VATICAN CITY, Vatican
Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Baba Mtakatifu Leo XIV amekutana na kuzungumza na kikundi cha wanahija kutoka Parokia ya Mtakatifu Thomás wa Villanuova - Alcalá ya Henares nchini Hispania.
Katika hotuba yake kwa lugha ya kihispania, Papa alionesha furaha yake kukutana nao katika siku ya Oktava ya Noeli na kuwakaribisha sambamba na kuzungumza nao mambo mbalimbali.
Kama Jumuiya ya Parokia, alisema kwamba waliweza kujiandaa kwa jitihada kubwa katika hija ya kijubilei na wakati wa mwaka huu kwa namna ya pekee kwa Kanisa ambapo walimsindikiza Mfuasi wa Mtume Petro kwa sala zao na kwa ukarimu wao.
Dar es Salaam
Na Dk. Felician B. Kilahama
Mapokeo ya kihistoria tangu miaka ya 1880, yanathibitisha kwamba baadhi ya mataifa barani Ulaya mathalani, Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, Ubelgiji na Hispania, yaliweza kufika barani Afrika.
Hivyo, 1884 kukafanyika kikao maalumu jijini Berlin-Ujerumani, kwa lengo mahususi kugawana maeneo kuitawala Afrika.
Kwa upande wa Afrika-Mashariki, Wajerumani wakatawala “Tanganyika” na wakaweza kufika maeneo ya Iringa, ambako Hifadhi-Ruaha inapatikana. Wakiwa huko waliona sehemu imesheheni rasilimali nyingi za wanyamapori, na kuifananisha na “Bustani ya Edeni”.
Kiuhalisia Ruaha kuna urithi wa aina yake, mathalani milima na mabonde pamoja na rasilimali-misitu aina ya miombo, misitu inayostawi kandokando ya mito, na Mto Ruaha-Mkuu. Mto huu ni msaada mkubwa aina yake, ikiwemo wanyamapori wanaoishi kwenye hifadhi ya Ruaha.
Waamini kutoka Parokia mbalimbali za Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, wakiwa katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Nadhiri za Kwanza za Masista wa Shirika la Mtakatifu Fransisko wa Asizi Dada Wadogo, iliyofanyika katika Makao Makuu ya Shirika hilo, Mbagala-Dar es Salaam.
Watoto wa Shirika la Kipapa la Utoto Mtakatifu kutoka Parokia mbalimbali za Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, wakiwa katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Sherehe ya Watoto Mashahidi iliyofanyika katika viwanja vya Parokia ya Kristo Mfalme, Tabata jimboni humo hivi karibuni.
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Sana Jude Thaddaeus Ruwa’ichi (aliyeshika Fimbo ya Kichungaji), Askofu Msaidizi wa Jimbo hilo, Mhashamu Henry Mchamungu (kushoto), Askofu wa Jimbo Katoliki la Bagamoyo Mhashamu Stephano Musomba (kulia) na Mapadri wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Shirika la Masista wa Mtakatifu Fransisko wa Asizi Dada Wadogo na Masista walioweka Nadhiri za Kwanza, baada ya Adhimisho la Misa Takatifu ya Nadhiri hizo.
MWANZA
Na Paul Mabuga
Hebu vuta picha: Zamani kijana wa Kitanzania hakukurupuka tu kuitwa mzazi. Kulikuwa na mifumo madhubuti ya Jando, Unyago, na yale mafunzo ya kando ya moto kutoka kwa babu na bibi, yaliyomjenga mtu kifikra na kihisia.
Lakini leo, “moto” pekee unaowaunguza vijana wetu ni wa data za simu, na mianga ya mitandao ya kijamii. Wakati mifumo hiyo ya kijadi ikipumzika kwenye makaburi ya historia, tunapaswa kujiuliza kwa uchungu: Je, vijana wetu wanajifunza wapi kuwa wazazi?
Dar es Salaam
Na Joseph Mihangwa
Chimbuko la Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni Mapinduzi ya Zanzibar, yaliyofanyika Visiwani humo Januari 12, 1964.
Bila Mapinduzi hayo tusingezaliwa Tanzania, wala Chama tawala cha sasa - Chama cha Mapinduzi (CCM), ambacho ni Muungano wa Vyama vya Tanganyika African National Union (TANU) cha Tanganyika, na Afro-Shirazi Party (ASP) cha Zanzibar.
Chama kilichozaliwa Februari 5, 1977, miaka 13 baada ya Muungano uliofikiwa Aprili 26, 1977, ni matokeo ya kero za Muungano.
Mapinduzi haya yaliyoshangaza dunia kwa staili yake, yalifanyika kwa harakati za siasa za mrengo wa Kikomunisti, na kutia hofu nchi za Magharibi, hasa Marekani na Uingereza, zikaamua kuingilia kati kuyadhibiti Mapinduzi hayo, kuzuia kuenea kwa Ukomunisti Afrika kupitia Afrika Mashariki.
Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Henry Mchamungu akibariki vipaji wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Mkesha wa Mwaka Mpya 2026, katika Parokia ya Bikira Maria Mama wa Huruma - Mbezi Beach, jimboni humo. (Picha na Mathayo Kijazi)
Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA) Jimbo Kuu la Dar es Salaam wakishangilia jambo wakati wa Homilia katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Beach Mass iliyoadhimishwa ufukweni Jimbo Katoliki la Bagamoyo.
Mwenyekiti wa Parokia ya Mtakatifu Kamili Yombo Kiwalani Josephat Moshi, akiwa katika picha ya pamoja na Wanakwaya wa Kwaya ya Shirikisho ya parokia hiyo, baada ya Adhimisho la Misa Takatifu ya Krismasi iliyofanyika parokiani hapo.
Masista wa Shirika la Mtakatifu Fransisko wa Asizi Dada Wadogo Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, wakiwa katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Nadhiri za Kwanza iliyofanyika katika Nyumba ya Masista hao Mbagala jimboni humo.
DAR ES SALAAM
Na Nicholas Kilowoko
Siku chache mara baada ya pambano lililomalizika, kwa Hassan Mwakinyo kumtandika bondia Stanley Eribo kutoka nchini Nigeria kwa ‘KO’, katika raundi ya pili ya pambano la raundi 10, bondia Twaha Kiduku ameubeza ushindi wake.
Bondia Twaha alisema kuwa pambano hilo lililofanyika siku ya Boxing Day, lilikuwa halina hadhi kutokana na mpinzani wa bondia mwenzake Mwakinyo, kutokuwa katika kiwango kinachotakiwa.
DAR ES SALAAM
Na Nicholas Kilowoko
Kocha wa vijana wa klabu ya soka ya Simba, John Bocco, ameelezea mikakati yake mipya ya kuisaidia timu yao kubwa, kupata vijana wazawa wenye vipaji na watakaolisaidia Taifa pia.
Kwa muda mrefu nyota huyo wa zamani, ambaye alifanya makubwa ndani ya klabu ya Simba, Azam FC, na JKT Tanzania, alikuwa yupo kimya mara baada ya kumaliza kazi yake ya uchezaji.
DAR ES SALAAM
Na Arone Mpanduka
Mkuu wa Kitengo cha Habari cha klabu ya soka ya Azam FC, Thabit Zacharia maarufu kama Zaka Zakazi, amesema kuwa kitakwimu winga wa Taifa Stars Simon Msuva, bado ataendelea kuwa juu katika ufungaji wa mabao mengi katika kikosi hicho, kuliko mchezaji mwingine yoyote.
Akitoa ufafanuzi kuhusiana na ubishani unaoendelea, wa kumlinganisha Msuva na mchezaji wa zamani wa Taifa Stars Mrisho Ngassa, Zaka alisema kwamba nyota hao wanalinganishwa kimakosa, kwa sababu Msuva ana mabao 21 aliyoifungia Taifa Stars pekee, huku Ngassa mabao yake yakichanganywa na aliyoifungia Kilimanjaro Stars, ambayo ni ya Tanzania Bara pekee.