KARONGA, Malawi
Chama cha Wanawake Wakatoliki (Catholic Women Association: CWA) nchini Malawi, kimefanya Mkutano Mkuu wa 45 wa Mwaka kuanzia Desemba 18–22 mwaka huu.
Mkutano huo ulifanyika katika Misheni ya Chaminade, Jimbo Katoliki la Karonga chini ya kauli mbiu isemayo: “Kukuza Uzazi, Njia ya Furaha ya Furaha na Utakatifu.”
Akizungumza, Mwenyekiti wa CWA Taifa, Doreen Banda Zimba alisema kuwa maandalizi yalikuwa yakiendelea vizuri, akitolea mfano shughuli za kamati ndogo.
“Kila kamati, ikiwa ni pamoja na zile za itifaki, liturujia, malazi, afya, na usafi wa mazingira, miongoni mwa zingine, ziko chini kuhakikisha kwamba kila kitu kinawekwa kabla ya muda uliopangwa,” alisema.
Aliongeza kuwa wanawake kutoka kila Jimbo walijitolea kufanya maandalizi ya usafiri wa kuwapeleka kwenye eneo la mkutano.
Mazungumzo mengine yalihusu mada, kama vile asili na madhumuni ya ndoa na familia, Kanuni Nne za Mafundisho Jamii ya Kanisa, Kiroho cha CWA, na Uongozi Kanisani, na Maoni ya Kitamaduni na Kisheria kuhusu Utoaji Mimba na Muungano wa Jinsia Moja, miongoni mwa mambo mengine.
Mawasilisho hayo yaliwezeshwa na Maaskofu, Mapadre na Walei, ambapo Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki nchini Malawi, Mhashamu Askofu Mkuu George Desmond Tambala, aliongoza liturujia ya ufunguzi katika Mkutano huo.