Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Na Askofu Method Kilaini

Katika safu hii wiki iliyopita, tuliendelea kuwaletea jinsi himaya za kipagani zilivyokuwa kigingi kwa wakristo na pingamizi toka kwa watawala wa enzi hizo. Leo tunaanza sehemu nyingine ya Historia ya Kanisa Afrika. Sasa Endelea…

UTANGULIZI
Afrika iliinjilishwa katika vipindi vitatu katika historia yake. Kipindi cha kwanza ni kuanzia siku ya Pentekoste hadi karne ya nane. Katika kipindi hiki nchi ya kwanza kuinjilishwa  ilikuwa ni Misri kufuatana na uhusiano wake wa karibu na Palestina. Kutoka Misri dini ilienea hadi Nubia ambayo sasa ni Sudan na Ethiopia au Abyssinia. Sehemu ya  pili kuinjilishwa ilikuwa Afrika ya Kaskazini ambayo ilikuwa inatawaliwa na Warumi.
Isipokuwa Ethiopia katika sehemu nyingine Ukristo ulitoweka au kudhoofika shauri ya Uislamu. Kipindi hiki kwa sehemu kubwa kilisimuliwa katika historia ya jumla ya kanisa.
Hapa tutaongelea kwa ufipi ili kuiunganisha na historia nyingine ya Afrika. Katika historia ya jumla tuliongelea sana juu ya dhuluma na mateso dhidi ya Wakristo kati ya mwaka 64 BK hadi mwaka 313 BK. Katika dhuluma hiyo Wakristo Waafrika wengi walikufa kwa ajili ya imani yao.
Vile vile katika historia jumla tuliongelea juu ya uzushi na mitaguso mbali mbali iliyojaribu kusuluhisha na kuleta umoja na amani ndani ya kanisa.
Kipindi cha pili kilikuwa katika karne ya 15 hadi 17. Wareno katika uvumbuzi wao na ukoloni waliambatana na wamisionari kuanzia Afrika ya Magharibi, ya kati, ya kusini na ya mashariki. Uinjilishaji wa kipindi hiki haukudumu isipokuwa katika sehemu chache sana kwa sababu ulitegemea sana nguvu za Wareno wakoloni. Ukoloni uliposhindwa na dini ilitoweka.
Kipindi cha tatu ni kuanzia karene ya 18 hadi sasa. Wamisionari Wakatoliki na Waprotestanti walijitosa bila kungojea wakoloni na kuwainjilisha Waafrika moja kwa moja hasa chini ya Sahara kwa mafanikio makubwa. Hadi leo Ukristo Afrika unakua kwa kasi kuliko bara lingine lo lote lile. Kipindi hiki ndicho cha uinjilishaji halisi wa Afrika.
KANISA LA MISRI
Misri ilikuwa na usataarabu miaka mingi sana kabla ya Kristo. Watu wemgi waliishi kwenye mwambao wa bahari ya Mediteranea na ukingo wa mto Nile. Nje ya hapo lilikuwa ni jangwa bila watu. Miaka 300 kabla ya Kristo Misri ilitekwa na Aleksanda Mkuu, mfalme huyu  Mgriki alijenga mji wa Aleksandria na kuingiza utamaduni wa Kigriki. Miaka 30 KK Misri ilitekwa na Warumi kisiasa lakini kiutamaduni ilibakia ya Kigriki kama sehemu nyingine za mashariki ya kati. Aleksandria ulikuwa mji wa pili kwa ukubwa na umaarufu katika dola ya Kirumi baada ya Roma. Hata hivyo huko Misri utamaduni wa Kigriki ulikuwa kwa ajili ya wasomi wachache, wengi hasa mashambani na nje ya miji walikuwa Wakopti, wengi wao wakiwa maskini.
Kwa zaidi ya miaka 2000 KK, Misri ilikuwa na uhusiano wa karibu na Palestina na Syria. Tunasoma katika biblia hata Ibrahimu na Yakobo walikwenda Misri. Wakati wa Kristo ikiwa chini ya Waruni ilikuwa na zaidi ya Wayahudi milioni moja na mji wa Aleksandira ulikuwa na Wayahudi zaidi ya 200,000 au 2/5 ya wakazi wa mji huo.
UINJILISHAJI WA MISRI
Katika Agano Jipya, Misri inatajwa mara kadhaa, kwa mfano Maria na Yoseph walimkimbiza mtoto Yesu Misri asiuawe na Herode, (Mt. 2:13); Simoni wa Kirene alitoka Misri (sehemu hiyo siku hizi iko Libya), (Lk. 23:26); na Apolo alikuwa mzaliwa wa Aleksandria (Mat. 18:24). Katika mapokeo ya mitume inaaminika kwamba Mtakatifu Tomaso akielekea India alipitia Misri na kuinjilisha na baadaye alikuwa mwinjilisti Marko aliyeinjilisha Misri na kufia huko kama shahidi.
Wamisri wa kwanza kuongoka walikuwa wale walioongea Kigriki hasa watu wa mataifa waliokuwa wamekubali desturi za Kiyahudi. Hawa tayari waliijua biblia ya Kigriki ‘Septuagint’. Kwa ajili yao biblia ilikuwa imetafriwa kutoka katika Kiebrania. Hawa Wamisri-Wagriki walianza kuelezea Ukristo katika lugha na falsafa ya Kigriki.
Aleksandria palifunguliwa shule maarufu ya dini chini ya Panteanus na baadaye ikawa na waalimu mashuhuri kama Clementi wa Alexandria na Origen. Katika kanisa la mwanzo kanisa la Aleksandria lilikuwa la pili kwa umaarufu baada ya Roma. Mwishowe askofu wa Aleksandria alitambuliwa kama patriarka akiwa na mamlaka karibu yote katika kanisa la Misri.
Mwishoni mwa karne ya pili Ukristo ulienea mashambani kati ya Wakopti. Mwaka 202 wakati wa mateso ya mfalme Kaizari Septimus Severus wanatajwa Wakristo Wakopti wengi waliouawa mashahidi kwa ajili ya imani yao. Katika dhuluma hiyo dhidi ya Ukristo, viongozi wa dini walipopelekwa uhamishoni mashambani kama adhabu, lilikuwa kosa lenye heri kwa sababu liliwapa fursa nzuri ya kuanzisha makanisa imara huko mashambani. Hata biblia ilitafsiriwa katika lugha ya Kikopti katika kilugha (dialect) cha Bohairic ambayo baadaye ilikuwa lugha rasmi ya kanisa la Kikopti na kanisa zima la Misri. Wakati Misri ilikuwa imetawaliwa na Warumi toka Roma au Konstantinopole, dini ndiyo iliwaunganisha katika utaifa wao.
 Wakati Wakristo wa Misri wa lugha ya Kigriki walichangia sana katika kuunda teologia ya kanisa zima la ulimwengu, Wakristo Wamisri - Wakopti walichangia katika kuanzisha umonaki wa wakaa pweke kama Paulo wa Thabes na Antoni wa Jangwani na umonaki wa monasteri kubwa ulioanzishwa na Pakomius. Mwishowe pole pole Wakristo wa Misri  walitengeneza utamaduni mmoja wa Kikopti na kuacha lugha ya Kigriki.
Ingawa kanisa la Misri lilijulikana kwa mafundisho yao sahihi likiongozwa na mapatriarka shupavu kama Aleksanda na Atanasio waliotetea Utatu Mtakatifu, bahati mbaya mwishowe alikuja patriarka Dioscorus aliyekosea na kufundisha kwamba Kristo ni Mungu tu ambaye  utu wake uliliwa na umungu wake. Huu ulikuwa ni uzushi wa monofisiti  uliopingwa na Mtaguso Mkuu wa Kalcedoni mwaka 451 BK.
Bahati mbaya kanisa la Misri wakati zamani lilifurahia ushindi katika mitaguso mbali mbali huko nyuma halikutaka kushindwa na kukubali uamuzi wa mtaguso nkuu huo bali lilijitenga. Kujitenga kwao kuliwagonganisha na kanisa la Konstantinopoli na wafalme wao na kuleta uhathama kati yake na kanisa la ulimwengu. Ingawa utengano ulisaidia kujenga kanisa imara la kitaifa, kanisa la Misri lilijifungia peke yake na kuwa kisiwa likiacha kuchangia katika mawazo ya ulimwengu yaliyolikuza hadi hapo.
Vile vile wamonaki ambao walikuwa ngome kubwa ya kanisa la Misiri bahati mbaya kufikia karne ya tano na kuendelea watu wengi mno wenye uwezo walikimbilia milimani na jangwani kuwa wamonaki wakaa pweke na miji ikabaki na watoto na wazee ambao hawakuweza kuendeleza nchi au kuilinda dhidi ya maadui.  Vile ile wamonaki hao mara nyingi walipokuja mjini wakati wa migongano na mafarakano, walitetea upande mmoja kisiasa na kufanya fujo na hili lilidhoofisha kanisa la Misri.
 Uislamu ulipokuja katika karne ya sita ulikuta kanisa limedhoofika na kutengana na kanisa la ulimwengu la Roma na Konstantinopoli. Siyo tu Kanisa la Kikopti la Misri halikuwa na nguvu ya kugigana na majeshi wa Waislaamu lakini mara nyingine liliungana nao kupigana na Wakristu wengine wa Konstantinopoli.
KANISA LA AFRIKA YA KASKAZINI
Afrika ya kaskazini ilikuwa sehemu ya mwambao yenye upana wa kilometa 320 kuanzia Libya ya leo hadi Morroco.  Mji mkuu wa sehemu hiyo ulikuwa Kartago, ulioanzishwa na wapuniki kutoka Lebanoni karibu miaka 1,000 Kabla ya Kristo, (KK).
Dola ya kipuniki ilienea hadi Sierra Leone. Baada ya vita vya karibu miaka 100, gemadali Mpuniki Hannibal alishindwa na Warumi mwaka 146KK. Warumi walipoteza sehemu kubwa ya dola na kubakia tu na sehemu ya upana wa kilomita 320 kwa sababu wao walijali tu kutunza mipaka kwa usalama wa dola yao.
Wakati wa dola ya Kirumi kuanzia mwaka 146 ustaarabu wa Kirumi uliletwa hasa na maaskari pamoja na wahamiaji wachache na kuenea sehemu zilizotekwa. Wapuniki kwa kiasi fulani waliingia katika utamaduni wa Kirumi lakini wazawa, Waberba, ambao leo tunawaita wabeduini wengi wao walibaki katika utamaduni wao. Hivyo utamaduni wa Kirumi au Kilatini ulibakia wa waja.
Itaendelea wiki ijayo.
UINJILISHAJI WA AFRIKA YA KASKAZINI
Mapokeo yanasimulia kwamba mtume Filipo aliinjilisha Kartago katika safari zake za kimisionari. Maandishi ya kwanza ya kuthibitisha Ukristo ni ya mwaka 180 BK ambapo watu 12 (wanaume saba na wanawake watano) walihukumiwa kuuawa wakati wa mateso ya Marko Aurelio kwa kukataa kumkana Yesu. Tangia hapo Afrika ilikuwa na mashahidi wengi waliofia dini. Mwanateologia maarufu, Tertullian aliandika kwamba ‘damu ya mashahidi ndiyo mbegu ya Ukristo’.
Kartago ulikuwa ndiyo mji wa fasihi ya Kilatini katika dola ya kirumi, wasomi wake walijivunia namna ya kuongea Kilatini kuliko hata katika mji wa Roma wenyewe. Vile vile walifundisha wanasheria wengi na stadi mpaka mji huo ukaitwa kiota cha wanasheria. Kanisa la Afrika Kaskazini lilifuata nyayo likawa kanisa la Kilatini na sheria.
Kanisa la Afrika ndilo lilitafsiri kwa mara ya kwanza Biblia Takatifu katika Kilatini. Kanisa lilitoa wanateologia wakubwa kama Tertullian, Cyprian na Augustino walioweka misingi ya teologia ya kanisa lote la magharibi au kanisa la Roma. Tertulian anaitwa baba wa teologia ya Kilatini. Wanateologia hawa wenye misingi ya kisheria walielezea mafundisho katika maneno ya msamiati wa kisheria yasiyo na ncha mbili au maana zenye utata. Ni kwa sababu hiyo kanisa la magharibi halikuwa na uzishi ya kinadharia bali uzushi wa utendaji na hukumu kati ya dhambi na haki pamoja na adhabu zake.
UZUSHI KATIKA KANISA LA AFRIKA YA KASKAZINI MAGHARIBI
Kwa sababu kanisa la Afrika ya kaskazini magharibi lilitwama juu ya sheria, hivyo hata teologia yake ilikuwa ya mambo ya kimatendo na si kinadharia. Hasa walitaka Mkristu aishi maisha ya utauwa kiasi kwamba ionekane tofauti kati ya maisha yake na yale ya wapagani. Bahati mbaya hii ilielekea kwenye dini kuwa na msimamo mkali na hivyo uzushi wa msimamo mkali ulipata ardhi nzuri ya kusitawi.
Uzushi wa Montanus ilifundisha juu ya maono binafsi kama chanzo cha imani ya kanisa. Ulisisitiza juu ya ulazima wa kuwa mashahidi hivyo ilikuwa dhambi kujificha au kukimbia. Mbaya zaidi walisistiza kwamba dhambi kubwa tatu yaani kuua, kuzini na kuabudu miungu zisingeliweza kuondolewa au kusamehewa. Mtu akifanya hizo dhanbi hawezi kusamehewa na kanisa au kushiriki tena na wanakanisa wenzake. Hii siasa kali iliwateka wengi Afrika akiwamo hata mwanateologia mkuu Tertullian. Uzushi huu ulisumbua kanisa la Afrika hadi Karne ya sita.
Uzushi mbaya zaidi ulikuwa ule wa Donatus. Kwake yule aliyetenda dhambi kama kumkana Kristu kwa woga wa kuuawa alipoteza ukristo wake na inabidi abatizwe upya. Vile vile sakramenti inayotolewa na yule aliye na dhambi si halari lazima irudiwe. Kwa namna hiyo wote waliopewa upadre na uaskofu na maaskofu waliokuwa wametoa vitabu vitakatifu vichomwe hawakuwatambua. Hili lilileta mgawanyiko mkubwa sana. Hawa wafuasi wa Donatus walianza kanisa lao na walikuwa na nguvu hasa mashambani. Ilichukua nguvu za Mtakatifu Augustino kwa maandishi yake (393-411) na majeshi ya Mfalme Kaizari Honorius (398) kuwashinda. Ila vita hivyo vilidhoofisha sana kanisa la Afrika hasa mashambani na kulibakiza kanisa la Warumi tu.
Uzushi mwingine ulikuwa ule wa Pelagius ambaye ili kuwapinga wale waliofanya dhambi bila kujali, kwa kisingizio kwamba binadamu ni dhaifu sababu ya dhambi ya asili ya Adamu na Hawa, alifundisha kwamba binadamu anaweza kwa nguvu zake tu kufanya mema akitaka. Waafrika wengi walimfuata. Mtakatifu Augustino aliandika sana juu ya neema ya Mungu kumpinga mpaka akaitwa ‘Daktari wa neema ya Mungu’.  Alitetea kwamba binadamu hawezi kufanya lolote jema bila msaada wa neema ya Mungu, ila Mungu anatupa neema yake kila mara na tuna uhuru wa kuipokea.
Uzushi wa Afrika ya kaskazini magharibi kama unavyoonyeshwa unatafuta ukweli juu ya matendo ya binadamu, lipi ni sahihi na lipi ni dhambi, mtu afanye nini ili aokoke na ni nani mwenye uwezo wa kutoa huduma za kanisa. Siyo maswali ya kifalsafa kama kanisa la Kigriki la Mashariki ikiwemo Misri bali ya kisheria au kiutendaji.
UVAMIZI WA WAVANDALI
Katika karne ya tano dola ya kirumi ilidhoofika na washenzi mipakani mwake wakaanza kuivamia. Dola ya Kirumi ya magharibi, ambayo ndiyo hasa dola ya Kirumi mji wake mkuu ukiwa Roma, ilisambaratika kabisa mwaka 476. Tangia hapo hapakuwapo tena utawala wa kuunganisha dola nzima hapo Roma. Kaizari wa mashariki, Konstantinopole aliendelea kudai kutawala dola yote lakini hakuwa na maaskari au miundombinu ya kutosha kuithibiti, kila mara ilitegemea nguvu alizokuwa nazo.
Wakati sehemu nyingine za Ulaya zilivamiwa na washenzi wapagani kama Wafranki, Wavisigoti,  Wahuni, Wasaksoni, Waburgundi na wengine; Afrika ilikuwa na bahati mbaya kuvamiwa na wavandali. Hawa walikuwa wabaya kuliko wote kwa sababu waliharibu kila kitu walichoona. Kwa lugha za wazungu kusema vandali maanake mharibifu (vandalism). Baada ya kupitia Spain walitua Afrika na kuharibu ustaarabu wote chini ya kiongozi wao Genseriki. Wakiwa wazushi Waariani waliwanyanganya wakatoliki makanisa yao yote na wakawapeleka maaskofu uhamishoni. Walikataza ibada na mafundisho yote ya Kikatoliki na waliokataa kutii amri hiyo waliuawa mashahidi. Walichangia sana kudhoofisha kanisa la Afrika. Majeshi ya Kaizari Justiniani wa mashariki, Konstantinopole, yaliwashinda Wavandari mwaka 535 na kuwafukuza lakini kanisa la Afrika ya Kaskazini halikupata nguvu tena mpaka walipovamiwa na Waislamu katika karne ya nane.

Waamini wa Parokia ya Mwenyeheri Isdori Bakanja, Boko, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, wakiwa katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Jumatano ya Majivu iliyoadhimishwa hivi karibuni parokiani hapo. (Picha zote na Yohana Kasosi)

Masista kutoka Mashirika mbalimbali wanaofanyakazi ya Kitume Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, wakiwa katika Semina ya Kupinga Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu, iliyofanyika katika ukumbi Parokia ya Kristo Mfalme, Tabata, jimboni humo.

Wanawake Wakatoliki Tanzania (WAWATA) Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam wakipeleka majitoleo Altareni kwa Askofu Mkuu wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Kutabaruku Kanisa jipya la Seminari Ndogo ya Mtakatifu Maria, Visiga, jimboni humo.

Waamini walioshiriki Kongamano la Karismatiki Katoliki Kambi ya Uponyaji, wakiongozwa na Kwaya kusifu na kuabudu wakati wa kuhitimisha kongamano hilo lililofanyika katika Parokia ya Mtakatifu Anthony wa Padua, Mbagala Zakhiem, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam. (Picha na Celina Matuja)

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, akifungua Mlango Mkuu wa Kanisa kuashiria uzinduzi wa Kanisa jipya la Seminari ya Mtakatifu Maria- Visiga, wilayani Kibaha mkoani Pwani, wakati wa Kutabaruku Kanisa hilo. Kushoto ni Gombera, Padri Philipo Tairo, na wa pili ni Kansela wa Jimbo hilo, Padri Vincent Mpwaji.

DAR ES SALAAM

Na Arone Mpanduka

Jumamosi ya Februari 10 mwaka huu majira ya mchana, zilitoka taarifa za kwamba aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Imani Madega, amefariki dunia.
Hakika zilikuwa ni taarifa za ghafla zilizotokana na kifo cha ghafla, kwani inaelezwa kwamba asubuhi ya siku hiyo akiwa nyumbani kwake Chalinze mkoani Pwani, alimuomba mtoto wake ampeleke hospitali kwa madai kwamba anajisikia vibaya, ingawa alikuwa na nguvu zake akitembea mwenyewe, lakini wakati akifanyiwa vipimo na matibabu hospitalini, hali ilibadilika na alifariki kwa tatizo la shinikizo la damu.
Katika kolamu hii, nitakusimulia baadhi ya matukio ambayo Madega aliwahi kuyafanya akiwa na Yanga ambayo aliiongoza kuanzia Mei mwaka 2007 hadi 2010.
APINGA YANGA KAMPUNI
Hiyo ilikuwa ni mwaka 2007 ikiwa ni siku chache baada ya kushinda nafasi ya uenyekiti wa Yanga, ambapo yeye na Viongozi wenzake, waliitwa ofisini kwa Yusuph Manji ambaye wakati huo alikuwa mfadhili.
Katika wito huo, Manji alimtaka atie saini mkataba wa makubaliano ya kuifanya Yanga iwe Kampuni na baada ya hapo Francis Kifukwe angepewa urais ndani ya mfumo huo, kitu ambacho Madega alikataa.
Sababu ya kukataa ni Katiba kutoruhusu kwa wakati huo, huku pia akiwa na wasiwasi kwamba huenda likawa changa la macho la kutaka klabu hiyo kubinafsishwa kihuni.
Madega aliitisha mkutano na waandishi wa habari na kusema kwamba hawezi kufanya kitu kama hicho na kwamba Manji hana nia nzuri na klabu, hivyo ni vyema awaachie timu yao na wao wapo tayari kupambana nayo ili kuiendesha. Hapo ndipo uhasama kati yake na Manji ulipoanza.
KAULI YA KIBABE BAADA YA YANGA KUTEKWA
Ilikuwa Oktoba mwaka 2007, ambapo wakati huo uhasama kati yake na Manji ulizidi kupamba moto na kuibua makundi mbalimbali ambayo mengine yaikuwa yanampinga yakitaka aondoke madarakani.
Siku moja Yanga ikiwa chini ya kocha Mmalawi, Jack Chamangwana (sasa marehemu), ilitekwa na kundi la makomandoo ambao inasemekana walikuwa upande wa Madega na kwenda kufichwa Morogoro.
Katika mahojiano yake na kipindi cha Spoti Leo cha Redio One, Madega alikaririwa akisema, “Sitakuwa tayari kuiona Yanga ikiuzwa na kutawaliwa na mtu mmoja kwa nguvu ya pesa, masikini na mwanawe, tajiri na mali zake, Manji baki na mali zako au heshimu Katiba. Vinginevyo baki na mali zako au fadhili timu nyingine.” Baada ya sekeseke hilo, baadaye hali ya hewa ilikaa sawa.
AMSHUTUMU MANJI KUHUJUMU TIMU
Mwezi huo huo mwaka 2007, Yanga ilicheza dhidi ya Simba kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro, na Yanga kufungwa bao 1-0. Baada ya mchezo Madega aliibuka na kumshutumu Manji kwamba alitoa pesa kwa wachezaji ili wajifungishe kwa lengo la kumfanya aonekane hafai kuiongoza klabu hiyo na aondolewe kirahisi.
Ikumbukwe kuwa kabla ya mchezo, Manji alitoa Shilingi milioni 40 za maandalizi, huku akitoa na milioni 10 kwa wazee ili wafanye mambo ya kishirikina kwa ajili ya mchezo.
AOMBA RADHI WAZEE/MANJI
Ilikuwa mwishoni mwa mwaka huo huo wa 2007, ambapo siku moja waandishi tuliitwa kwenda kuchukua habari kwenye ukumbi wa hoteli ya Travertine, Magomeni jijini Dar es Salaam ambapo Madega aliingia ukumbini, na wanahabari wote tulitakiwa kusubiri nje kwanza. Baada ya dakika kadhaa tukaitwa na kutaarifiwa kwamba mzozo kati ya Madega, Manji, na wazee umekwisha baada ya Mwenyekiti huyo kuomba radhi.
AONGOZA MKUTANO KWA DAKIKA TATU
Ilikuwa mwaka 2008 ambapo Madega aliitisha mkutano wa wanachama kwenye ukumbi wa Police Officers Mess, na waandishi wa habari tulikwenda kushuhudia kile kilichofanyika. Miongoni mwa yaliyokwenda kufanyika, ni kupitisha baadhi ya marekebisho ya vipengele kwenye katiba.
Kabla ya mkutano kuanza, wanachama walipewa rasimu ya katiba ili kuweza kupitia na kufanya maamuzi. Ilipofika majira kama ya saa 3 na nusu asubuhi, Madega aliingia mkutanoni kuhakiki akidi na moja kwa moja kuhoji wanachama wote kama wanakubali rasimu ipite ama la.
Wanachama wengi walinyoosha mikono juu kuonyesha wameridhia, na hapo hapo Madega alitangaza kuwa rasimu imepita na kufunga mkutano huo, huku akisindikizwa na wimbo wa Pepe Kalle (hayati) wa Young Africans. Mkutano huo ulitumia dakika 3 tu na kuwashangaza wengi.
ATUKANWA NA NICOLAUS MUSONYE
Hilo lilijiri baada ya Yanga kukataa kuingiza timu uwanjani julai mwaka 2008, ambapo ilitakiwa kucheza na Simba kuwania mshindi wa tatu katika michuano ya Kagame. Siku hiyo uwanja ulifurika kuzisubiri timu ziingie uwanjani, lakini walionekana wachezaji wa Simba pekee.
Madega alipoulizwa, alisema kuwa walikubaliana pande zote (Simba na Yanga), kuwa wasipeleke timu uwanja mpya wa Taifa (sasa Benjamin Mkapa) kama matakwa yao yasingetekelezwa na CECAFA (ya mgawo wa mapato ya milangoni), lakini cha kushangaza wenzao wamewasaliti kwa kupeleka timu uwanjani.
Siku moja baada ya tukio hilo, aliyekuwa Katibu Mkuu wa CECAFA Nicolaus Musonye, alituita wanahabari kwenye ukumbi wa jengo la Millenium Tower, Mwenge, na ‘kuwaponda’ viongozi wa Yanga akidai kwamba wote wakiongozwa na Madega, ni dhaifu, na hawajitambui pamoja na kauli zingine nyingi zisizoandikika, huku wakiifungia Yanga kutoshiriki kwa miaka mitatu.
AIWEKEA NGUMU TBL
Ilikuwa mwaka 2008 ambapo Madega alikataa agizo la wadhamini wao TBL la kutaka waajiri watendaji kama mkataba wao ulivyokuwa unaelekeza.
Madega alisema kuwa hayo hayakuwa makubaliano, bali walikubaliana kuajiri Mweka Hazina kwa sababu hawakuwa na uwezo wa kuwalipa watendaji, kama vile Katibu.
Mvutano huo ulitokea kabla ya Shirikisho la Soka Duniani FIFA kutaka wanachama wake wote kuwa na watendaji wa kuajiriwa, ambapo mwaka 2010 Simba na Yanga zilianza kuajiri Maafisa Habari na Makatibu.
AMSHUSHUA NGASSA
Ilikuwa mwaka 2009 ambapo ilidaiwa kwamba mchezaji Mrisho Ngassa aliuomba uongozi umuongezee mshahara kwa sababu kipindi hicho alikuwa na uwezo mkubwa uwanjani kushinda hata baadhi ya wachezaji wa Kimataifa waliokuwa wanasajiliwa klabuni hapo.
Siku moja Madega alifanya mkutano na waandishi wa habari na kuchomekewa swali hilo, na katika majibu yake, alisema kwamba haiwezekani mchezaji anakwenda Yanga akiwa mnyenyekevu halafu baadaye anatanua mabega akitaka kuongezewa mshahara.
Aliongeza kwa kusema kwamba Ngassa kuna kipindi alikuwa akipewa Shilingi elfu tano tu anatetemeka, hivyo asijifanye ana thamani sana, na badala yake akumbuke alipotoka.
AWEKA MSIMAMO USAJILI WA NGASSA ULAYA
Kuna mwaka ziliibuka taarifa kwamba klabu ya Lov-ham ya Norway ilikuwa inamtaka Ngassa, lakini uongozi ulimzuia.
Madega alitoa ufafanuzi kwa kusema kwamba haiwezekani wakala akawa anazungumza na vyombo vya habari tu bila wao kujua, hivyo suala hilo ni uzushi kwa sababu taarifa rasmi hazijawafikia mezani.
AACHA MILIONI 200 KWENYE AKAUNTI
Mwaka 2010 baada ya muda wake kuisha ndani ya Yanga, Madega hakutaka kutetea tena kiti chake na kuwaachia wengine wagombee. Katika taarifa yake kwenye Mkutano Mkuu wa Uchaguzi, Madega alitangaza rasmi kwamba anaondoka, huku kwenye akaunti ya klabu akiwa ameacha zaidi ya shilingi milioni 200.
Hali hiyo ilimfanya awe Mwenyekiti pekee wa timu za Tanzania kuondoka madarakani na kuacha akaunti zikiwa zimenona.
Huyo ndiyo marehemu Imani Madega na harakati zake ndani ya Yanga. Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amina.

LOS ANGELES, Marekani
Bingwa mara tano wa National Basketball Association (NBA), Kobe Bryant, alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 41 katika ajali ya helikopta, pamoja na bintiye Gianna mwenye umri wa miaka 13, na watu wengine saba, mwaka 2020.
Sanamu yake ya shaba, iliyo na futi 19 na uzani wa lb 4,000, iko nje ya nyumba ya Lakers, Crypto.com Arena. Inaonyesha Bryant ambaye aliichezea Lakers maisha yake yote, katika jezi yake namba nane maarufu.
Gwiji wa Los Angeles Lakers Kobe Bryant ametunukiwa sanamu hiyo na timu ya NBA kufuatia kifo chake mwaka 2020. Mjane wake Vanessa na nguli wa zamani wa Lakers, Kareem Abdul-Jabbar walikuwa miongoni mwa watu waliotoa heshima zao, wakimuelezea Bryant kama “jinsi ubora unavyoonekana”.

LEVERKUSEN, Ujerumani
Mkurugenzi wa Michezo wa klabu ya Bayer Leverkusen ya Ujerumani, Simon Rolfes anasema kuwa ana uhakika kwamba kocha wa klabu hiyo, Xabi Alonso atasalia katika klabu hiyo baada ya majira ya joto, huku kukiwa na uvumi unaomhusisha kocha huyo kwenda katika klabu ya Liverpool ya Uingereza.
Alonso, ambaye alishinda Ligi ya Mabingwa na Kombe la FA katika kipindi cha miaka mitano kama mchezaji Anfield, ametajwa kama mbadala wa Jurgen Klopp, ambaye ataondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.
Mhispania huyo ameibadilisha Leverkusen tangu kuteuliwa kwake BayArena Oktoba mwaka 2022, na amekuwa akiwahangaisha vigogo wengi katika mechi zake ambazo amekutana nao.
Leverkusen walikuwa kwenye eneo la kushushwa daraja wakati Alonso alipochukua usukani, lakini sasa wanajikuta wakiwa kileleni mwa msimamo baada ya kuichapa Bayern Munich 3-0 kwenye mchezo wa Ligi hiyo ya Bundesliga uliochezwa hivi karibuni.
“Ndiyo, nina uhakika na hilo moja ya sababu ni mkataba, nyingine ni jinsi anavyojisikia vizuri, familia, yeye mwenyewe”.

DAR ES SALAAM

Na Nicolaus Kilowoko

Baada ya kukaa miezi saba bila kuwa na pambano lolote, bondia Suleiman Kidunda anatarajiwa kupanda ulingoni mwezi Machi mwaka huu dhidi ya bondia kutoka nchini Afrika Kusini.
Selemani Kidunda anatarajiwa kuzipiga dhidi ya bondia Asemahle Wellem kutoka Afrika Kusini katika pambano ambalo litapigwa Machi 1 mwaka huu katika ukumbi wa Warehouse, Masaki, jijini Dar es Salaam.
Kidunda alisema kuwa kimya kingi, kishindo huvuma, hivyo kwa sasa ameshaingia vitani kupambana na kukaa kwake pembeni kumemfanya aendelee kujifua dhidi ya mapambano yake huko mbele.
Bondia Asemahle Wellem kutoka Afrika Kusini ni sawa na mfupa uliowashinda wengi, kwani amekuwa na mapambano mengi na kuwashinda wengi katika mapambano yake.
“Mashabiki wangu naomba msiwe na hofu, dogo katangaza vita na mimi nishaingia vitani, yaani nimeshaingia chaka, nipo tayari kupambana, tuombe Mungu tukutane hiyo siku,” alisema Kidunda.