Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Watoaji kashfa wawekwa ‘kikaangoni’

Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Henry Mchamungu akiongoza Ibada ya Ijumaa Kuu katika Parokia ya Bikira Maria Msaada wa Daima, Kimara- Korogwe, jimboni humo. Kushoto ni Paroko wa Parokia hiyo, Padri Paul Mushi, na kulia ni Shemasi Yohana Marunda. (Picha na Yohana Kasosi) Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Henry Mchamungu akiongoza Ibada ya Ijumaa Kuu katika Parokia ya Bikira Maria Msaada wa Daima, Kimara- Korogwe, jimboni humo. Kushoto ni Paroko wa Parokia hiyo, Padri Paul Mushi, na kulia ni Shemasi Yohana Marunda. (Picha na Yohana Kasosi)

Dar es Salaam

Na Mwandishi wetu

Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Henry Mchamungu, amewaonya watu wenye tabia ya kusengenya, kuponda na kuwachafua wengine kwa maneno mabaya ya kashfa.
Askofu Mchamungu alisema hayo wakati akitoa homilia yake katika Ibada ya Ijumaa Kuu, iliyofanyika katika Parokia ya Bikira Maria Msaada wa Daima, Kimara Korogwe.
“Katika jamii pia watu wengine kazi yao ni kuponda wengine na kusengenya watu wengine. Wanatumia midomo yao vibaya kusema mabaya juu ya wengine, hawa hawana tofauti na wale waliomtemea mate Yesu Kristo,”alisema Askofu Mchamungu.
Askofu Mchamungu alisema kuwa katika jamii ya sasa pia wapo watu wengine ambao kazi yao ni kuchafua sifa za watu kwa kuwashuhudia maneo ya uongo, jambo alilosema ni baya katika maisha.
Ataka wenye mamlaka kutoa haki
Aliwataka waamini kuhakikisha wanatetea haki za wengine, na kutoogopa maneno ya watu kama alivyofanya Pilato, hasa wanapokuwa katika nafasi za kutetea haki za wengine.
“Kila mmoja kwa nafasi yake ajitahidi kutetea haki za jamii, hasa wanapoona kitu kimekuwa siyo sahihi,”alisema Askofu Mchamungu.
Kwa upande wake Ibrahimu Meresho, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Walei Parokia ya Kimara Korogwe, alisema kuwa wapo katika mkakati wa ujenzi wa Kanisa kubwa jipya na la kisasa, kwani kila kitu kimefanyika.
“Kwa sasa vibali vyote vya ujenzi vimeshapatikana. Tunatafuta mtu wa kurekebisha tu ramani yetu, na baada ya hapo tutaipelekea kwa Baba Askofu ili naye aiangalie na kutoa baraka zake ili ujenzi uanze kufanyika,”alisema Meresho.
Parokia ya Kimara Korogwe haina Kigango hata kimoja, na ina mwaka mmoja tu tangu itangazwe kuwa Parokia kamili, ikiwa na Kanda tano na Jumuiya 20, ikiongozwa na Mapadri wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.