Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Serikali yaweka mkakati wa kutokomeza TB 2030

Waziri wa Afya, Jenista Mhagama (kulia), akikabidhi mashine katika hafla iliyofanyika katika Kituo cha Afya Chamwino, Dodoma. Waziri wa Afya, Jenista Mhagama (kulia), akikabidhi mashine katika hafla iliyofanyika katika Kituo cha Afya Chamwino, Dodoma.

DODOMA

Na Mwandishi Maalum

Serikali imegawa mashine mpya 185 zenye thamani ya Shilingi bilioni saba  kwa ajili ya uchunguzi na ugunduzi wa vimelea vya ugonjwa wa Kifua Kikuu ili kutokomeza ugonjwa huo nchini, ifikapo mwaka 2030.
Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa Afya, Jenista Mhagama, kwenye hafla ya ugawaji wa mashine hizo iliyofanyika katika Kituo cha Afya Chamwino, Dodoma, iliyoenda sambamba na uzinduzi wa Mpango Harakishi wa Kuibua Wagonjwa wa Kifua Kikuu katika Halmashauri 76 za Mikoa tisa.
Waziri Mhagama alisema kuwa Tanzania inafanya vizuri kwenye mapambano dhidi ya ugonjwa wa Kifua Kikuu, ambapo kwa sasa ni nchi ya sita kati ya nchi zote zinazofanya vizuri, lakini bado juhudi zinaendelea ili kufanya vizuri zaidi kwa kuwa bado tupo ndani ya nchi 30 zenye maambukizi makubwa.
“Ugonjwa wa Kifua Kikuu bado ni ugonjwa tishio nchini na ulimwenguni kwa ujumla, kwa kuwa Tanzania ni miongoni mwa nchi 30 zenye maambukizi makubwa ya ugonjwa huo, ambazo kwa pamoja zinachangia asilimia 87 ya wagonjwa wote wa Kifua Kikuu Duniani,” alisema Waziri Mhagama.
Alisema, “Tanzania ilikadiriwa kuwa na wagonjwa wapya wa Kifua Kikuu 122,000, ikiwa ni sawa na wagonjwa 183 kwa kila watu 100,000, ambapo kwa mwaka 2023, Tanzania iliweza kugundua na kuwaweka katika matibabu wagonjwa 93,250, ikiwa ni sawa na asilimia 76 ya wagonjwa 122,000 waliokadiriwa na Shirika la Afya Duniani (World Health Organization: WHO) kuwepo nchini.
Alisema kuwa hali hiyo imeleta msukumo mkubwa ndani ya Serikali kwa kushirikiana na Wadau wa Sekta katika kuongeza juhudi za kupambana na Kifua Kikuu.
Kwa kuzindua mashine hizo, Tanzania inaendelea kuimarisha mtandao wa huduma za uchunguzi na ugunduzi wa vimelea vya Kifua Kikuu kwa njia ya vinasaba ambapo sasa kutakuwa na jumla ya mashine 569 zenye uwezo wa kupima vimelea vya Kifua Kikuu pamoja na usugu wa dawa kutoka mashine 384 zilizokuwepo mwaka 2023, sawa na ongezeko la asilimia 48.
Katika hatua nyingine Waziri Jenista alizindua Mpango Harakishi wa Kuibua Wagonjwa wa Kifua Kikuu kwenye Halmashauri 76 katika Mikoa 9, amabyo kwa 2024 imeonyesha kuwa na kiwango kidogo cha uibuaji wa wagonjwa, ikilinganishwa na ilivyokuwa katika miaka ya nyuma.
Waziri Jenista aliitaja mikoa hiyo kuwa ni Dar es Salaam, Dodoma, Geita, Kagera, Mara, Ruvuma, Shinyanga, Simiyu na Tanga
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Chamwino, Janeth Mayanja, aliishukuru Serikali kwa kuendelea kuboresha huduma za afya nchini.
Alisema kuwa mashine hizo zilizotolewa, zitakwenda kusaidia katika utambuzi wa mapema wa wagonjwa wa Kifua Kikuu, hivyo kuibua watu wengi zaidi wanaougua ugonjwa huo, na kupata tiba mapema.
Naye Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dk. Ahmad Makuwani alisema kwamba licha ya ugonjwa huo kuendelea kuwa tishio, Tanzania imepiga hatua kubwa katika kukabiliana na Kifua Kikuu, ikiwa ni miongoni mwa nchi sita (6) zinazofanya vyema katika mapambano.
Dk. Makuwani alisema kuwa juhudi kubwa sasa zinaelekezwa katika uibuaji wa wagonjwa wapya wa Kifua Kikuu, na Serikali imefanya uwekezaji mkubwa katika teknolojia ya matibabu, hasa kwenye vifaatiba, hivyo sasa tuna jukumu la kutoacha mtu nyuma kwenye mapambano hayo ya kutokomeza Kifua Kikuu ifikapo mwaka 2030.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.