Vijana Waimarishwa wa Sakramenti Takatifu ya Kipaimara wa Parokia ya Bikira Maria Mama wa Rozari Takatifu, Makongo Juu, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, wakiwa kanisani wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya kutoa Sakramenti hiyo.
Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Henry Mchamungu, akiwa katika picha ya pamoja na Mapadri na vijana waliopokea Sakramenti Takatifu ya Kipaimara katika Parokia ya Mtakatifu Rita wa Kashia – Temboni, jimboni humo, baada ya Adhimisho la Misa Takatifu. Kulia kwa Askofu, ni Paroko wa Parokia hiyo, Padri Festo Ngonyani. (Picha na Mathayo Kijazi)
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi akimbariki mtoto katika Parokia ya Bikira Maria Mama wa Rozari Takatifu, Makongo Juu, wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Kipaimara iliyoadhimishwa parokiani hapo. Kulia kwa Askofu Mkuu, ni Paroko wa Parokia hiyo, Padri Joseph Massenge, na aliyesimama ni Paroko Msaidizi wa Parokia hiyo, Padri Canisius Hali.
Watoto wa Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu wa Parokia ya Mwenyeheri Antonio Rosmini, Mpiji Magoe, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, wakiwa kanisani wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Kipaimara. Kushoto aliyesimama ni Mlezi wa Shirika hilo, Krista Kimalio.
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, akiwa katika picha ya pamoja na Mapadri na Viongozi wa Halmashauri ya Walei wa Parokia ya Bikira Maria Mama wa Rozari Takatifu, Makongo Juu jimboni humo, wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Kipaimara iliyoadhimishwa hivi karibuni parokiani hapo. (Picha zote na Yohana Kasosi).
Vijana Waimarishwa wa Parokia ya Mwenyeheri Antonio Rosmini, Mpiji Magohe, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, wakiwa kanisani wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Sakramenti Takatifu ya Kipaimara iliyoadhimishwa hivi karibuni parokiani hapo.
Waamini wa Parokia ya Bikira Maria Mama wa Rozari Takatifu, Makongo Juu, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, wakiwa kanisani wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Kipaimara iliyoadhimishwa parokiani hapo hivi karibuni.
Waamini wa Parokia ya Mtakatifu Maria De Mathias, Mivumoni, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, wakiwa kanisani wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Dominika.
Wasimamizi wa Zaka wa Parokia ya Bikira Maria wa Mlima Karmeli, Bunju Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, wakiwa kanisani wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Dominika.
Waamini wa Parokia ya Mwenyeheri Antonio Rosmini, Mpiji Magohe, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, wakiwa kanisani wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Sakramenti Takatifu ya Kipaimara iliyoadhimishwa hivi karibuni parokiani hapo.
Wanakwaya wa Parokia ya Bikira Maria Mama wa Rozari Takatifu, Makongo Juu Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, wakiwa katika picha ya pamoja baada ya Adhimisho la Misa Takatifu ya Sakramenti Takatifu ya Kipaimara iliyofanyika parokiani hapo hivi karibuni. (Picha zote na Yohana Kasosi)
WASHINGTON, America
Nahodha wa timu ya Taifa ya Wales, Aaron James Ramsey, ambaye pia ni kiungo wa klabu ya Cardiff City inayoshiriki EFL Championship nchini Uingereza, amesema kuwa anaamini kwamba kuna nyakati za kusisimua mbele kwa Wales chini ya Kocha Mkuu wake mpya, Craig Bellamy.
Wales ilimteua mshambuliaji wa zamani Bellamy kwa mkataba wa miaka minne mwezi Julai, baada ya kumfuta kazi Rob Page mwezi Juni.
Kiungo wa kati wa Cardiff City Ramsey, 33, alicheza pamoja na Bellamy kwa klabu na nchi na anamuunga mkono kocha msaidizi wa zamani wa Burnley na Anderlecht, kustawi katika nafasi yake mpya.
Bellamy mzaliwa wa Cardiff, alishinda mechi 78 za Wales na kuwa nahodha wa timu kati ya 2007 na 2010, akarithiwa na Ramsey wakati huo akiwa kiungo wa Arsenal akiwa na umri wa miaka 20 pekee.
Baadaye Ashley Williams na Gareth Bale walivaa kitambaa kwa Wales kabla ya Ramsey kupewa jukumu tena baada ya kustaafu kwa Bale Januari mwaka 2023.
“Nimefurahi sana. Nimemfahamu Craig kwa miaka kadhaa sasa na nimefurahishwa naye, nina hakika atakuwa na mafanikio ya kweli. Ukiangalia timu alizoshiriki nazo na jinsi walivyocheza, kushinikiza juu, ukali, kudhibiti mchezo nadhani Wales wana mengi ya kutarajia natumai kuna nyakati za kusisimua mbeleni,” alisema Ramsey.
BARNSLEY, Uingereza
Mwingereza Molly Caudery ameondolewa katika kufuzu fainali ya mbio za kupokezana vijiti katika Michezo ya Olimpiki inayoendelea jijini Paris, Ufaransa ya mwaka huu 2024.
Caudery, bingwa wa dunia wa ndani ambaye aliweka rekodi ya Uingereza ya mita 4.92 katika hafla hiyo mwezi Juni mwaka huu, alishindwa kuvuka mita 4.55 katika uwanja wa Taifa wa Ufaransa wa mpira wa miguu, Stade de France.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 alitarajiwa kuonyeshwa vyema kwenye michezo hiyo baada ya mwaka mzuri ambapo amerekodi kanda tisa bora za kibinafsi.
Pia, alishinda shaba kwenye Mashindano ya Uropa mwezi Juni, na kumaliza wa tano kwenye Mashindano ya Dunia ya mwaka jana.
Mwanariadha wa zamani wa Uingereza wa mbio za mita 400, Katharine Merry alisema kuwa huo ni mshtuko mkubwa wa mashindano ya Olimpiki hadi sasa.
“Molly Caudery amekwenda juu ya urefu wa 4.92m [msimu huu] - 4cm juu kuliko mtu mwingine yeyote duniani,” alisema Merry.
DAR ES SALAAM
Na Ibrahim Mkamba
Tanzania ina wawakilishi wanne kwenye mashindano makubwa ya soka Afrika. Young Africans, (nitakaowataja baadaye Yanga), na Azam FC watatuwakilisha kwenye ligi ya mabingwa Afrika, huku Simba na Coastal Union wakituwakilisha kwenye mashindano ya kugombea ubingwa wa Kombe la Shirikisho Afrika.
Makala hii inaongelea hatari ya timu kujiamini kupita kiasi au kuelezewa ubora wao kupita kiasi dhidi ya wapinzani wao, tena kwa kauli zinazowafikia wapinzani hao. Hii ipo kwa Yanga na Simba, na si kwa Azam FC na Coastal Union, na ndiyo sababu makala hii itaziongelea tu timu hizo za Kariakoo, Dar es Salaam.
Ukweli haupaswi kupingika kwamba, ukisahau kucheza nusu fainali ya mashindano ya kugombea ubingwa wa Afrika mwaka 1974 kwa mfumo wa mtoano mwanzo mwisho, sahau kucheza fainali ya mashindano ya CAF mwaka 1993 na potezea kuivua ubingwa wa Afrika Zamalek ya Misri na kutinga makundi kuwania ubingwa wa Afrika mwaka 2003, tangu mwaka 2018 mpaka sasa, Simba imekuwa moja ya timu za Afrika ya kufika hatua ya robo fainali katika mashindano makubwa ya soka ya Afrika kwa mfululizo.
Ukiiondoa Al Ahly ambayo kwao kubeba ubingwa wa Afrika si habari tena, timu nyingi kubwa za bara hili zimeshindwa kufikia hatua hiyo mfululizo miaka hii. Kuna zilizopotea kipindi fulani kama Zamalek, Esperance de Tunis, Raja Athletic Club, TP Mazembe na nyinginezo kubwa. Kwa hiyo walichofanya Simba si kidogo bali ni kikubwa kinachofanya wastahili sifa. Timu kuwa na uimara ule ule kwa misimu mitano mfululizo, ni jambo kubwa.
Yanga wamekuwa na historia ya kusifika kwenye mashindano ya Afrika tangu 1969 walipotolewa kwenye hatua ya robo fainali kwa kura ya shilingi jijini Dar es Salaam na Asante Kotoko ya Ghana ya kipa wao Robert Mensah, na mkali wa mabao Ibrahim Sunday.
Ni Yanga ndiyo ilikuwa ya kwanza kucheza hatua ya makundi mashindano ya ligi ya mabingwa Afrika mwaka ule ule 1998 utaratibu huo ulipoanzishwa. Wakafika fainali Shirikisho Afrika msimu wa 2023/2024 na msimu uliomalizika waliishia robo fainali Afrika. Kwa sasa Yanga ni moja ya timu tishio Afrika. Hili si la kubishaniwa.
Pamoja na ukubwa walionao Yanga na Simba kwa sasa, hiyo haimaanishi watazishinda timu zote, za hadhi zozote, nyakati zote. Kama Simba walivyoifunga Al Ahly Dar es Salaam mechi mbili miaka hii ya karibuni kwa ushindi wa 1-0 kila mechi, magoli ya Meddy Kagere na Luis Miquissone ya mechi hizo tofauti, ndivyo Uhamiaji Zanzibar au wawakilishi wa Libya wanavyoweza kuitupa Simba nje ya mashindano ya Kombe la Shirikisho hatua ya awali.
Kama Yanga ilivyoipiga CR Belouizdad 4-0 jijini Dar es Salaam, ndivyo Vital’O inavyoweza kuishinda Yanga na kuitupa nje ya mashindano kwenye hatua ya awali. Yanga inaweza kupenya hapo kisha kukwama kwa SC Villa ya Uganda, au Commercial Bank ya Ethiopia.
Natoa tahadhari hizo kutokana na kauli ya kujirudiarudia ya Afisa Habari wa Yanga na ya wachambuzi kadhaa wa soka kwamba Yanga itabeba ubingwa wa soka wa Afrika msimu huu. Kwa upande mwingine, kuna baadhi ya wachambuzi wa soka husema Simba itabeba ubingwa wa Kombe la Shirikisho. Angalau kwa upande huo, Afisa Habari wa Simba hajawahi kutamba hivyo. Afadhali kwa Yanga iliyo kamili tangu msimu wa 2023/2024, lakini Simba iko kwenye matengenezo.
Madhara ya kauli za kuzipaisha Yanga na Simba kwenye ushiriki wao wa mashindano ya Afrika ni, kwanza, zinawafanya wachezaji wao wawe kwenye shinikizo kubwa wakutanapo na timu wanazoaminishwa kuwa dhaifu. Vichwani mwao hujiuliza itakuwaje wakishindwa kuwashinda wadogo hao? Kucheza kwa shinikizo, si jambo salama kwenye soka.
Pili, timu zetu zitaziendea mechi hizo katika hali ya kama kwamba zimeshashinda kwa jinsi zinavyopotoshwa. Hivyo, watabweteka, na wakishtuka tu, mambo tayari yameshakuwa magumu. Zaidi soma Tumaini Letu