London, Uingereza
Meneja wa Arsenal Mikel Arteta, amekiri kuwa watakuwa wakiangalia kwa makini usajili unaowezekana, wakati wa dirisha la uhamisho la Januari.
The Gunners walitumia takribani pauni milioni 250 msimu huu wa joto, na kuleta wachezaji wapya nane, huku wakitafuta kuongeza ubora katika kikosi chao, ili kukabiliana na orodha ya mechi zilizojaa, na kushindania mataji katika mashindano mengi.
Msimu uliopita kampeni ya Arsenal iliharibiwa na majeraha, kwani walikuwa bila mlinzi Gabriel Magalhaes, kwa sehemu ya mwisho ya msimu na walicheza na kiungo Mikel Merino, kama mshambuliaji wa muda, walipomaliza wa pili katika Ligi Kuu kwa msimu wa tatu mfululizo, na walitolewa katika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa na Paris St-Germain.
Msimu huu The Gunners pia wamekuwa wakisumbuliwa na majeraha, mara baada ya kumpoteza Kai Havertz tangu siku ya ufunguzi, huku nahodha Martin Odegaard na Bukayo Saka, Gabriel Martinelli, Noni Madueke na Max Dowman wakiwa wamekosa nafasi.
Sasa baada ya majeraha kuwaathiri zaidi wachezaji washambuliaji, ni safu ya nyuma ya Arsenal inayoteseka, Arteta alilazimika kumchezesha Declan Rice, katika nafasi isiyojulikana ya beki wa kulia dhidi ya Brighton siku ya Jumamosi, kwa sababu Jurrien Timber alikuwa majeruhi, na Riccardo Calafiori alipata tatizo wakati wa mazoezi ya kupasha misuli.
Melboune, Australian
Uwanja wa Kriketi wa huko mjini Melbourne umekadiriwa kuwa hauridhishi, Baraza la Kriketi la Kimataifa (ICC) limethibitisha.
Uamuzi huo unamaanisha kuwa, Uwanja wa Kriketi wa Melbourne unapata pointi moja ya upungufu. Ikiwa uwanja unapata pointi sita za upungufu katika kipindi cha miaka mitano, unasimamishwa kuandaa kriketi ya kimataifa kwa miezi 12.
Ni mara ya kwanza uwanja nchini Australia, kuonekana kuwa chini ya kiwango, tangu ICC ibadilishe mfumo wake miaka miwili iliyopita.
Wiketi thelathini na sita zilianguka katika vipindi sita katika mechi ya Boxing Day, huku harakati nyingi za kushona zikitolewa kwa wapiga mpira wa kasi.
“Kwa wiketi 20 zikianguka siku ya kwanza, 16 siku ya pili na hakuna mpigaji hata mmoja aliyefikia nusu karne, uwanja ulikuwa hauridhishi kulingana na miongozo, na uwanja unapata pointi moja ya upungufu,” alisema mwamuzi wa mechi Jeff Crowe.
DAR ES SALAAM
Na Arone Mpanduka
Mchezo wa skwashi ulianzishwa karne ya 19 nchini Uingereza. Ulianza kama mabadiliko ya mchezo wa racquetball, na kuendelezwa katika shule za wasichana na wavulana.
Mchezo huu ulienea haraka katika nchi za Uingereza, kisha ulienea duniani kote, hasa katika nchi zilizoathiriwa na Wazungu kama Canada, Marekani, Australia, na baadhi ya nchi za Afrika.
DAR ES SALAAM
Na Remigius Mmavele
Rigobert Bamundele Ifoli, maarufu kwa jina Rigo Star, alizaliwa Agosti 28,1955 jijini Kinshasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).Rigo Star ni mpiga gita hodari aliyetikiza duniani kwa kupiga chombo hicho, alianza kuonyesha uwezo wake akiwa na umri mdogo ambapo alikuwa mmoja wa wapiga gitaa wenye ushawishi mkubwa nchini mwake.
Katika safu hii ya Chimba Chimba Historia ya Kanisa wiki iliyopita, tuliendelea kuwaletea historia ya mitaguso mikuu, kwa kuendelea na Mtaguso Mkuu wa Kostantinopole. Leo tunawaletea historia ya kuasi kwa Kanisa la Wakopti Misri, na historia ya Mababa wa Kanisa wa Magharibi. Sasa endelea…
Bahati mbaya, Wakristo wa Misri ambao kabla walikuwa kila mara wanashinda, na hivyo wakajiona kama watetezi imara wa imani, mara hii waliposhindwa hawakufurahi. Walishinda wakati wa Arius na walishinda wakati wa Nestorius, lakini sasa kwa kusisitiza mno umoja na umungu wa Kristo walishindwa.
Hawakupokea kushindwa, hivyo Kanisa zima likaendelea na uzushi huo ulioitwa ‘Monophysitism’, maana yake Yesu ni Mungu na utu wake umekandamizwa.
Bagamoyo
Na Laura Mwakalunde
Askofu wa Jimbo la Bagamoyo, Mhashamu Stephano Musomba, amewataka Waamini kutokuwa na Roho dhaifu, za kushindwa kuvumilia shida na matatizo.
Askofu Musomba alisema hayo hivi karibuni, wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Dominika ya Tatu ya Furaha ya Majilio, iliyofanyika katika Parokia ya Bikira Maria wa Mlima Karmeli-Bunju, jimboni humo.
Mgeta
Na Angela Kibwana
Zaidi ya watoto Wamisionari 300 wa Shirika la Kipapa, Dekania ya Mgeta Jimboni Morogoro, wameshiriki Kongamano la kufunga mwaka, katika dekania hiyo.
Kongamano hilo limefanyika katika Parokia ya Bikira Maria wa Mlima Karmeli-Mgeta, Morogoro, likihusisha watoto kutoka Parokia sita zinazounda Dekania hiyo, kama njia mojawapo ya kuwakuza watoto kiimani na kimaadili, kupitia mafundisho ya semina na michezo mbalimbali.
Dar es Salaam
Na Laura Mwakalunde
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Sana Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, amewataka Waamini kutambua kwamba, Karamu ya Sakramenti Takatifu haikuja ili kushibisha tumbo.
Askofu Ruwa’ichi alisema hayo hivi karibuni, wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya kuzindua Mnara wa Kanisa, iliyofanyika Parokia ya Mwenyeheri Anuarite-Makuburi, jimboni humo.
Morogoro
Na Angela Kibwana
Mhashamu Askofu Lazarus Vitalis Msimbe -SDS, wa Jimbo Katoliki Morogoro, ameongoza Misa Takatifu ya Sherehe ya Bikira Maria Mkingiwa dhambi ya asili, Msimamizi wa Jimbo hilo, na kuwataka Waamini jimboni humo kukimbilia maombezi yake mara kwa mara, ili Jimbo liweze kustawi kiroho na kimaendeleo.
Adhimisho hilo lilifanyika katika Kanisa Kuu la Mtakatifu Patris, jimboni Morogoro, iliyokwenda sambamba na kufunga mwaka Mtakatifu wa Jubilei ya matumaini miaka 2025, jozi 44 za ndoa Takatifu, pamoja na kutoa shukrani kwa Mungu, kwa mavuno ya Tegemeza Jimbo mwaka huu 2025.
Kisarawe – Pwani
Na Mathayo Kijazi
Chansela wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Padri Vincent Mpwaji, amewaalika Wakristo kutafakari na kutambua kwamba jukumu lao la kwanza la msingi, ni kuwa Mashahidi wa Yesu Kristo.
Padri Mpwaji aliyasema hayo katika homilia yake, wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Sakramenti ya Kipaimara kwa vijana 21, katika Parokia ya Mtakatifu Joseph Cottolengo – Masaki - Kisarawe, jimboni humo.
Dar es Salaam
Na Mathayo Kijazi
Imeelezwa kuwa kila anayepokea Sakramenti Takatifu ya Kipaimara, anatumwa kuwa Mkristo kweli aliye tayari kuacha dhambi na kumrudia Mungu, huku akiwa mtu wa toba.
Hayo yalisemwa na Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Henry Mchamungu, wakati wa homilia yake katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Sakramenti ya Kipaimara kwa vijana 72, katika Parokia ya Mtakatifu Maria Magdalena – Kimara Mtoni, jimboni humo.
LILONGWE, Malawi
Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Lilongwe, nchini Malawi, Mhashamu Vincent Frederick Mwakhwawa, amewataka Waamini kudumisha heshima na uvumilivu wakati wa Misa, akisisitiza kwamba sherehe ya Ekaristi haipaswi kukatizwa kamwe, hata wakati wa changamoto.
Wito huo aliutoa hivi karibuni wakati wa ziara yake ya Kitume, katika Parokia ya Mtakatifu Paulo - Namitete, jimboni humo, ambapo yeye binafsi aliwashukuru na kuwatia moyo washiriki wa Utoto Mtakatifu (Watoto wa Wamisionari).
LILONGWE, Malawi
Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Lilongwe, nchini Malawi, Mhashamu Vincent Frederick Mwakhwawa, amewataka Waamini kudumisha heshima na uvumilivu wakati wa Misa, akisisitiza kwamba sherehe ya Ekaristi haipaswi kukatizwa kamwe, hata wakati wa changamoto.
Wito huo aliutoa hivi karibuni wakati wa ziara yake ya Kitume, katika Parokia ya Mtakatifu Paulo - Namitete, jimboni humo, ambapo yeye binafsi aliwashukuru na kuwatia moyo washiriki wa Utoto Mtakatifu (Watoto wa Wamisionari).
VATICAN CITY, Vatican
Baba Mtakatifu Leo XIV amekutana na kuzungumza na Rais wa Mongolia, Ukhnaagiin Khürelsükh, katika Jumba la Kitume mjini Vatican, ambapo baadaye Rais huyo alikutana pia na Kardinali Pietro Parolin, Katibu Mkuu wa Vatican akiambatana na Monsinyo Mih Blaj, Katibu Msaidizi wa Mahusiano na Mataifa.
Katika majadiliano yao katika Sekretarieti ya Jimbo, Papa na Rais huyo walizungumzia pia uhusiano mzuri kati ya Vatican na Mongolia, kwa nia ya kuuendeleza pia katika nyanja ya kitamaduni.