Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Manchester, Uingereza
Cristiano Ronaldo amesema Meneja wa Manchester United Ruben Amorim hatofanya miujiza kwa sababu kwa sasa klabu haipo katika njia nzuri.
Mshambuliaji huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 40 alijiunga na Al-Nassr muda mfupi baada ya kumaliza kipindi chake cha pili akiwa na United mnamo Novemba 2022.
Mchezaji mwenzake wa zamani wa Ureno, Amorim alichukua nafasi ya Erik ten Hag kama bosi mnamo Novemba 2024 na United ikamaliza msimu uliopita katika nafasi ya 15 kwenye Ligi ya Premia ukiwa mwisho wao mbaya zaidi wa ligi tangu washushwe daraja kutoka ligi kuu mnamo msimu wa 1973-74.

DAR ES SALAAM

Na Nicholausi Kilowoko

Timu ya Umoja wa Maveterani wa Soka Tanzania (UMSOTA), imeahidi kuendelea kushiriki mashindano mbalimbali ndani na nje ya nchi, kwa lengo la kuimarisha umoja na kukuza michezo.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa UMSOTA, Paul Ambrose Lusozi maarufu kama Father, huku akiishukuru serikali kwa kutambua mafanikio yao kimataifa.
Timu hiyo ilitwaa ubingwa wa mashindano ya soka ya Maveterani Afrika Mashariki, yaliyofanyika Oktoba mosi mwaka huu, huko nchini Kenya.

DAR ES SALAAM

Na Arone Mpanduka

Beki wa zamani wa timu ya Taifa Stars, Simba, CDA na Azam FC, Boniface Pawasa amezitaka timu nne zinazoshiriki hatua ya makundi ya michuano ya kimataifa ngazi ya klabu kuondoa woga.
Pawasa ametoa ushauri huo zikiwa ni siku chache zimepita tangu timu za Simba, Yanga, Azam FC na Singida Black Stars kuwafahamu wapinzani itakaokutana nao katika hatua ya makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa na Shirikisho Afrika.
Akizungumza na Tumaini Letu, Pawasa alisema hivi sasa soka la Afrika limebadilika sana tofauti na ilivyokuwa miaka ya zamani, hivyo kila timu ijiandae kupambana vilivyo ili kwenda hatua ya robo fainali.

Shinyanga

Na Angela Kibwana

Mhashamu Askofu Liberatus Sangu wa Jimbo Katoliki la Shinyanga, amewata Wakatoliki kuendelea kuombea na kulinda amani ya nchi, hasa kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Jumatano Oktoba 29 mwaka huu, ili uwe huru na haki.
Askofu Sangu alisema hayo, wakati akihubiri katika Adhimisho la Misa Takatifu, iliyofanyika Parokia ya Mt. Rosa wa Lima – Kitangili jimboni humo, akiwakumbusha Wakatoliki kumuomba Mama Bikira Maria, alinde familia zao na Taifa kwa ujumla kuelekea Uchaguzi Mkuu, kabla na baada ya uchaguzi huo.

Visiga

Na Laura Mwakalunde

Makamu wa Askofu wa Jimbo Katoliki la Bagamoyo, Padri Edward Sabbas amesema kwamba, Taifa linaloshindwa kufuata misingi bora ya utu hupotoka.
Padri Edward alisema hayo hivi karibuni, wakati akihubiri katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Mahafari ya Kidato cha Nne, katika Seminari Ndogo ya Maria –Visiga, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam.

Dar es Salaam

Na Mwandishi Maalumu

Watanzania wametakiwa kujenga utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara, hasa magonjwa yasiyo ambukiza, ili kuepuka madhara zaidi.
Rai hiyo ilitolea hivi karibuni, na Daktari Bingwa wa magonjwa ya ndani kutoka Taasisi ya Saratani Ocean Road, jijini Dar es Salaam, Dk. Kezia Tessua, wakati akizungumza na Wananchi katika eneo la Bunju, kwenye Programu ya Viongozi Wanawake, inayosimamiwa na Taasisi ya Uongozi.

Dar es Salaam

Na Celina Matuja

Wanafunzi wanaohitimu masomo yao ya Sekondari, katika Shule ya Msingi na Sekondari ya St. Rosalia Kinyerezi, jijini Dar es Salaam, wanapaswa kuangalia fursa za kusomea ubaharia, kwani ni taaluma inayoweza kuwasaidia maishani.
Wito huo ulitolewa na CPA Pascal Karomba, Mkurugenzi wa Fedha wa Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC), wakati akizungumza katika mahafali ya shule hizo, kwa Shule ya Awali, Msingi na Sekondari, ili wapate elimu hiyo nzuri ya ubaharia.
Aidha, Karomba aliupongeza uongozi wa shule hizo, kwa kuiona kiu ya Watanzania juu ya elimu, kuondoa ujinga kwa watoto wa kitanzania.

Dar es Salaam

Na Laura Mwakalunde

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Sana Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, amewaonya Waamini kuacha kuwa Wakristo goigoi.
Aliyasema hayo hivi karibuni, wakati akitoa homilia yake katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Sakramenti Takatifu ya Kipaimara, iliyofanyika Parokia ya Bikira Maria wa Fatima-Msimbazi, jimboni humo.

Mahenge

Na Mathayo Kijazi

Askofu wa Jimbo Katoliki la Mahenge, Mhashamu Agapiti Ndorobo, amesema kuwa kuelekea katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, ni vyema kuchagua kiongozi anayefaa na anayejali kila mmoja, bila kuangalia dini, rangi, kabila, wala utaifa wake.
Askofu Ndorobo aliyasema hayo hivi karibuni, wakati wa homilia yake katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Jubilei ya Miaka 75, ya Seminari ya Mtakatifu Francis – Kasita, jimboni humo.

Dar es Salaam

Na Mathayo Kijazi

Imeelezwa kuwa imani ya kweli si kujisifia, kujivuna, wala kujiona, bali kujishusha.
Hayo yalisemwa na Monsinyori Novatus Mrighwa, Mwalimu wa Seminari Kuu ya Mtakatifu Karoli Lwanga – Segerea, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, wakati wa homilia yake katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Sakramenti ya Kipaimara, katika Parokia ya Mtakatifu Gaudance - Makoka, jimboni humo.