Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha
Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Judith Nguli, akipokea vifaatiba vyenye thamani ya shilingi Milioni 500 kwa ajili ya vituo mbalimbali vya kutolea huduma za afya vilivyotolewa na Bohari ya Dawa yaliyofanyika katika Hospitali ya Wilaya. (Picha na Maktaba) Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Judith Nguli, akipokea vifaatiba vyenye thamani ya shilingi Milioni 500 kwa ajili ya vituo mbalimbali vya kutolea huduma za afya vilivyotolewa na Bohari ya Dawa yaliyofanyika katika Hospitali ya Wilaya. (Picha na Maktaba)

MVOMERO

Na Faustine Gimu

Mkuu wa Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro, Judith Nguli ametoa wito kwa wananchi wa Wilaya hiyo kutumia fursa ya Siku ya Afya Duniani kuchunguza Afya zao bure.
Aidha amewataka wananchi hao kushiriki kikamilifu kaatika mazoezi ili kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza.
Judith alisema hayo ofisini kwake wilayani Mvomero mkoani Morogoro, baada ya kufanya Kikao na Timu kutoka Wizara ya Afya, Ofisi ya Mganga Mkuu wa Mkoa na Halmashauri ya Mvomero, kuelekea maadhimisho hayo yanayofanyika April 7, kila mwaka.
Alibainisha kuwa katika kuelekea Siku ya Afya Duniani April 7, wananchi wanatakiwa kuchangamkia fursa kuchunguza Afya zao na kushiriki Michezo mbalimbali.
“Wananchi wa Mvomero tuchangamkie kuchunguza Afya zetu katika kuelekea Siku ya Afya Duniani, maana kutakuwa na uchunguzi wa Saratani ya mlango wa kizazi, shinikizo la juu la damu, lishe hivyo nawakaribisha sana,”alisema Judith.
Aidha, Judith alisema kupitia maonesho hayo itakuwa ni fursa kubwa kwa Wananchi kufanya mazoezi kupitia mashindano ya michezo yatakayosaidia kuimarisha Afya ya mwili, na akiipongeza Wizara ya Afya kwa kuchagua Wilaya ya Mvomero kufanyiwa maadhimisho hayo.
Maadhimisho ya Afya Duniani yatafanyika yakienda sambamba na kaulimbiu isemayo”Afya Yangu, Haki Yangu”

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.