Dar es Salaam
Na Arone Mpanduka
Klabu ya soka ya Simba imeshindwa kuvunja rekodi yake waliyoiweka wenyewe katika michuano ya ligi ya Mabingwa Afrika kwa muda mfupi ya kufunga mabao mengi zaidi.
Simba ilifanikiwa kuweka rekodi hiyo katika mchezo wao wa hatua ya awali michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mighty Wanderers FC ya Malawi waliowafunga mabao 6-1 katika mchezo ambao Simba walikuwa wenyeji wa mchezo huo.
Ndani ya kipindi cha mwezi mmoja tu klabu ya soka ya Simba imefanikiwa kurejesha tena furaha kwa mashabiki wake kwa kufanikiwa kupata uwiano wa mbao mengi zaidi katika mchezo wa kimataifa na hili ni baada ya kuwagalagaza 15 De Agosto kwa mabao 6-1 katika mchezo wa kwanza wa raundi ya pili ya kufuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2026/27.
Raha zaidi ambazo mashabiki wa klabu hiyo wameipata ni baada mshambuliaji wao raia wa Mali Ibrahim Doumbia kupachika mabao mawaili katika mchezo huo na kuwashangaza wote waliomuona kama kituko akiwa uwanjani.
Ni muda mrefu Doumba hajapachika bao lolote tangu asajili ndani ya klabu hiyo msimu huu na kitendo hicho cha kufunga mabao mawili kimemuongezea uhai ndani yake na hali kubwa ya kupambana.
Hivi karibuni Kocha wa zamani wa klabu hiyo na vilabu mbalimbali Jamhuri Kihwelu “Julio” alisikika akidai kuwa mshambuliaji huyo wa Simba SC, hajui mpira licha ya jitihada za kupambana kutaka kufunga mabao.
Julio alisema kuwa kwa sasa nyota huyo amegeuka kuwa kituko na kichekesho uwanjani kila mara anapopata nafasi ya kucheza na uongozi umeamua kumfumbia macho bila kuelezea ukweli kuhusu usajili wake.











