwona, bila shaka aliweka tabasamu usoni mwangu,” alisema.
Alisema kwamba viongozi kutoka kote duniani wamekuwa wakitoa heshima kwa Papa tangu kifo chake.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.