Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

New York, Marekani
Shirikisho la soka Duniani, FIFA, limetangaza kupiga marufuku matumizi ya vuvuzela na filimbi, ndani ya viwanja vyote, vitakavyotumika katika kombe la Dunia 2026, nchini Marekani, Canada na Mexico.
Kwa mujibu wa kanuni mpya za viwanjani, mashabiki watakaobainika na vifaa hivyo, katika lango la kuingia watanyang’anywa au kuzuiwa kuingia uwanjani. Hatua hiyo, inalenga kuboresha mazingira ya mechi kwa wachezaji, waamuzi, watazamaji na watangazaji.
Uamuzi huo unatarajiwa kuzua mjadala mkubwa hasa barani Afrika, ambapo vuvuzela ilijizolea umaarufu mkubwa, wakati wa kombe la Dunia la mwaka 2010, nchini Afrika Kusini. 
Kwa wengi, vuvuzela ni sehemu ya utamaduni wa soka wa Afrika, na huchangia hali ya shamrashamra viwanjani, huku wengine wakidai kelele zake, huathiri mawasiliano ya wachezaji, na ubora wa matangazo ya televisheni.
FIFA imesema kwamba, marufuku hiyo ni sehemu ya juhudi za kuhakikisha usalama, uratibu na mazingira yenye udhibiti zaidi, katika mashindano hayo yatakayoshirikisha timu 48 kwa mara ya kwanza, katika historia ya kombe la Dunia.

New York, Marekani
Serena Williams anasema kwamba, hana cha kuthibitisha kurudi kwake kwenye tenisi ya ushindani, baada ya kutokuwepo kwa karibu miaka minne, akiongeza kuwa motisha yake kuu, ni matarajio ya binti zake kumuona akicheza tena.
Bingwa huyo mara 23 wa ‘Grand Slam single’, raia wa Marekani alisema kuwa, hakuwa akijiwekea shinikizo lolote anaporudi kwenye mchezo, ambao aliutawala kwa miaka mingi.
Williams alijifungua Olympia, ambaye sasa ana umri wa miaka minane, mnamo 2017, na akarudi kwenye tenisi miezi michache baadaye, na kufikia fainali nne kuu za single, baada ya kupata binti yake mkubwa.
Binti yake wa pili, Adira, alizaliwa mwaka wa 2023, na hajawahi kumuona mama yake akicheza kwenye nyanja hiyo.
Alipoulizwa umuhimu wake wa kuonesha bado anaweza kushinda, Williams alijibu kuwa hahitaji kushinda, kwani ameshinda zaidi ya watu wengi, katika maisha yao yote.
“Kuwa na fursa ya kuweza kufanya hivyo mara ya mwisho, ni jambo la kufurahisha na la kusisimua pia, ni kwamba, kuwa mwanariadha ni jambo bora zaidi, ambalo unaweza kuwa katika nafasi ya juu zaidi”, alisema Serena.

DAR ES SALAAM

NA NICHOLAUS KILOWOKO

Wakati kikosi cha Yanga SC, kikiendelea na mazoezi kujiandaa na mechi tano za mwisho za Ligi Kuu, mchezaji wa klabu hiyo, Salum Aboubakar maarufu Sure Boy, amefunguka siri ya wachezaji wengi vijana, kushindwa kuonesha uwezo wao viwanjani.
Sure Boy alikiri kuwa katika ligi kuu, ushindani umekuwa mkubwa sana, lakini pia ushindani huo unahitaji sana ubora wa wachezaji, lakini hilo limekuwa tofauti sana, kwa wachezaji wengi vijana, ambao pia wanapata nafasi ya kucheza, lakini hawajitoi kwa asilimia zote.

DAR ES SALAAM

LAURA CRISPIN

Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam limeanzisha Klabu ya michezo itwayo St. Joseph Sport Club’ ili kuimarisha shughuli za uinjilishaji kupitia michezo, kuboresha afya na kutoa ajira kwa vijana.
Akizungumza na Tumaini Letu katika mahojiano maalum yaliyofanyika hivi karibuni, Padri Vitalis Kassembo, Mkurugenzi wa Walei Jimbo Kuu la Dar es Salaam alisema kwamba kitu kilichowasukuma kuanzisha timu ya mpira wa miguu ya St. Joseph Sport Club ni kwa ajili ya muendelezo wa Warsha ya Walei.
 “Tumeanzisha klabu ya St. Joseph Sports kwa lengo la kuinjilisha kupitia michezo, kuwafanya vijana wawe na afya nzuri pamoja na kuwapatia vijana ajira kupitia michezo, japokuwa siyo wote ni kwa wale wenye vipaji vya michezo,”alisema Padri Kassembo.
Alisema kuwa mara zote wamekuwa wakipoteza timu baada ya Warsha kuisha na kuwafanya kila mwaka kutafuta timu mpya.
Padri Kassembo aliendelea kusema kuwa wameanzisha timu hiyo kwa lengo la kuacha alama ya Jubilee ya Miaka 75 ya Jimbo Kuu la Dar es Salaam na kujenga mwili wenye afya pamoja na Roho yenye afya.
Alibainisha kwamba klabu hiyo ya St. Joseph Sport inabebwa na kauli mbiu ambayo wataishi siku zote katika michezo, ambayo ni ‘Imani, Michezo na Ushindi’.
 Padri Kassembo aliendelea kusema kwamba, ikiwa wataishi katika kauli mbiu yao ya imani, michezo na ushindi basi mapato yatakayopatikana kupitia timu hiyo, yataenda kusaidia ujenzi wa Kanisa mbadala Pugu.

BAGAMOYO

Askofu wa Jimbo Katoliki la Bagamoyo, Mhashamu Stephano Musomba, alisema kuwa siasa ni neno zuri ila watu wameliharibu, kwa kutumia uongo na kupotosha.
Askofu Musomba alisema hayo wakati akitoa homilia yake, katika Ibada ya Ijumaa Kuu, iliyofanyika katika Parokia ya Bikira Maria wa Mlima Karmeli-Bunju, jimboni humo.
“Ukweli mara zote unauma, japo unaponya na ni mchungu, ingali huwa ni mtamu kama asali, ikiwa utatenda katika mastahili ya ukweli,” alisema Askofu Musomba.
Aidha, aliwasihi Waamini kusikiliza kila wanachoambiwa, kwa sababu kitawafanya wawe bora zaidi, japokuwa wakati mwingine huzaliwa ‘machawa’, ambao kazi yao ni kusifia bila kukosoa, wakifanya hivyo kwa ajili ya kujipatia kipato tu.

Na Mwandishi wetu

Katika kuadhimisha Sikukuu ya Pasaka mwaka huu, jamii imeonywa kuacha tabia ya kukimbilia kuchukua picha na video katika majanga, na kuanza kuzituma mitandaoni, badala yake waanze kutoa msaada kwa watu waliokumbwa na mkasa huo.
Onyo hilo lilitolewa hivi karibuni, na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Sana Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, akiwataka watu wenye tabia ya kupiga picha na kuchukua video kwenye majanga, bila ya kutoa msaada, kuacha mara moja kufanya hivyo.

Na Edvesta Tarimo

Matumizi ya dawa za kulevya, yanaendelea kuwa tishio kubwa kwa afya ya akili na uchumi wa taifa, huku wataalamu wakionya kuwa bila hatua za pamoja, jamii itaendelea kupoteza nguvu kazi yake, hususani vijana.
Matumizi ya madawa ya kulevya yameendelea kuongezeka duniani, huku Ripoti ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2023, ikionesha kuwa idadi ya watumiaji wa dawa za kulevya duniani, ilifikia milioni 316, sawa na 6% ya idadi ya watu wenye umri wa kati ya miaka 15–64.

Katika safu hii ya Chimba Chimba Historia ya Kanisa wiki iliyopita, tuliendelea kuwaletea  historia ya Kanisa kuibuka kuwa Mlezi wa Elimu, Leo tunaendelea kuwaletea historia ya kuibuka kwa mashirika yalianzishwa kwa ajili ya kuimarisha moyo huo Mtakatifu wa kidini. Sasa endelea…

Wakartusiani:
Wakartusiani walikuwa aina ya wakaa pweke, kwa mfano wa Mtakatifu Antoni wa Jangwani, ila waliishi pamoja bila mawasiliano. Wamonaki hawa walisali pamoja na kufunga, bila kuongea au kuwa na mawasiliano na watu wengine wa nje.
Hawa walianzishwa na Mtakatifu Bruno mwaka 1084. Shirika hili lilikuwa thabiti kiasi kwamba mashirika mengine yalipolegea, lenyewe lilibaki imara bila kupakwa uchafu wa dunia. Palikuwa na msemo kwamba, hapajakuwa na ulazima wa kurekebisha shirika hili, kwa sababu halijateteleka kwa uozo (never reformed because never deformed).
Wengi wao walikufa mashahidi, wakati wa Waprotestanti kwa kukataa kuacha Utawa. Kwa kufuata mfano huo, yalianzishwa mashirika mengine kama Wasistesiani, walioimarishwa na Mtakatifu Bernardo wa Clairvaux mwaka 1090.

Wanakwaya wa Kwaya ya UKWAKATA Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam wakiimba wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Jumatatu ya Pasaka, Kijimbo iliyoadhimishwa katika Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu - Manzese jimboni humo. Wengine ni Waamini walioshiriki Adhimisho hilo.

Waamini wa Parokia ya Mtakatifu Rita wa Kashia - Goba, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, wakishiriki Adhimisho la Misa Takatifu ya Ibada ya Ijumaa Kuu iliyofanyika parokiani hapo.