NJOMBE
Na Mwandishi wetu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dk. John Jingu, amewataka Maafisa Maendeleo ya Jamii mkoani Njombe, kutunza na kutumia kwa umakini pikipiki walizopewa na serikali, ili kuboresha utendaji na utoaji wa huduma kwa wananchi.
Dk. Jingu alisema hayo wakati wa hafla ya makabidhiano ya pikipiki nane, kwa Maafisa Maendeleo ya Jamii wa ngazi ya Kata, mkoani humo.
Dar es Salaam
Na Mwandishi wetu
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila amesema kwamba huduma ya mabasi yaendayo haraka (Mwendokasi) katika barabara ya Morogoro kuelekea Kimara, Moroco na Barabara ya Kilwa kutoka katikati ya mji kwenda Mbagala imesitishwa kwa muda.
Hatua hiyo imetokana na kuaharibika kwa miundombinu ya barabara hizo.
Chalamaila (pichani) alitoa tamko hilo jijini Dar es Salaam mbele ya Waandishi wa Habari na kutaja kuwa kwa sasa Serikali ipo katika hatua ya kufanya tathmini ya hasara iliyopatikana na kufanya ukarabati wa miundombinu hiyo, hivyo pindi itakapokaa sawa huduma hiyo itarejea.
“Tumelazimika kusitisha huduma ya usafiri huo kutokana na uhalifu uliofanyika wakati wa uchaguzi na kundi la waandamanaji na kusababisha kuharibika kwa mifumo yote ya ukatajai tiketi na sehemu za kupakilia abiria hivyo sasa tunatoa maelekezo kwa LATRA kutoa vibali vya muda kwa wamiliki wa daladala hili waweze kuwahudumia wakazi wa maeneo hayo ambao kwa sasa wanahitaji kufika mjini,”alisema Chalamila.
Tabora
Na Munir Shemweta
Zoezi la uthamini wa maeneo, yatakayopitiwa na ujenzi wa Mradi wa Reli ya Kisasa (Standard Gage Railway-SGR), kipande cha sita kutoka Tabora hadi Kigoma, linaendelea kwa kasi katika Wilaya sita za mikoa hiyo.
Wilaya hizo ni Tabora Mjini, Uyui, Urambo, Kaliua, Uvinza pamoja na Wilaya ya Kigoma.
Timu kutoka Ofisi ya Mthamini Mkuu wa Serikali, ikiongozwa na Mthamini Kiongozi FRV James Mark Mwanakatwe, ipo mkoani Kigoma, ikiendelea na kazi ya uhamasishaji pamoja na ukusanyaji taarifa za mali uwandani, kwa wananchi ambao maeneo yao yanaguswa na mradi huo.
Bagamoyo
Na Mathayo Kijazi
Wakristo wametakiwa kuepuka kiburi na majivuno, kwa kudhani bila wao mambo hayawezi kufanyika katika Kanisa, na jamii kwa ujumla.
Hayo yalisemwa hivi karibuni na Askofu wa Jimbo Katoliki la Bagamoyo, Mhashamu Stephano Musomba -OSA, wakati wa homilia yake katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Dominika, sanjari na kutoa Sakramenti Takatifu ya Kipaimara, katika Parokia ya Mtakatifu Toma – Muungano, jimboni humo.
“Tunaona katika Injili ya leo, yule Farisayo anamwambia Mungu ‘Mbona huoni? Mimi niko moja, mbili, tatu, mimi nafanya hiki na hiki, siwezi kuwa kama huyo, huyo ni mdhambi, huyo anatoza ushuru. Kwa hiyo anaona kwamba yeye ni bora kuliko yule mwingine. Na ndio maana kwa kuigaiga, tunaweza kusahau njia yetu ya kumwelekea Mungu.
DAR ES SALAAM
Na Mwandishi wetu
Waamini wametakiwa kufuata mafundisho ya Bwana Yesu Kristo na mwenendo wake, kwa kuwarithisha watoto wao Imani Katoliki.
Wito huo ulitolewa hivi karibuni, na Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Augustino-Salasala, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Padri Peter Assenga, wakati akitoa homilia yake katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Sakramenti ya Ubatizo na Ekatisti.
“Mkristo kamili lazima awe amebatizwa na mwenye kushiriki Ekaristi Takatifu, na kufanya maungamo mara kwa mara,” alisema Padri Assenga.
Aidha, aliwasihi Waamini kutopokea Ekaristi Takatifu kama pipi, kwa sababu ni kufuru na ni dhambi.
ASMARA, Eritrea
Kanisa nchini Ethiopia na Eritrea, limeadhimisha Jubilei ya Miaka 50, ya kuinuliwa hadi utakatifu wa Mtakatifu Justin De Jacobis, kwa Misa Takatifu ya Shukrani iliyoongozwa na Askofu Mkuu Menghisteab Tesfamariam, akiambatana na wakubwa wa kidini na Mapadri zaidi ya 20, wa sherehe katika Kanisa Kuu la Mama Yetu wa Msaada wa Daima-Kidane Mehret.
Katika barua yake kwa Waamini wote na makutaniko ya kidini nchini, Askofu Mkuu Tesfamariam, aliwaalika kushiriki katika tukio hilo maalumu la kumshukuru Mungu na kumheshimu Mtume wa Imani Katoliki nchini, Mtakatifu Justin de Jacobis, ambaye alipandishwa cheo na Baba Mtakatifu Paulo VI, mnamo Oktoba 26, 1975.
NAIROBI, Kenya
Wanafunzi wa Vyuo Vikuu kutoka Taasisi 26 za Elimu ya Juu nchini Kenya, wamepewa ujuzi unaojumuisha ubora wa kiakili na huduma ya kujitolea, ili kufikia uongozi wenye mabadiliko na athari kubwa kwa jamii.
Programu ya Uongozi ya Kizazi Kijacho (NGLP), ambayo hapo awali ilikuwa Programu ya Udhamini wa Kikatoliki, ambayo inazingatia mafunzo ya kitaaluma na uongozi kwa wanawake, wanaume, na Waamini wa kidini wa Kiafrika, inawafunza wasomi wake kuwa Miale ya Matumaini, ambapo imeitwa Kutumikia, Kubadilisha, na Kuhamasisha.
Katika tafakari iliyotolewa na Padri John Webootsa, mwanachama wa Comboni Missionaries of the Heart of Jesus (MCCJ), kwa zaidi ya wanafunzi 150 wakati wa kumbukumbu zao katika Bustani ya Ufufuo, katika Mji Mkuu Nairobi, Kenya, alisema kuwa jamii kwa sasa ina njaa ya uongozi halisi na uwazi wa maadili.
VATICAN CITY, Vatican
Katibu Mkuu wa Vatican, Mwadhama Pietro Kardinali Parolin, ametaka ushiriki wa Marekani na jukumu kubwa kwa Ulaya, katika juhudi za kukomesha mzozo wa Ukraine, akisisitiza kwamba China pia ina neno la kusema kwa ajili ya amani.
Aliyasema hayo hivi karibuni, aliposhiriki katika Hospitali ya Watoto ya Bambino Gesù, akiashiria kumbukumbu ya miaka 40 ya kutambuliwa kwake, kama Taasisi ya Kisayansi ya Kulazwa Hospitalini na Matibabu.
Akizungumzia mkutano na Waziri Mkuu wa Hungaria, Viktor Orbán, aliuelezea kama majadiliano mazuri, na kwamba wanajaribu kuleta misimamo yao karibu zaidi.
DAR ES SALAAM
Na Shemasi George Timalias
Karibu ndugu msikilizaji wa Radio Vatican, katika tafakari hii, inayotugusa kwa karibu sana, ambayo inakumbusha Sikukuu ya Watakatifu wote, kila ifikapo tarehe Mosi Novemba ya kila mwaka, lakini pamoja na Watakatifu, kuna ndugu zetu Marehemu wote waliotutangulia mbele ya haki, ambapo Mama Kanisa anatupatia fursa ya kuwakumbuka, kila ifikapo tarehe 2 ya mwezi Novemba na kuendelea hadi mwisho wa mwezi.
Kwa hiyo tuanze tafakari hii, sehemu ya kwanza ya Watakatifu. Fundisho kuu tunalopata katika siku hii ya watakatifu wote, ni msisitizo wa maisha yetu kuishia mikononi mwa Mungu aliyetuumba huko mbinguni.
Katika safu hii ya Chimba Chimba Historia ya Kanisa wiki iliyopita, tuliendelea kuwaletea historia ya kuibuka kwa Dola ya Kikristo, hususani tuliwajuza kuhusu Faida na Hasara za Dola ya Kikristo. Leo tunawaletea historia ya Miundombinu ya Kanisa kuanzia Karne ya nne na tano. Sasa endelea…
Watumishi wa Kanisa na Mitaguso:
Bwana wetu Yesu Kristo, aliacha amewachagua na kuwaweka mitume 12 na wafuasi 70 (72), ili waendeleze kazi aliyoianza (Lk. 6:13-16; 10:1-12). Hawa walirithiwa kama Maaskofu na Mapadri.
Katika Kanisa la mwanzo, polepole kufuatana na mahitaji katika misingi aliyoiweka Kristo, miundombinu hiyo iliongezeka na kuboreshwa.
Kuanzia Karne ya nne na tano, palikuwepo na madaraja saba katika watumishi wa Kanisa. Kati ya madaraja hayo, madogo ni manne yakiwemo Mfungua Mlango, Msomaji, Mtoa Mashetani na Mtumishi wa Ibada, na madaraja makubwa ni matatu, Ushemasi, Upadri na Uaskofu.
Padri Andreas Chitanda Paroko wa Parokia ya Bikira Maria Malkia-Luagala Jimbo Katoliki la Mtwara, akibariki kinanda kipya cha Kigango cha Kutukuka kwa Msalaba-Lyenje jimboni humo, wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Dominika iliyoadhimishwa hivi karibuni.
Waimarishwa wa Sakramenti Takatifu ya Kipaimara wa Parokia ya Mtakatifu Toma – Muungano, Jimbo Katoliki la Bagamoyo, wakiwa katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Sakramenti hiyo, iliyoadhimishwa hivi karibuni parokiani hapo. (Picha na Mathayo Kijazi)
Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo, Askofu Mkuu Mstaafu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Kamati Tendaji ya Parokia ya Mtakatifu Yakobo Mkuu-Mtume, Mabwepande jimboni humo. Wa tatu kulia ni Paroko wa Parokia hiyo, Padri Thomas Mtei na kushoto ni Paroko Msaidizi, Padri Dickson Sambala.
Moshi
Na Paul Charles Mabuga
Wiki moja tu inatosha kunasa moyo wako, katika mtego mtamu wa pilikapilika za Moshi. Huu si mji wa kawaida, bali ni lulu iliyolala katika kivuli kitukufu cha Mlima Kilimanjaro.
Huku ukiahidi utulivu wa kitalii, uhalisia wake umejaa mizunguko ya kusisimua, milio isiyotarajiwa, na siri za kitabibu zinazofichwa kwenye glasi ya maziwa ya ngamia, na kikombe cha kahawa bora kabisa duniani.
Nilipowasili, hali ya hewa ilinikumbatia kwa ubaridi laini wa majira haya, ule unaochochea hamu ya kahawa ya moto hata mchana. Lakini ghafla, palikuwa na mabadiliko ya joto! Joto jipya lilianza kuhisiwa ghafla, kana kwamba Mlima Kilimanjaro ulikuwa umeamua kuachia pumzi yake ya joto badala ya baridi. Mabadiliko haya ya ghafla yananukia mabadiliko ya tabianchi, yanayobadilisha mood ya mji.