Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Mtoleeni Kristo maisha yenu yote asema Askofu

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Sana Jude Taddaeus Ruwa’ichi, akipokea zawadi kutoka kwa WAWATA wa Parokia ya Mtakatifu Antony Maria Claret, Kimara Michungwani jimboni humo, wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya kutoa Sakramenti Takatifu ya Kipaimara iliyoadhimishwa parokiani hapo. (Picha na Yohana Kasosi) Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Sana Jude Taddaeus Ruwa’ichi, akipokea zawadi kutoka kwa WAWATA wa Parokia ya Mtakatifu Antony Maria Claret, Kimara Michungwani jimboni humo, wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya kutoa Sakramenti Takatifu ya Kipaimara iliyoadhimishwa parokiani hapo. (Picha na Yohana Kasosi)

DAR ES SALAAM

Na Celina Matuja

Waamini wametakiwa kuamua wenyewe kutoka ndani ya mioyo yao  kumtolea Bwana Yesu Kristo, maisha yao kwa imani safi, moyo wa upendo na maadili bora.
Wito huo ulitolewa hivi karibuni na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Sana Jude Taddaeus Ruwa’ichi wakati akitoa Homilia yake katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Sakramenti Takatifu ya Kipaimara iliyofanyika Parokia ya Mtakatifu Antony Maria Claret, Kimara Michungwani.
Askofu Ruwaich’i amewashauri na kuwataka kila mwamini mfuasi wa Kristo kujipanga kumtolea Yesu maisha yake akimtambua kuwa ni Bwana na Mungu wake.
“Maisha ya Ufuasi yanatakiwa kuenda sambamba na Matendo mwamini huna budi kumuungama Kristo kwa kumpa maisha yako kwa imani safi, moyo wa upendo, maadili mazuri,”alisema Askofu Mkuu Ruwa’ichi.
Aidha alibainisha kwamba MamaJusi watatu Merkioli, Gaspary na Baltazari walimtolea Yesu zawadi, ambazo zinambakisha, katika ukuu wake, na zawadi hizo ni Ubani ambao unawafanya wamuungame Yesu kuwa ni Bwana na Mungu wao,
Alisema waamini wa sasa wanatakiwa pia kumtambua Yesu Kristo kuwa ni Bwana na Mungu wao, kwani Mama Jusi hao pia walimtolea  Yesu Zawadi ya dhahabu ambayo inaelezea ufalme na walimtolea zawadi hiyo kwa kutambua kuwa ni Mfalme wa ulimwengu.
Na zawadi ya tatu Askofu Mkuu aliitaja kuwa ni Mane Mane (Marashi au Mafuta mazuri) ambayo yanatumiwa na watu na kwa kumtolea marashi hayo waliashiria kifo chake  Masalabani tena cha aibu na atakaye fufuka kwa ajili ya ukombozi wa watu wote, kwa maana hiyo Yesu Kristo alijidhihirisha kwa ulimwengu kuwa ni Mungu na mwokozi wa ulimwengu.
Askofu huyo, alisisitiza kwa waamini kuendelea kumkiri Yesu katika maisha yao kuwa ni Bwana na aliyeshinda dhambi, mauti na aliyeukomboa ulimwengu.
Alisema kila mwamini apende kujipambanua na kuishi maisha ya Mwana wa Mungu kama mtu aliyekombolewa na sio kuishi kiholela bali wenye imani thabiti, usafi wa moyo na sahihi.
Kwa upande wa Waimarishwa Askofu Mkuu Ruwa’ichi, aliwataka vijana hao kuzingatia ufupisho wa habari njema ya wokovu kwamba Kristo aliteswa, Kristo alikufa, amefufuka ni mshindi na mtukufu.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.