Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Unyenyekevu, hekima ni fadhila za Kimungu-Padri

Paroko Msaidizi wa Parokia ya Kristo Mfalme – Tabata, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Padri Bonaventura Kissoka, akimwombea marehemu Mzee Michael Lesio Kissoka (baba yake mzazi), wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya kumwombea marehemu huyo, katika Parokia ya Mtakatifu Anna – Kirima, Jimbo Katoliki la Moshi. (Picha na Mathayo Kijazi) Paroko Msaidizi wa Parokia ya Kristo Mfalme – Tabata, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Padri Bonaventura Kissoka, akimwombea marehemu Mzee Michael Lesio Kissoka (baba yake mzazi), wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya kumwombea marehemu huyo, katika Parokia ya Mtakatifu Anna – Kirima, Jimbo Katoliki la Moshi. (Picha na Mathayo Kijazi)

MOSHI

Na Mathayo Kijazi

Wakristo wametakiwa kuwa wanyenyekevu na wenye hekima katika maisha yao, kwani hiyo itawasaidia kuishi maisha yanayompendeza Mungu.
Hayo yalisemwa na Padri Festo Tingo wakati wa homilia yake katika Misa Takatifu ya kumwombea marehemu Mzee Michael Lesio Kissoka, baba mzazi wa Padri Bonaventura Kissoka AJ, Paroko Msaidizi wa Parokia ya Kristo Mfalme – Tabata, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, iliyoadhimishwa katika Parokia ya Mtakatifu Anna – Kirima, Jimbo Katoliki la Moshi.
Padri Tingo aliwasihi Waamini walioshiriki katika Adhimisho hilo, kuiga mfano wa maisha ya Mzee Kissoka, yakiwemo ya unyenyekevu na kuwajibika, kwani ni katika jitihada tu ndipo wanafanikiwa.
“Ukimya ni jambo lenye tafsiri nyingi katika maisha ya binadamu, ambapo pia ndani yake ukimya huashiria busara. Mzee Kissoka alikuwa mkimya, mnyenyekevu, mwenye busara, na mwenye kupenda kusali. Kwa hiyo ndugu zangu, ni vema kila mmoja akatumia muda wake vizuri kufanya matendo yaliyo mema, kwa sababu kwa kufanya hivyo, mtakuwa mmeitengeneza njia ya kwenda mbinguni,” alisema Padri Tingo.
Alisema pia kwamba hata kama Mzee huyo amefariki, bali watoto pamoja na ndugu kwa ujumla, wasiache kwenda kusalimia, kwani Kirima bado ina watu wanaostahili kwenda kusalimiwa.
“Usiseme kwamba siendi tena Kirima kusalimia kwa sababu mzee wangu hayupo, hapana. Endelea kuja kusalimia kwa sababu Wanakirima wapo, na Kirima ipo,” alisema Padri huyo.
Kwa upande wake Padri Bonaventura Kissoka aliwashukuru Mapadri wenzake, Waamini kutoka Majimbo mbalimbali, pamoja na watu wengine kwa kushiriki na kuwafariji katika msiba huo.
Padri Kissoka alisema kuwa wao kama familia, wanamshukuru Mungu kwa maisha ya baba yao kwa kuwalea katika misingi iliyo bora, ikiwa ni pamoja na kuwasomesha.
Akisoma wasifu wa marehemu, Michael Kissoka ambaye ni mjukuu wa Mzee Michael Lesio Kissoka, alisema Mzee huyo alizaliwa Septemba 26 mwaka 1926, Kibosho - Kirima Kati, Wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro. Alipata elimu ya watu wazima mwaka 1954, pamoja na elimu ya ufundi seremala na udereva.
Aliongeza kuwa Mzee huyo aliwafundisha kusali, kwani alipenda kusali kabla ya kufanya chochote, desturi ambayo aliipata kwa Masista, ambapo kwa kuishi hivyo, alijenga familia ya maisha ya sala, jambo lililomfanya kuwahimiza watoto wake kuwa na desturi ya kusali kila mara.
Kuhusu ugonjwa, mjukuu huyo alisema kwamba babu yake hakuwahi kusumbuliwa na ugonjwa wowote katika utu uzima wake hadi mwaka 2015, ambapo alikabiliwa na tatizo la koo na kuanza matibabu katika hospitali ya KCMC iliyopo mjini Moshi, mkoani Kilimanjaro, na baadaye kupata matibabu zaidi katika hospitali ya OCEAN ROAD, Dar es Salaam baada ya kugundulika kuwa na saratani ya koo.
Aliendelea kusema kuwa mwezi Juni mwaka 2015, alipatiwa matibabu katika mji wa Ahmedabad nchini India, na baadaye aliendelea na matibabu katika klinik ya BESTA iliyopo Kinondoni Dar es Salaam, ambapo baada ya vipimo, alionekana kupona ugonjwa huo, na hivyo kuendelea na maisha yake kama kawaida.
Marehemu Mzee Michael Lesio Kissoka aliyefariki dunia Jumamosi Novemba 2 mwaka 2024 siku ya kuwakumbuka na kuwaombea Waamini Marehemu Wote; ameacha watoto.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.