Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Kazi ya Kanisa ni kusaidia Waamini kumjua Mungu

Mashemasi wapya wakikata keki wakati wa sherehe ya kuwapongeza kwa kupokea Daraja Takatifu ya Ushemasi. Mashemasi wapya wakikata keki wakati wa sherehe ya kuwapongeza kwa kupokea Daraja Takatifu ya Ushemasi.

DAR ES SALAAM

Na Laura Chrispin

Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mhashamu Henry Mchamungu amewataka Waamini watambue kazi ya Kanisa ni kumfanya mtu aweze kujitafakari na kuwa safi mbele ya Mungu.
Askofu Mchamungu alisema hayo wakati wa Ibada ya Masifu ya Jioni, kiapo cha useja na kukiri imani kwa Mafrateri wanane katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Yosefu, Jimboni humo.
“Mnatakiwa kutambua Utume wa Kanisa ni kuwasaidia watu waishi katika nuru, kwani hata Kristo alikuja kutuongoza ili tuweze kutembea katika mwanga,” alisisitiza Askofu Mchamungu
Alisema pia kwamba mtarajiwa wa Ushemasi au Upadri wa kudumu kabla ya kupokea Daraja Takatifu lazima afanye kiapo cha useja katika ibada, na tena hadharani ikiwa ni sheria iliyowekwa.
Askofu Mchamungu aliendelea kusema kuwa hapo awali kulikuwa na aya mbili, lakini kifungu na.1009 kiliongezwa aya ya tatu ambayo ilieleza kuwa wahudumu wanaopewa Daraja la Uaskofu au Padri, wanapewa uwezo au utume wa kutenda katika nafsi ya Kristo (In Persona Christi).
Sambamba na hayo alisema kwamba wale wa Daraja la Ushemasi, nao wanapewa nguvu za kulitumikia Taifa la Mungu katika Liturujia ya Neno na upendo.
Pia, aliwataka watambue kuwa Shemasi ni Mkrelo na siyo Kasisi, huku akiwahimiza wawe katika imani iliyo thabiti, na siyo kuhangaika kwa wahubiri tofauti badala yake wasimame katika imani yao na mafundisho yake.
Askofu Mchamungu aliwasihi wawe ni watu wenye manufaa, na kufaa katika kazi kusaidiana na Askofu na kusema inapoonekana hana manufaa hatapewa daraja.
Vile vile aliwataka Mafrateri kuwa na nia sahihi kwa kuwa wasaidizi wa Askofu kwa kumsaidia katika kuchunga kondoo wake kwa uadilifu (haimaanishi Maaskofu Wasaidizi).
Mbali na hayo, lazima awe na elimu ya kutosha kabla ya kupewa daraja kwani haiwezekani asimalize kupata elimu na Askofu akampa daraja.
Aliendelea kusema kwamba anayepewa daraja, lazima awe na nidhamu mbele za watu, na watu wamheshimu, na akionekana haheshimiki na watu hataweza kupatiwa daraja la Upadri.
Askofu Mchamungu aliwataka Mafrateri wawe na fadhila za Kimungu, kwani itawasaidia katika kutekeleza majukumu yao vyema, bila matatizo.
Pia aliwataka Waamini wazidi kuwaombea Mafrateri hao{sasa Mashemasi}kwa Mungu, ili waweze kuishi vyema viapo vyao vya kumtumikia Mungu siku zote za maisha yao.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.