Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

TEC: Vijana mpiganie Taifa

Baadhi ya vijana kutoka shule mbalimbali za Sekondari na Vyuoni wakisikiliza mada wakati wa Kongamano la Vijana lililofanyika katika Chuo cha ufundi Don Bosco, Oysterbay, Jijini Dar es salaam. Baadhi ya vijana kutoka shule mbalimbali za Sekondari na Vyuoni wakisikiliza mada wakati wa Kongamano la Vijana lililofanyika katika Chuo cha ufundi Don Bosco, Oysterbay, Jijini Dar es salaam.

DAR ES SALAAM

Na Laura Chrispin

Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padri Dk. Charles Kitima, amewaasa vijana watambue kuwa wao ni Taifa la leo na si taifa la kesho, akiwasihi kuwa na uchungu na taifa lao.
Padri Kitima alisema hayo hivi karibuni katika Kongamano la Vijana lililofanyika katika Chuo cha ufundi Don Bosco, Oysterbay, Jijini Dar es salaam.
“Unatakiwa kuwa na uchungu na taifa lako kwa kuitambua vyema nchi yako ya Tanzania pamoja na ‘focus’ yaani nchi inapolenga kwa ajili ya maendeleo ya uchumi huku ukifahamu malengo ya viongozi”. Alisema
Alikumbusha kipindi cha nyuma ambapo kulikuwa na sera kama Tanzania ya viwanda au Kilimo kwanza lakini cha ajabu kwa sasa hakuna focus yeyote ya nchi ambayo itasaidia katika maendeleo.
Hata hivyo Padri Kitima alisema kuwa unapojengewa ‘physical skills’ unapewa mbinu ya kujitambua kama Mtanzania ni vyema kutumia maarifa ili uweze kufikia malengo ya nchi.
Mbali na hayo alizungumzia‘Development plan’ ya Hayati Rais Benjamin Mkapa iliyolenga kwa kila mtu kujitegemea, Mkapa aliwekeza katika kuanzisha taasisi zilizoweza kumuongoza katika sheria kama Tanroads, Takukuru, Tanzania Revenue Authority na zingine nyingi ambazo aliweza kusaidiana nazo katika kuingoza nchi”.
Vilevile Padri Kitima alisema nchi yetu imelenga kwa vijana ili kutoa taarifa zilizo sahihi kwa kuwasimulia matukio ya nyuma kwani 1884-1885 kulitokea na tukio kubwa ambalo lilibadili siasa zote za Tanzania ambalo ni Mkutano wa Berlin ambao uliligawa bara la Afrika na kuunganishwa na makoloni mengine ya ujerumani na kuanza kutumia siasa ya pamoja.
Hata hivyo alieleza kuwa hapo ndipo ushirikiano wa makabila ulianza kwani waliwekwa pamoja na kuanza kazi kwa umoja japo wajerumani walikuwa na lengo la kuwanyonya waafrika.
Padri Kitima alisema Tanzania ina wawekezaji wengi wa nje kuliko wa ndani lakini India wawekezaji wao wengi ni wahindi ambao wanasaidia mapato yao yasiende mbali bali yazunguke ndani ya taifa lao kutokana na wawekezaji wao.
Pia aliwataka vijana watambue kuwa Marekani matajiri wazawa ndiyo wanao ikopesha serikali na kusema inasikitisha kwa Tanzania hakuna hata Mzawa mmoja anayeimiliki hoteli kubwa kwani waliokuwa wakimiliki kipindi cha nyuma wamezibinafsisha kwa sera ya kusema hawawezi kuziendesha.
Padri Kitima aliwataka vijana kuwa na malengo na jambo Fulani kwa kuiga mfano wa Rais Obama wa kutamani kuongoza Marekani na lengo lake kutimia hivyo basi aliwaasa vijana kuwa na ndoto ya siku moja kuja kuondoa mfumo wa chama kimoja bungeni na kuruhusu vyama vingi.
Aliendelea kusema aliyepita kwa wizi wa kura hawezi kuwatetea wananchi wake, na kuwataka vijana kukataa dhambi ya kuchukua pesa kwa ajili ya kutangaza majibu ya uwongo wakati wa uchaguzi.
Aliwataka vijana kutoruhusu nchi ya vyama vingi kutawaliwa na chama kimoja kwa kusema kitashika serikali na bunge hata mahakama itashindwa kufanya kazi yake kwa haki.
Padri Kitima alisema vijana wanawajibika kuamka sasa kabla hawajaingia maofisini na baadaye kuanza kulia machozi wakati watu hao wameanza majukumu.
Alitoa wito kwa vijana kuchagua kiongozi muwazi na muwajibikaji ili aweze kutekeleza wajibu kwa haki.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.