Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

‘Bila Mungu hakuna mafanikio’

Watawa na Waamini wakiwa kanisani wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Sakramenti Takatifu ya Kiapaimara iliyoadhimishwa katika Parokia ya Mtakatifu Yakobo Mkuu Mtume – Kijitonyama, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam. Misa hiyo iliongozwa na Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo. (Picha na Yohana Kasosi) Watawa na Waamini wakiwa kanisani wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Sakramenti Takatifu ya Kiapaimara iliyoadhimishwa katika Parokia ya Mtakatifu Yakobo Mkuu Mtume – Kijitonyama, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam. Misa hiyo iliongozwa na Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo. (Picha na Yohana Kasosi)

DAR ES SALAAM

Na Mathayo Kijazi

Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, ametoa wito kwa Vijana wanaopokea Sakramenti Takatifu ya Kipaimara, kumweka Mungu maanani siku zote za maisha yao.
Kardinali aliyasema hayo wakati wa homilia yake katika Adhimisho la Misa Takatifu iliyoambatana na Sakramenti hiyo katika Parokia ya Mtakatifu Yakobo Mkuu Mtume – Kijitonyama, jimboni humo.
“Wanakipaimara tambueni kwamba katika maisha yenu ni lazima mumuweke Mungu Mwenyezi maanani. Na ndilo Neno lililotukusanya leo hapa, mlipotualika tuje kuadhimisha, kushuhudia adhimisho lenu la Sakramenti ya Kipaimara, ni ninyi mmetualika. Huwa hamumwoni Askofu anakuja hapa kanisani, lakini ni kwa sababu yenu ninyi mnaopokea Sakramenti ya Kipaimara, mimi niko hapa…
“… na hawa wote waliopo hadi Wanakwaya, huwa wanakuwepo sawa, lakini kwa leo ni kwa sababu yenu kuonyesha kwamba tunaweka maanani tendo mnalolifanya siku hii ya leo. Ni tendo kubwa lenye manufaa, siyo kwenu tu, ni tendo kubwa ambalo mnalifanya kwa niaba ya Kanisa zima. Kwa hiyo tunawaombea kwa Mungu Mwenyezi atekeleze maombi yanayokuwa ndani ya moyo wa kila mmoja wenu,” alisema Kardinali Pengo.
Aliongeza kwamba hakuna mwanadamu anayeweza kufanya kitu na kufanikiwa bila kumtanguliza Mungu, akisisitiza kuwa kila mmoja ahakikishe anamtanguliza Mungu katika mipango yake.
Sambamba na hayo, Kardinali alitoa mfano wa watu waliotaka kujenga mnara mrefu ili wakamwone Mungu mbinguni, na kwamba Mungu hakuona wivu juu ya maamuzi hayo, bali lengo ni kuwaonyesha kuwa hakuna kitu kinachofanywa na mwanadamu bila kumweka Mungu maanani.
“Waliotaka kujenga mnara ili uwe kumbukumbu yao hata kama hawapo, Mungu Mwenyezi alipogundua kwamba hawa watu wanataka kujenga kitu cha namna hii, akaamua kuwachanganya kwa lugha, hawakuweza kuelewana tena; mmoja akitumwa na mwenzake lete jiwe, yeye analeta maji; naomba mchanga, yeye analeta maji, kwa hiyo hawakuweza kuendelea kwa sababu hawaelewani tena…
“Si kwamba Mungu Mwenyezi aliwaonea wivu kwamba watafanya kitu kikubwa hivyo, lakini Mwenyezi alitaka kumwonyesha mwanadamu kwamba ‘ukitaka kufanya kitu chochote bila kuniweka mimi Mungu maanani, haiwezekani, hutafanikiwa,” alisema Kardinali Pengo.
Vile vile, alitoa wito kwa Vijana waliopokea Sakramenti Takatifu ya Kipaimara katika Adhimisho hilo, pengine wana mipango mikubwa iliyopo katika maisha yao, bali watambue kwamba hawataweza kufanikiwa bila kumweka Mungu mbele.
Aliwasisitiza kufahamu kuwa hakuna anayeweza kuwazuia kupanga mipango, hasa ya kimaendeleo maishani mwao, bali wakumbuke kwamba bila kumweka Mungu maanani, hakuna kitakachofanikiwa.
Wakati huo huo, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo aliwakumbusha Vijana hao kuendelea kuishi maisha yanayompendeza Mungu, kwani hayo ndiyo yatakayowasaidia kupokea baraka katika kila wanaloliomba kwake.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.