Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Zanzibar kujenga ghala za kuhifadhi vyakula

Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi. Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi.

ZANZIBAR

Na Salum Ali

Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali inajipanga kwa ujenzi wa Maghala ya kuhifadhia chakula ili kuwa na uhakika wa chakula.
Amesema kuwa kujitokeza kwa Sekta binafsi kuanza kujenga ghala ni jambo linalopaswa kuungwa Mkono.
Rais Dk. Mwinyi alisema hayo alipofungua ghala la kuhifadhia chakula Gando, Wilaya ya Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba linalomilikiwa na Kampuni ya Yasser Provision.
Aidha Rais Dk. Mwinyi alisema Serikali inalenga kuwapunguzia mzigo wa gharama Wafanyabiashara wanaoleta chakula nchini ili kuwepo kwa Unafuu wa bei kwa Wananchi.
Rais Dk. Mwinyi alielezea njia nyengine ni kuwa na Ushuru Maalum kwa Bidhaa zinazopelekwa Pemba .
Dk. Mwinyi alibainisha kuwa mpango wa kuifungua Pemba kiuchumi una dhamira thabiti ya kuhakikisha bei za bidhaa muhimu zinashuka na kutoa unafuu wa maisha kwa Wananchi.
Alisema ujenzi wa Bandari za mkoani, Shumba Mjini na Wete ambao utaanza karibuni ni miongoni mwa hatua muhimu ya kuwawezesha Wafanyabishara kuleta mizigo yao moja kwa moja Pemba kutoka nchi wanazoagiza ili kupunguza gharama za mzunguko wa Usafirishaji.
Hata hivyo, Dk. Mwinyi alisema Serikali inajipanga Kutafuta njia bora za kupunguza gharama za chakula kwa Wananchi wa Pemba.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.