Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Stephano Musomba - OSA (mwenye fimbo ya kichungaji), akiwa katika picha ya pamoja na Mapadri na Viongozi wa Kamati Tendaji wa Parokia ya Mtakatifu Pio wa Pietrelcina - Ulongoni ‘B’, baada ya Adhimisho la Misa Takatifu ya Sherehe ya Miaka 10 ya Parokia hiyo. Kushoto kwa Askofu ni Paroko wa Parokia hiyo, Padri Leonard Amadori - OFMCap (Picha na Mathayo Kijazi)

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Sana Jude Thaddaeus Ruwa’ichi akiwa katika picha ya pamoja na Mapadri, Viongozi wa Kamati Tendaji na Kamati ya Ujenzi wa Shule mpya ya Awali na Msingi ya Mary of The Rosary Pre & Primary School ya Parokia ya Bikira Maria wa Rozari Takatifu - Makongo Juu.

Shule mpya ya Awali na Msingi ya Mary of The Rosary Pre & Primary School ya Parokia ya Bikira Maria wa Rozari Takatifu - Makongo Juu, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam kama inavyoonekana pichani baada ya kubarikiwa na kuzinduliwa na Askofu Mkuu wa Jimbo hilo, Mhashamu Sana Jude Thaddaeus Ruwa’ichi.

Mwanza

Na Paul Mabuga

Kuna makundi kadhaa ya vizazi kutokana na mazingira na matukio katika nyakati mbali mbali.
Mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia, na hasa mapinduzi ya kidijitali, yamechangia zaidi kuongezeka kwa tofauti kati ya makundi ya vizazi, hali ambayo imeathiri mahusiano, mitindo ya maisha, na makuzi.
Uhusiano wa kizazi kimoja kwenda kingine, limekuwa ni jambo lenye changamoto kulimudu. Katika muktadha huo, mwandishi wetu Paul Mabuga  anaangalia uhusiano kati ya wanandoa kutoka zama za ‘baby boomer’ na ‘milenia’.
Harufu ya sangara anayekaangwa, imetanda katika nyumba moja iliyopo katika mtaa wa Nyamanoro jijini Mwanza. Kwa hakika inavutia, kwani hata kwa mwenye hisia ndogo ya kunusa, anaweza kuitambua, na kwa mwenye njaa aliye jirani, ni lazima aombe msaada.
Baba mwenye nyumba tunayemwita Adam Fungamwango, yupo sebuleni akisoma gazeti. Unamtazama, unapokewa na sura yenye mikunjo inayokutangazia kuwa Bwana huyu umri wake kwa makadirio ni miaka 64. Na wewe ni mgeni pekee sebuleni.
“Karibu, lakini kabla ya yote fanya ufanyavyo kwenye mahojiano, lakini jina langu sitaki lijulikane! Vinginevyo hakuna mahojiano hapa,” anasema bwana huyu akikukaribisha na kuendelea na mazunguzo baada ya kuhakikishiwa kuwa litatumika jina bandia ili kuficha utambulisho wake, “Mie nilikuwa dereva, na nimeendesha maafisa wengi wakubwa, na sasa ni miaka minne tangu nimestaafu.”
Anasema, mkewe ambaye naye, tunamtambulisha, kwa jina la bandia la Diana Fungamwango, bado ni mfanyakazi kama katibu muhtasis katika moja ya mashirika ya umma jijini Mwanza, na ana umri wa miaka 44 kwa sasa. Walioana miaka 23 iliyopita, na kwamba  Diana anatumia muda mwingi kazini isopokuwa siku za mwisho wa juma.
Diana ambaye ndiye anayekaanga samaki, hana makuu, katopea katika simu yake ya mkononi akitaradika na yaliyomo. Pengine anaanza leo wasanii gani wamechambana kwenye mitandao,  anashuka na wale wasemaji wa timu za mpira na washabiki wao, na baadaye anatambaa na darasa la sifa za mume bora, na kumalizia na hadithi. Yeye ameshika mbili na wala hazimponyoki, huku ana simu, na kule  anakaanga.
Hii ni ndoa kati ya mume  ambaye katika zama za vizazi, yupo kwenye kundi la ‘Baby Boomer,’ ambao wamezaliwa kati ya miaka ya 1946 na1964  na mke ambaye yupo kwenye lile linalojulikana kama ‘milenia’, ambao walizaliwa kati ya  1981 na1996. Makundi haya ya vizazi na mengine,  kila moja  lina sifa zake,
Kwa maana hiyo  watu katika kundi la ‘baby boomer’ wana umri kati ya miaka 61 na 79 kwa mwaka huu wa 2025. Kwa idadi kulingana na taasisi mbali mbali [Shirika la Takwimu la Taifa linalosimamia Sensa ya Watu na Makazi, (National Bereau of Statistics: NBS), na Benki ya Dunia, idadi yao hapa nchini ni kama milioni tatu, ama asilimia tano, ya Watanzania .  
Wale walioko kwenye kundi la milenia, wana umri kati ya miaka 29 na 44, na idadi yao kulingana na taasisi hizo,  inakadiriwa kuwa kama nilioni 12 ama asilimia 20 ya Watanzania kwa kadirio. Ni sawa na kusema ni  kundi lenye watu wengi, na ambalo kwa idadi, ni mara nne ya lile la ‘baby’ boomer. Licha ya changamoto kadhaa, lakini kuna ndoa baina ya makundi haya kama ilivyo katika makala haya.
“Ni kweli kuna tofauti za kimtazamo katika baadhi ya mambo kati yangu na mke wangu, mathalan, mimi najali sana mambo ya maendeleo kitaifa, nikiona mtu anaonewa siwezi kupita bila kuhakikisha haki inapatikana;
Ninajali majaliwa ya taifa letu siku za usoni, na nipo tayari kujitolea kwa ajili ya jamii yangu,” anasema Fungamwango wakati alipotakiwa kufafanua baadhi ya mambo   anayopendelea katika fikra zake,
Sifa hizi anazozieleza  Mfungamwango, zinaelezwa na watafiti kuwa zinatokana na ukweli kwamba, ‘baby boomers’ walizaliwa katika kipindi cha harakati za kuleta mabadiliko katika jamii, na kupambania haki za binadamu, na hii ndiyo sababu ya wao kuwa hivi,
Kwa upande mwingine, tafiti zinaonesha kizazi cha  milenia, kimetekwa na  teknolojia, hasa kwa sababu wamekulia katika mazingira ya kuibuka na kushamiri kwa matumizi ya  ‘internet’. Wana mapokeo yenye uwanda mkubwa ikilinganishwa na baby boomer na hivyo kuwafanya wao kuwa huru. Wanapenda kuwa wajasirimali na wanafanya kazi kwa uwiano na uhuru. Wanajali sana mitindo ya mavazi na vifaa vingine

MIAMI, Marekani
Kocha wa klabu ya soka ya Inter Miami Javier Mascherano amejibu maoni ya Neymar kuhusu uwezekano wa kuungana tena na Lionel Messi na Luis Suarez katika klabu ya Inter Miami.
Akizungumza na vyombo vya habari, Mascherano alisema kuwa hawawezi kumzungumzia Neymar kwa sababu hawana lolote, japokuwa ni wazi kwamba Neymar ni mchezaji mkubwa.
Mascherano alisema kwamba kila kocha duniani anamtaka, lakini kwa sasa, Ligi yao inatawaliwa kuhusu kikomo cha mshahara kwa wachezaji, hivyo kwao kwa wakati huu, haiwezekani kujaribu kufikiria juu yake.
Neymar amekuwa akihusishwa na uwezekano wa kuondoka Al-Hilal msimu wa joto, huku timu hiyo ya Saudi Pro League ikiripotiwa kutokuwa na uwezekano wa kuongeza mkataba wake kwa mwaka mwingine.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32, amesalia kimya kuhusu mustakabali wake, huku akitarajia kupata tena utimamu kamili na kujenga mdundo ufaao kabla ya kutamba na Brazil kwenye Kombe la Dunia la 2026.
Neymar amekuwa akihusishwa na kutaka kujiunga na klabu ya Ligi Kuu ya Soka ya Inter Miami ili kuungana na wachezaji wenzake wa zamani wa Barcelona Messi, Suarez, Jordi Alba na Sergio Busquets, na kuchochea tetesi za uhamisho wiki ya jana.

MADRID, Hispania
Mkurugenzi Mtendaji wa Saudi Pro League, anadai uhamisho wa Vinicius Junior ‘ni suala la muda tu,’ huku Real Madrid wakipania kupata ofa nyingine kubwa.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Brazil, akiwa na umri wa miaka 24 tu, tayari ameona kuhamia Mashariki ya Kati kunakisiwa.
Imedaiwa kuwa kifurushi kilichovunja rekodi cha thamani ya Euro bilioni 1 (£854m/$1.1bn) kinawekwa akilingana katika ligi ambayo tayari inawahesabu magwiji wa Real Cristiano Ronaldo na Karim Benzema ndani ya safu yake.
Omar Mugharbel, Mkurugenzi Mtendaji wa Saudi Pro League, anaamini kwamba Vinicius atapita njia sawa ya kazi, wakati fulani katika siku zijazo zisizo mbali sana.
Kuvutiwa na Ligi ya Saudia kunaendelea kuimarika kote ulimwenguni, huku Mugharbel akiwa na imani kuwa wanaweza kushindana na timu zinazoongoza barani Ulaya.
Aliendelea kusema: “Sisi ni ligi namba moja barani Asia, lakini tunataka kuwa sehemu ya 10 bora duniani. Sasa hivi siwezi kukuambia tulipo. Tunapaswa kusubiri hadi mwisho wa msimu”.

DAR ES SALAAM

Na Remigius Mmavele

Sylvain Mbon, almaarufu Oxy-Oxygène alianza kazi yake katika bendi ya Choc Dallas katika mtaa aliochaguliwa na Petit kama mwimbaji, ingawa alikuwa na ndoto ya kuwa mpiga gita.  Mnamo 1990, alicheza kwa muda mfupi katika bendi ya Visa Mondial.  Katika mwaka huo huo, alijiunga na bendi ya Jean Juif Mava ya Cogiex Star.
Mnamo 1993, kikundi cha Cogiex Star kilipata shida kadhaa ambazo zilimfanya aachane nayo na kuanza harakati za uundaji wa bendi ya Extra Musica, ambayo alikuwa mwanzilishi mwenza. Katika kipindi cha miaka kumi na mmoja, alichoitumikia bendi hiyo, amehusika katika utunzi wa nyimbo kadhaa, zikiwemo: Nako bala yo na ko;  Génération méchante;  Ziya;  Innondation;  Cri du cœur (tuzo ya wimbo bora wa mwaka);  Moselekete;  Rufin Bouka na nyimbo nyingine nyingi zilizotolewa kwa majina ya baadhi ya wenzake.
Isivyo bahati, mnamo Desemba 16, 2004, aliachana na  kikundi cha Extra Musica na kuunda bendi yake aliyoipa jina la Universal Zangul.
Mnamo Septemba 2006, alitoa albamu ya Tapis Rouge na kuiingiza sokoni.Mnamo 2008, alianza kuandaa albamu ya Conjugaison, ambayo hapo awali ilikuwa opus ya kikundi.
Miaka mitatu baadaye, yaani mwaka 2011, albamu hiyo haikuwa kwenye soko la rekodi kutokana na sababu mbalimbali.
Wasanii kadhaa waliondoka kwenye kundi hilo, na albamu ya Conjugaison ilishindwa kuingia sokoni kutokana na changamoto kadhaa. Oxy-Oxygène aliamua kuanza kazi kwa bidii, na akasaini na kampuni ya uzalishaji ya Letiok.  Hatimaye ilikuwa Februari 2015 ambapo Conjugaison, albamu ya kwanza ya Jenerali Sotonyoto Oxy Oxygène, ilitolewa.
Albamu ya Conjugaison ina nyimbo kumi, ambazo ni: Mimi, Wewe;  Kwa magoti yako;  Mlinzi O;  Mhandisi wa kumbukumbu;  Mavazi ya pili;  Tonga ya zagazaga;  Zukuru;  Kaké elanga;  Anniv mapasa;  Maboko minei.

MADRID, Hispania
Mkurugenzi Mtendaji wa Saudi Pro League, anadai uhamisho wa Vinicius Junior ‘ni suala la muda tu,’ huku Real Madrid wakipania kupata ofa nyingine kubwa.
Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Brazil, akiwa na umri wa miaka 24 tu, tayari ameona kuhamia Mashariki ya Kati kunakisiwa.
Imedaiwa kuwa kifurushi kilichovunja rekodi cha thamani ya Euro bilioni 1 (£854m/$1.1bn) kinawekwa akilingana katika ligi ambayo tayari inawahesabu magwiji wa Real Cristiano Ronaldo na Karim Benzema ndani ya safu yake.
Omar Mugharbel, Mkurugenzi Mtendaji wa Saudi Pro League, anaamini kwamba Vinicius atapita njia sawa ya kazi, wakati fulani katika siku zijazo zisizo mbali sana.
Kuvutiwa na Ligi ya Saudia kunaendelea kuimarika kote ulimwenguni, huku Mugharbel akiwa na imani kuwa wanaweza kushindana na timu zinazoongoza barani Ulaya.
Aliendelea kusema: “Sisi ni ligi namba moja barani Asia, lakini tunataka kuwa sehemu ya 10 bora duniani. Sasa hivi siwezi kukuambia tulipo. Tunapaswa kusubiri hadi mwisho wa msimu”.

MIAMI, Marekani
Kocha wa klabu ya soka ya Inter Miami Javier Mascherano amejibu maoni ya Neymar kuhusu uwezekano wa kuungana tena na Lionel Messi na Luis Suarez katika klabu ya Inter Miami.
Akizungumza na vyombo vya habari, Mascherano alisema kuwa hawawezi kumzungumzia Neymar kwa sababu hawana lolote, japokuwa ni wazi kwamba Neymar ni mchezaji mkubwa.
Mascherano alisema kwamba kila kocha duniani anamtaka, lakini kwa sasa, Ligi yao inatawaliwa kuhusu kikomo cha mshahara kwa wachezaji, hivyo kwao kwa wakati huu, haiwezekani kujaribu kufikiria juu yake.
Neymar amekuwa akihusishwa na uwezekano wa kuondoka Al-Hilal msimu wa joto, huku timu hiyo ya Saudi Pro League ikiripotiwa kutokuwa na uwezekano wa kuongeza mkataba wake kwa mwaka mwingine.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32, amesalia kimya kuhusu mustakabali wake, huku akitarajia kupata tena utimamu kamili na kujenga mdundo ufaao kabla ya kutamba na Brazil kwenye Kombe la Dunia la 2026.
Neymar amekuwa akihusishwa na kutaka kujiunga na klabu ya Ligi Kuu ya Soka ya Inter Miami ili kuungana na wachezaji wenzake wa zamani wa Barcelona Messi, Suarez, Jordi Alba na Sergio Busquets, na kuchochea tetesi za uhamisho wiki ya jana.

DAR ES SALAAM

Na Mwandishi wetu

Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” Simon Msuva amefunguka kuwa hafikirii kurejea nchini kwa miaka ya hivi karibuni kutokana na kuwa bado anajiona ana uwezo wa kuendelea kupambana katika soka la ushindani nje ya nchi.
Msuva alisema kuwa pamoja na umri wake wa miaka 31, lakini haumfungi yeye kutundika daruga hivi karibuni na kufungua milango ya kurudi kucheza katika Ligi Kuu Tanzania.
Alidai kuwa muda ukifika atarejea nchini, ila kwa sasa bado ana njaa ya kutafuta fedha, na ikitokea amerudi Tanzania basi itakuwa ni mipango tu ya Mungu, ila kwa sasa bado sana kurejea nchini, kwani anatamani kuendelea kusakata kabumbu kwa miaka mingi zaidi nje ya nchi.
Alisema kuwa kwa sasa yeye maamuzi yake ya kuendelea kupambana nje ya nchi ni kuhakikisha anatafuta hela kwa kila hali, kwani bado ana nguvu kuliko vijana ambao kwa sasa wanaonekana wako vizuri uwanjani.
“Itakapofikia, nitarudi tu Tanzania wala Watanzania wasijali, ila kwa sasa bado sana naitafuta hela Waswahili wanasema kwa sasa nina njaa, kwani nataka kuendelea kutafuta hela sana, na wala siyo kurudi nchini kwa sasa”, alisema Msuva.
Alisema kuwa wakati ukifikia, ataweka wazi wazi kuwa ni wapi atakapomalizia soka lake, kama ni Simba au Yanga, ila kwa sasa bado hajafikiria kurudi, kwani mipango yake ni kuendelea kupambana kukusanya sana fedha.
Aidha, aliweka wazi kuwa maamuzi hayo ni ya kwake, na wala siyo ushauri wa mtu mwingine yeyote, kwani anachokifahamu ni kuwa muda bado unamruhusu kuendelea kuonekana sana uwanjani kutokana na uwezo aliokuwa nao.
Msuva alisema kuwa soka lake lazima atalimalizia Tanzania, hivyo kuhusu kuchaguliwa timu ya kucheza pale ambapo atakaporejea, siyo kitu ambacho atakiwekea kipaumbele, kwani anatamani kumaliza soka lake kwa heshima ili historia yake iendelee kuandikwa.
Aliendelea kudai kuwa siyo ndani ya miaka mitatu au minne ya hivi karibuni kurejea nchini, kwani bado ana nguvu za kutafuta hela katika soka la Kimataifa.
“Hayo ni maamuzi yangu mwenyewe, na siyo ya mtu mwingine kunichagulia nikacheze Simba au Yanga, kwani nina nguvu sana ya kukimbia zaidi ya wachezaji wengine vijana. Hivyo, sijachoka kama wengine wanavyodhani”, alisema Msuva.
Msuva ni mmoja ya wachezaji waliofanikiwa kuisaidia Taifa Stars kufuzu kucheza michuano ya Afcon mwaka 2027, na amekuwa msaada mkubwa katika timu hiyo kutokana na uwezo wake kuwa mkubwa.
Katika misimu ya karibuni, Msuva amekuwa akihusishwa kurudi katika klabu za nyumbani Tanzania lakini mwenyewe amesema bado hajaamua, na Watanzania wasiwe na wasiwasi ni wapi atakapocheza, kwani atahitaji muda wa kufikiria juu ya kucheza Simba au Yanga.