Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Taratibu za kufuata unapotaka kuandaa marathon

DAR ES SALAAM

Na Arone Mpanduka

Marathon ni mbio za barabarani za umbali mrefu. Kwa mujibu wa sheria za kimataifa za riadha (World Athletics), marathon halisi ni kilometa 42.195.
Nchini Tanzania tunatumia neno ‘marathon’ kwa mazoea kuita tukio lolote la mbio za barabarani, hata kama lina umbali tofauti kama vile kilometa (Fun Run) kwa watu wote, kilometa 10, kilometa 21.1 na kilometa 42.195.
Hata hivyo, kwa mtu ama taasisi inayotaka kuandaa marathon inapaswa kufuata hatua zifuatazo kwa kuzingatia usahihi wake.
WEKA LENGO
Kwa nini unaandaa? Ni kwa ajili ya afya, kuchangisha pesa (charity), kutangaza kampuni au utalii? Lengo hilo litakusaidia kupata vibali na wadhamini.
UNDA KAMATI
Jambo kama hilo huwezi kufanya peke yako, unahitaji watu wa kusaidia maeneo kadhaa ikiwemo fedha na udhamini, logistics na njia ya kukimbia, masoko na usajili na afya na usalama.
BAJETI NA WADHAMINI
Andika bajeti kamili inayojumuisha masuala kadhaa ikiwemo medali, t-shirt, maji, gari la wagonjwa, polisi, mfumo wa kuhesabu muda (timing chips), jukwaa, MC, leseni na kisha tafuta wadhamini.
KIBALI
Hili ni suala muhimu sana kwa sababu lisipofanyika huwezi kuruhusiwa kufanya chochote. Kwa hapa Tanzania unaweza kulitaarifu Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ili waweze kutambua mbio zako rasmi.
Mengineyo ni kuhakikisha kwamba lazima unawasiliana na Manispaa / Halmashauri ya Jiji au mji husika ili kupata kibali husika cha kutumia barabara. Kuwasiliana na Jeshi la Polisi kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani kwa ulinzi na kufunga barabara.

Kuwasiliana na TANROADS/TARURA ikiwa kama unatumia barabara kuu.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.