Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Watoto wa kiume wako hatarini, walindwe - Askofu

Waamini wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam wakiwa katika adhimisho la Misa Takatifu ya Warsha iliyoadhimishwa katika viwanja vya Kristo Mfalme, Tabata jimboni humo. Waamini wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam wakiwa katika adhimisho la Misa Takatifu ya Warsha iliyoadhimishwa katika viwanja vya Kristo Mfalme, Tabata jimboni humo.

Na Violet Tillya

Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mhashamu Henry Mchamungu, amelitaka Kanisa Katoliki nchini kuamka kifikra na kuwazingatia zaidi watoto wa kiume katika suala la malezi na makuzi, akisema hali yao kwa sasa ni ya kutisha na inahitaji hatua za haraka.
Alisema hayo hivi karibuni wakati akitoa homilia katika adhimisho la Misa Takatifu kwenye warsha ya walei ya Jimbo Kuu la Dar es Salaam, iliyofanyika katika Parokia ya Kristo Mfalme, Tabata.
Alisema watoto wa kiume wameonekana kusahaulika na kutopatiwa kipaumbele katika baadhi ya maeneo ya jamii, tofauti na watoto wa kike ambao kwa mujibu wake, wamekuwa wakisaidiwa zaidi na kushika nafasi za mbele katika shughuli mbalimbali.
Askofu Mchamungu alisema hali hiyo imechangia baadhi ya watoto wa kiume kupoteza kujiamini ikilinganishwa na watoto wa zamani, jambo ambalo linaweza kuathiri maendeleo yao na nafasi yao katika jamii.
Warsha hiyo ilihudhuriwa na mamia ya walei wa Jimbo hilo, ambao pia walipatiwa mada mbalimbali zilizowasilishwa na Padri Prosper Kessy na Padri Rogatian Msafiri baada ya kumalizika kwa Misa, kwa lengo la kukuza maisha yao ya kiroho na maendeleo kwa ujumla.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.