Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Askofu Mpwaji atoa angalizo kwa wenye ubaridi kiimani

Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhashamu Vincent Mpwaji (kulia) akimkabidhi picha ya Mt. Josefu Paroko wa Parokia ya Mt. Gaspar del Bufalo, Mbezi Beach, Padri Thaddaeus Memba wakati wa uzinduzi wa Jubilei ya Miaka 75 ya Jimbo Kuu la Dar es Salaam ngazi ya Dekania kwa Dekania ya Mt. Thomas More. Katikati ni Dekano wa Dekania hiyo, Padri Romuald Mukandala. Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhashamu Vincent Mpwaji (kulia) akimkabidhi picha ya Mt. Josefu Paroko wa Parokia ya Mt. Gaspar del Bufalo, Mbezi Beach, Padri Thaddaeus Memba wakati wa uzinduzi wa Jubilei ya Miaka 75 ya Jimbo Kuu la Dar es Salaam ngazi ya Dekania kwa Dekania ya Mt. Thomas More. Katikati ni Dekano wa Dekania hiyo, Padri Romuald Mukandala.

Na Mathayo Kijazi

Katika kuzindua Jubilei ya Miaka 75 ya Jimbo Kuu la Dar es Salaam ngazi ya Dekania ya Mtakatifu Thomas More, waamini wamekumbushwa kuitumia nafasi hiyo kuondoa changamoto za ubaridi wa kiimani na kutopokea Masakramenti, huku wakiwa wafariji kwa wenye shida na wanaopitia mazingira magumu katika maisha yao.
Hayo yalisemwa na Askofu Msaidizi wa Jimbo hilo, Mhashamu Vincent Mpwaji, wakati wa homilia yake katika adhimisho la Misa Takatifu ya Uzinduzi huo, iliyoadhimishwa katika Parokia ya Mtakatifu Gaspar - Mbezi Beach, jimboni humo.
“Kwa hiyo ndugu zangu, kupitia nafasi hiyo ya Jubilei ya Miaka 75 ya Jimbo Kuu la Dar es Saalam, tumwombe Mungu ili atuondolee changamoto mbalimbali tulizonazo, hasa za ubaridi wa kiimani na kutopokea Masakramenti,” alisema Askofu Msaidizi Mpwaji.
Askofu huyo aliwakumbusha waamini kuitumia Jubilei hiyo kama fursa ya kuimarika kiimani, kimaadili, kiutume na hata katika Umisionari wao.
Alitumia nafasi hiyo kuwasisitiza kila mmoja ndani ya Dekania hiyo, kuimarika katika umoja na uthabiti kama familia ya Mungu katika Kanisa mahalia jimboni humo, huku wakiwa chachu ya kuleta upyaisho ndani ya Jimbo lao.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.