Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Dar es Salaam

Na Mathayo Kijazi

Dekano wa Dekania ya Mavurunza, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Padri Vivian Menezes- OCD, amewasihi Waamini kufahamu kwamba kuwa na mali nyingi kusiwe sababu ya wao kufarakana na Mungu, kwani kila walichonacho kinatoka kwake.
Padri Vivian alisema hayo wakati wa homilia yake, alipomwakilisha Askofu Mkuu wa Jimbo hilo, Mhashamu Sana Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, kuadhimisha Misa Takatifu ya Sakramenti Takatifu ya Kipaimara kwa vijana 119, katika Parokia ya Mtakatifu Yohane Maria Muzeey - Tegeta ‘A’.

Tabora

Na Mwandishi wetu

Kauli ya Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (Tanzania Episcopal Conference: TEC), Mhashamu Wolfang Pisa, ya kuwataka Wakatoliki kulinda usafi wa Kanisa, na kutokubali Kanisa hilo linajisiwe na kudhoofishwa, bado imeendelea kutikisa kila kona.
Askofu Pisa, ambaye pia ni Askofu wa Jimbo Katoliki la Lindi, alitoa kauli hiyo yenye kuvuta na kugusa hisia za wengi hivi karibuni, wakati alipokuwa akitoa homilia yake, katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Jubilei ya Miaka 100, ya Seminari Kuu ya Mtakatifu Paulo - Kipalapala, Jimbo Kuu Katoliki la Tabora.

Dar es Salaam

Na Mathayo Kijazi

Paroko wa Parokia ya Kristo Mfalme – Tabata, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Padri Cornelius Mashare, amewataka wazazi kutowalea watoto wao kama mayai, kwa kutowaruhusu wafanye kazi za nyumbani, kwani kufanya hivyo ni kutengeneza kizazi legelege.
Akihubiri katika Adhimisho la Misa Takatifu ya shukrani kwa Mungu, kwa Mahafali ya 20 ya Darasa la Saba katika Shule ya Msingi Kristo Mfalme, iliyoadhimishwa parokiani hapo, Padri Mashare alisema kwamba inasikitisha kuona kijana wa darasa la saba, hawezi kutandika hata kitanda, kuosha vyombo, wala kufanya kazi yoyote, ambayo vijana wengine wa umri wake wanaweza kufanya.

Zanzibar

Na Mwandishi Wetu

Tume ya Ushindani (FCC) na Tume ya Ushindani wa Haki Zanzibar (ZFCC), zimetia saini mkataba wa ushirikiano wenye lengo la kuhakikisha masoko yanakuwa na ushindani wa haki, na kulinda maslahi ya walaji nchini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Tanzania Bara, Dk. Hashil Abdalah, alisema kwamba makubaliano hayo yameweka misingi muhimu, ambayo pande zote mbili zinapaswa kuizingatia katika utekelezaji.

Manyoni

Na Jackline Minja

Katika kuelekea kwenye kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Wazee Duniani, serikali imeendelea kudumisha huduma bora kwa wazee, kwa kuhakikisha kundi hilo linapata huduma za msingi, zinazowawezesha kuishi maisha yenye heshima, na kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya taifa.
 Hayo yalisemwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Wakili Amon Mpanju, wakati wa ziara yake katika Makazi ya Wazee Wasiojiweza, yaliyopo Sukamahela, wilayani Manyoni mkoani Singida.

Bukoba

Na Mwandishi wetu

Balozi na Mwanadiplomasia wa Vatican, Mhashamu Askofu Mkuu Novatus Rugambwa ambaye ni Mtanzania, amefariki Dunia Jumanne ya Septemba 16, mwaka huu mjini Roma nchini Italia.
Taarifa iliyotolewa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba Mhashamu Jovitus Mwijage  kwa Maaskofu, Mapadri, Watawa na Waamini ilieleza kwamba Askofu Mkuu Rugambwa aliaga Dunia wakati akipatiwa matibabu kutokana na changamoto za kiafya.

Dar es Salaam

Na Mathayo Kijazi

Wakristo wametakiwa kuwa na misalaba katika nyumba zao, iwasaidie kumshinda shetani pale anapowakaribia.
Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Henry Mchamungu, alitoa siri hiyo hivi karibuni wakati akitoa homilia yake katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Dominika, iliyokwenda sanjari na utoaji wa Sakramenti Takatifu ya Kipaimara kwa vijana 52, katika Parokia ya Mtakatifu Maurus - Kurasini, jijini Dar es Salaam.

Mbozi

Na Mwandishi Wetu

Katika hatua muhimu ya kupunguza upofu, Hospitali ya Rufaa ya Kanda Mbeya (MZRH) na Shirika la Helen Keller International, leo wamewasili mkoani Songwe kwa ajili ya kutoa Huduma Mkoba ya matibabu ya ugonjwa wa mtoto wa jicho “Cataract Management”, kwa wananchi takribani 700 wa Songwe, katika Hospitali ya Wilaya ya Mbozi (Vwawa).
Akiongea na Waandishi wa Habari, Dk. Jofrey Josephat Mratibu wa Huduma za macho Mkoa wa Songwe, alieleza kuwa kambi hiyo ya siku sita imelenga kukabiliana na magonjwa ya mtoto wa jicho, na kusogeza huduma hizo adimu katika maeneo ya karibu na wanapoishi (vijijini), ambapo imekuwa ngumu kupatikana na gharama kwa wananchi, kuzifuata katika hospitali kubwa.

Mwanza

Na Mwandishi Wetu

Simanzi imetawala katika Kanisa Katoliki nchini, kutokana na msiba mzito wa vifo vya Watawa wanne, wa Shirika la Mtakatifu Teresia wa Mtoto Yesu pamoja na dereva wao, waliofariki dunia katika ajali ya gari mkoani Mwanza.
Waliofariki dunia ni Mama Mkuu wa Shirika la Mtakatifu Teresia wa Mtoto Yesu duniani, Katibu Mkuu wa Shirika hilo, Masista wawili pamoja na dereva wao, katika ajali baada ya gari walilokuwa wakisafiria, kugongana na gari jingine.
Watawa hao ni Sista Lilian Kapongo (raia wa Tanzania), Mama Mkuu wa Shirika hilo duniani, Sista Nerina De Simone (raia wa Italia), Katibu Mkuu wa Shirika hilo duniani, Sista Damaris Matheka (raia wa Kenya), Sista Stellamaris Muthini (raia wa Kenya), na dereva wao Boniphace Peter Msonola, mkazi wa Bukumbi Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.

Dar es Salaam

Na Mathayo Kijazi

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Sana Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, ametoa ufafanuzi na kukanusha kwamba si kweli kwamba Wakatoliki wanaabudu sanamu, bali wanamwabudu Bwana Yesu Kristo, aliyejinyenyekesha, akatii mpaka kufa msalabani.
Aliyasema hayo hivi karibuni, katika homilia yake wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu, ya Sikukuu ya Fumbo la Kutukuka kwa Msalaba, iliyofanyika katika kituo cha Hija – Pugu, jimboni humo.