Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Wasimamizi Vijana wa Kipaimara wapewa somo

Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Henry Mchamungu (aliyekaa), akitoa Sakramenti ya Kipaimara kwa mmoja kati ya Waimarishwa 185 wa Parokia ya Mtakatifu Bonaventura, Kinyerezi, jimboni humo wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Dominika ya Pili ya Majilio ya Mwaka C wa Kanisa. (Picha na Jackson Njau) Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Henry Mchamungu (aliyekaa), akitoa Sakramenti ya Kipaimara kwa mmoja kati ya Waimarishwa 185 wa Parokia ya Mtakatifu Bonaventura, Kinyerezi, jimboni humo wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Dominika ya Pili ya Majilio ya Mwaka C wa Kanisa. (Picha na Jackson Njau)

DAR ES SALAAM

Na Joyce Sudi

Wasimamizi wa Vijana Waimarishwa wametakiwa kuwasimamia vizuri ili waweze kukua kiimani na kimaadili.
Rai hiyo ilitolewa hivi karibuni na Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Henry Mchamungu katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Dominika ya Pili ya Majilio ya Mwaka C wa Kanisa, sambamba na utoaji wa Sakramenti ya Kipaimara kwa Waimarishwa 185 wa Parokia ya Mtakatifu Bonaventura, Kinyerezi, jimboni humo.
Askofu Mchamungu alisema Wasimamizi wa Ubatizo na Kipaimara, wanalo jukumu la kusimamia watoto ili wakue kiimani hadi watakapokuwa watu wazima.
Kwa mujibu wa Askofu Mchamungu, Waimarishwa hao wa  Sakramenti Takatifu ya Kipaimara wanapaswa kuwa na mahusiano mazuri na Wasimamizi wao, na wanapopata nafasi, wanatakiwa kwenda  kuwasalimia.
Aidha aliwasihi Waimarishwa hao, kuendelea kusali na Waamini wenzao katika makusanyiko ya kanisani na Jumuiya, kwa kuwa wapo baadhi wakishapata Sakramenti hiyo, hawaonekani tena kwenye nyumba za ibada.
“Kila mtu anajua kuwa hataishi milele, hivyo mjitahidi kutubu kila wakati, na kuishi vizuri ili inapofikia siku ya mwisho, msiwe na mateso na mahangaiko,”alisema Askofu Mchamungu.
Alibainisha pia kwamba kwa bahati mbaya, ufahari wa dunia hii hawaondoki nao, wahangaikie roho zao kwa kuwa na mahusiano mazuri na Mwenyezi Mungu.
Askofu Mchamungu aliwataka Waimarishwa hao kabla hawajatoka kitandani wamshukuru Mungu na kuomba Baraka zake, na wajibiidishe katika shughuli mbalimbali.
Akizungumzia kuhusu utunzaji mazingira, Askofu Mchamungu alisema kuwa vijana hao na Waamini kwa ujumla, wanatakiwa kutunza mazingira, kupitia Waraka wa Baba Mtakatifu Fransisko wa Laudato Si.
Kwa upande wake, Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Bonaventura, Kinyerezi, Padri Francis Hizza, alisema kuwa neema waliyoipata Waimarishwa hao, ni kubwa, hivyo wanapaswa kumshukuru Mwenyezi Mungu,wazazi na walezi wao, pamoja na Wasimamizi ambao wamekubali kubeba dhamana ya kuwakuza kiroho.
Padri Hizza alisema kwamba wazazi wanatakiwa kuwahimiza watoto wao kwenda kanisani ili waweze kukua vyema kiroho, kiakili na kimwili, kwani mafanikio yoyote,  ikiwemo ya elimu kwani vyote hivyo chanzo chake  ni Mungu.
Aidha, amewataka Waamini wanaposubiria kuzaliwa kwa Bwana Yesu Kristo, wajitayarishe na wafurahie ndani ya mioyo yao, wakijua kwamba anayekuja ni Mfalme na mwenye uweza wa yote.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.