Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

PM aonya matumizi dawa za kulevya

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akizindua mbio za Mwenge wa Uhuru katika Viwanja vya Chuo cha Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro hivi karibuni. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akizindua mbio za Mwenge wa Uhuru katika Viwanja vya Chuo cha Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro hivi karibuni.

KILIMANJARO

Na Muhina Semwenda

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa wito kwa Watanzania kuepuka matumizi ya dawa za kulevya kwani yanaharibu nguvukazi ya Taifa, hasa kwa vijana ambao wanategemewa kuongoza kufanya shughuli za uzailishaji na kuharakisha maendeleo.
Alitoa wito huo katika sherehe za uzinduzi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru zilizofanyika kitaifa katika Viwanja vya Chuo cha Ushirika Moshi, Mkoani Kilimanjaro.
“Idadi kubwa ya waathirika wa matumizi ya dawa za kulevya ni watoto na vijana wenye umri kati ya miaka 13 hadi 24. Kundi hili ni nguvukazi ya Taifa letu, Serikali, haiwezi kunyamaza itaendelea kufanya msako mkali ili wahusika wote wa biashara hiyo haramu wachukuliwa hatua kali,”alisema Waziri Mkuu Majaliwa.
Alisema kuwa Serikali kwa kutambua umuhimu wa udhibiti wa biashara ya dawa za kulevya imeendelea kuongeza kasi ya mapambano ili kukomesha biashara, kilimo na matumizi ya dawa za kulevya. “Hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wote wanaojihusisha na kilimo hicho haramu pamoja na biashara ya dawa za kulevya”
Alisema mbio za Mwenge wa Uhuru za mwaka 2024 zitaendelea kutoa hamasa kwa jamii kusitisha kilimo haramu cha bangi, biashara na matumizi ya dawa za kulevya. Aidha, utajiekeleza kwenye kuhamasisha jamii kulima kilimo cha mazao halali ya biashara na chakula, pamoja na kuhamasisha jamii kushiriki katika shughuli nyingine halali na zenye staha.
Alibainisha, “Hivi karibuni, kumeibuka aina nyingine ya bangi yenye kiasi kikubwa cha kilevi, ikifahamika kama “skanka”. Aina hii ya bangi yenye sumu nyingi huchanganywa kwenye sigara, na vijana wamekuwa wakitumia skanka ambayo imekuwa ikipelekea kuchanganyikiwa,.”
Alisema kuwa vijana wamekuwa wakitumia bidhaa hizo wakifahamu uwepo wa skanka na wengine bila kufahamu na hivyo hujikuta wanakuwa waraibu wa bangi.
Kwa mujibu wa Waziri Majaliwa, idadi kubwa ya waathirika wa matumizi ya dawa za kulevya ni watoto na vijana wenye umri kati ya miaka 13 hadi 24.
Alisema kuwa Serikali itaendelea kufanya msako mkali ili wahusika wote wa biashara hiyo haramu wachukuliwe hatua kali, na kuongeza kasi ya mapambano ili kukomesha biashara, kilimo na matumizi ya dawa za kulevya.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu Majaliwa alisema kwamba mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka huu utaendelea  kuhimiza mapambano dhidi ya rushwa, huku akitoa wito kwa Watanzania kupambana na vitendo vya rushwa.
“Tafiti za taasisi za kitaifa na kimataifa zinaonesha kuwa Tanzania imeendelea kufanya vizuri katika mapambano dhidi ya rushwa. Kwa mujibu wa taarifa ya utafiti wa REPOA iliyotolewa Machi 9, mwaka 2022, Tanzania inafanya vizuri katika mapambano dhidi ya rushwa, ambapo zaidi ya asilima 77 ya Watanzania waliohojiwa walikiri kuwa rushwa imepungua nchini.”
Kadhalika, amesema kwamba Serikali kupitia mbio za mwenge, itaendelea kuwashurikisha wananchi na wadau wengine  katika mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI.
Naye Waziri wa Habari, Vijana Utanaduni na Michezo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Tabia Mwita Maulid, alisema kuwa mbio za mwenge wa Uhuru zimeendelea kudumisha Uhuru, amani mshikamano uzalendo na umoja wa kitaifa pia zimekuwa kichocheo kikubwa cha maendeleo ya kijamii.
Awali, Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu, Mheshimiwa Patrobas Katambi, amesema kwamba falsafa ya Mwenge wa Uhuru imekuwa ni kuwaunganisha Watanzania, kuleta matumaini pamoja na kukagua miradi inayotoa huduma kwa wananchi ili kusogeza huduma kwa wananchi.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.