KASESE, Uganda
Padri Raphael Balinandi Kambale ameadhimisha Jubilei ya Dhahabu katika Parokia ya Nsenyi, Jimbo Katoliki la Kasese nchini Uganda, akiwasihi Mapadri vijana na Wakristo kwa ujumla, kujenga upendo kwa Kanisa, na kujitolea kwa ajili ya Miito.
Padri Balinandi, ambaye kwa sasa ni Padri mzee zaidi katika Jimbo Katoliki la Kasese, alipewa Daraja Takatifu la Upadri, Desemba 14 mwaka 1974 katika Parokia ya Nsenyi na Askofu Vincent J. McCauley, mbele ya Askofu Sarapio Magambo na Askofu Kathaliko Emmanuel, kutoka Jimbo Katoliki la Butembo-Beni.
Yeye alikuwa Padri wa tatu kutoka Jimbo Katoliki la Kasese, akifuatiwa na Monsinyori Augustine Muhindo Hayati, aliyepewa Daraja la Upadri wa kwanza mwaka 1958 na Padri Louis Isingoma Byakuyamba mwaka 1972.
Katika hotuba yake muda mfupi baada ya Misa iliyoongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Kasese, Mhashamu Francis Aquirinus Kibira Kambale, Padri Balinandi alitajwa kuwa mtu wa thamani katika Jimbo na Wilaya kwa ujumla, ambaye amechangia maendeleo ya kiroho, kitamaduni na mazingira.
Askofu Francis Kibira alisema kuwa Ndoa Takatifu inachukuliwa kuwa ni Sakramenti yenye nguvu katika Kanisa Katoliki ambayo wanandoa wanapaswa kuilinda kwa wivu kwa sababu ni mfugaji wa Sakramenti nyingine.
Vile vile, Askofu Kibira ambaye alitoa wito wa mafunzo ya Katekesi miongoni mwa watoto, alisema kwamba ili Kanisa liwe na Mapadri wazuri na wanandoa miongoni mwa Miito mingine kanisani, wazazi wanatakiwa kuwa na sababu na kuweka thamani katika ndoa ili kuwalea watumishi makini wa Kanisa na Jumuiya.
Katika ujumbe wake, Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Gulu, Mhashamu John Baptist Odama, mwanafunzi mwenza wa Padri Balinandi, alirejea maelezo ya watu wengine kuhusu Padri, kwamba yeye ni mtu mwenye imani kubwa kuhusu maisha kama Kasisi.
Mbali na hilo, aliendelea kwa kusema, “Nina kumbukumbu zake za kuwa na shauku kubwa ya liturujia, na kutamani sana kufuata kanuni za kiliturujia na Neno la Mungu.”
Askofu Mstaafu wa Jimbo Katoliki la Kasese, Mhashamu Egidio Nkaijanabwo alisema kuwa Padri Balinandi alikuwa mtu wa mila nzuri, na alipenda utamaduni wake.
Kupitia utamaduni wake, kujifundisha, na kupitia elimu yake zaidi, Padri Balinandi ameonekana kuwa na ujuzi katika lugha ya Lhukonzo.
Miongoni mwa umahiri mwingine, alitafsiri vitabu vingi vya kiliturujia katika lugha ya kienyeji, zaidi ya yote aliyoheshimu Ufalme wake.
Katika mahubiri yake, Padri Expedito Masereka, Msimamizi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Bukangara, aliwataka Wakristo kujifunza kutoka kwa Padri Balinandi kujiendeleza kiujumla kwa kuanza na wao wenyewe.
Mratibu huyo wa zamani wa Kichungaji, alimpongeza mshereheshaji huyo kwa michango yake ya umoja, na kukuza lugha ya Lhukonzo, kazi inayowalazimu Wakristo katika Miito mingine kutimiza wajibu wao kwa umakini na matumaini, kama inavyotarajiwa hadi mwisho.
Mjubilei huyo, Padri Balinandi Kambale akiwa na furaha tele, alimpongeza Askofu Kibira kwa upendo na matunzo katika uzee wake, akisema kuwa aligubikwa na upendo, ukarimu na uangalizi alioonyeshwa na Wakristo, na watu wema.
Naye Mkuu wa Walei wa Jimbo Katoliki la Kasese, George Mayinja, aliwataka wazazi kuwalea watoto wao kulingana na huduma ya Kanisa, lakini pia kuwekeza katika Elimu yao.