Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Mungu akithibitisha, hakuna wa kuzuia - Mwinjilishaji

Mwinjilishaji Beatus Kabambe akitoa neno wakati wa Kongamano la Roho Mtakatifu lililofanyika katika viwanja vya Parokia ya Mtakatifu Antony wa Padua – Vigoa, Jimbo Kuu la Dar es Salaam. Mwinjilishaji Beatus Kabambe akitoa neno wakati wa Kongamano la Roho Mtakatifu lililofanyika katika viwanja vya Parokia ya Mtakatifu Antony wa Padua – Vigoa, Jimbo Kuu la Dar es Salaam.

Na Mathayo Kijazi

Kufuatia Kongamano la Roho Mtakatifu lililokuwa likifanyika katika viwanja vya Parokia ya Mtakatifu Antony wa Padua – Vigoa, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwinjilishaji Beatus Kabambe amewakumbusha waamini kwamba Mungu akithibitisha juu ya jambo fulani, hakuna wa kuzuia.
Aliyasema hayo wakati wa Kongamano hilo lililofanyika kwa siku 10 kuanzia Septemba 11 hadi 20, 2026 parokiani hapo.
“Mungu akithibitisha, hakuna wa kuzuia. Mungu akithibitisha, hata wakuloge, hutalogeka. Mungu akithibitisha, hata wakizuia kulia, utatokea kushoto. Mungu akithibitisha, hata wakiziba Mashariki, utatokea Magharibi. Mungu akisema ndiyo, imepita,” alisema Mwinjilishaji Beatus.
Aidha, aliwasihi Waamini wa Vigoa pamoja na wa Parokia za jirani, kuendelea kumwomba Mungu ili athibitishe yale wanayoyaomba katika maisha yao na kwamba yale wanayoyaomba yasiishie tu kwao, bali yathibitishwe na Mungu.
Vilevile, aliwaalika waamini kuongeza nguvu katika kusali na kuombea sadaka zao, kwani kwa kufanya hivyo, itawasaidia kuthibitishwa na Mungu kupitia sadaka hizo.
“Kuthibitishwa kwangu na Mungu kupitia sadaka. Yaani kupata kibali cha Mungu, kupata kwangu ‘Passport’ ya Mungu, kupata kwangu ‘Visa’ ya Kimungu. Wale wanaokwenda nje ya nchi, ili utoke nje ya nchi, mbali na vitu vingine vyote, kitu ambacho unatakiwa uwe nacho pale mpakani ni Hati ya Kimataifa ya Kusafiria.
“Sasa leo tunaongelea kuhusu sadaka. Sadaka nayo pia itazame kwa mtazamo huo, kwamba mbele ya Mungu tunaposafiri kutoka duniani kwenda mbinguni, sanjari na maisha ya Sakramenti, unahitaji pia maisha ya sadaka. Sadaka ione kama Passport, sadaka ione pia kama Visa,” alisema Mwinjilishaji huyo.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.