Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

LONDON, ENGLAND
Mshambuliaji wa Corinthians Memphis Depay amekosoa uamuzi wa Shirikisho la Soka la Brazil (CBF), kuwaadhibu wachezaji kwa mbwembwe za kusimama juu ya mpira wakati wa mechi.
CBF imetangaza kwamba wachezaji wanapaswa kuonyeshwa kadi ya njano, iwapo watasimama juu ya mpira kwa miguu yote miwili, na timu pinzani ikapewa mkwaju wa faulo usio wa moja kwa moja.
Uamuzi huo ulikuja baada ya Depay kufanya hatua hiyo katika dakika za majeruhi, wakati wa ushindi wa fainali ya Paulista A1 dhidi ya Palmeiras mnamo Machi 28.
Ustadi huo, uliochezwa karibu na bendera ya kona baada ya Depay kujifanya kuvuka mpira ndani ya kisanduku, uliwakera wachezaji wa Palmeiras na kuzua rabsha kubwa kati ya timu zote mbili.
Kipa wa akiba wa Palmeiras, Marcelo Lomba na kiungo wa kati wa Corinthians, Jose Martinez walitolewa nje baada ya ukaguzi wa muda mrefu wa VAR, ambao ulisababisha zaidi ya dakika 18 za muda wa nyongeza, kuongezwa na maafisa.
Katika barua iliyofuata kwa vilabu, CBF ilisema kwamba kitendo cha kusimama kwenye mpira ni chokozi kwa mpinzani na kutoheshimu mchezo.

LONDON, ENGLAND
Mlinzi wa Memphis Grizzlies, Ja Morant ametozwa faini ya dola 75,000, kwa kosa la kutumia ishara ya vidole wakati wa mchezo.
Morant alitoa ishara hizo wakati wa ushindi wa Grizzlies wa 110-108, dhidi ya Miami Heat huko Florida hivi karibuni.
NBA inasema kuwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 alionywa hapo awali na ofisi ya ligi, kwamba ishara ya kutumia vidole inaweza kutafsiriwa katika mtazamo mbaya.
Morant ambaye aliifunga timu inayoongoza kwa pointi 30 amesimamishwa mara mbili na NBA, kwa kuonyesha ishara ya bastola kwenye mitandao ya kijamii.
Alipigwa marufuku kwa michezo minane bila malipo mnamo Machi 2023, kwa kutoa ishara ya bunduki kwenye video ya Instagram Live.
Morant pia alipewa adhabu ya kufungiwa michezo 25 ili kuanza msimu wa 2023-24, baada ya video yake kuonyesha akipiga picha akiwa na bunduki kusambaa mtandaoni.
Baada ya tukio la kwanza, aliomba msamaha na kusema alichukua jukumu kamili kwa matendo yake.
Alisema kuwa atafanya kazi katika kujifunza mbinu bora za kukabiliana na mfadhaiko na ustawi wake kwa ujumla, na kwamba baada ya kutafakari, aligundua kile anachopaswa kupoteza.

Na Nicolaus Kilowoko

Kocha wa zamani wa Yanga Princess, Edna Lema ‘Mourinho’, ambaye kwa sasa ameongezwa kwenye Benchi la Ufundi la kikosi cha Wanaume cha Yanga, amekiri kuvutiwa na uwezo wa mchezaji Pacome Zouzoua.
Edna ambaye ameunganishwa katika kikosi cha wanaume mara baada ya Ligi ya wanawake kusimama, hivi karibuni ameonja ushindi wa kwanza mara baada ya timu yake ya Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union.
Alisema kuwa miongoni mwa wachezaji ambao anavutiwa nao na wenye uwezo, uzoefu, akili na maarifa wakiwa uwanjani ni Pacome ambaye kwa sasa ana mabao nane kwenye orodha ya wafungaji wa Ligi Kuu.

BAGAMOYO

Na Mathayo Kijazi

Baada ya mchakato wa muda mrefu hatimaye Bagamoyo Lango la Ukristo Tanzania sasa historia yake imekamilika, kutokana na kuundwa kuwa Jimbo jipya Katoliki, huku Baba Mtakatifu Fransisko akimteua Mhashamu Askofu Mteule Stephano Musomba, kuwa Askofu wa kwanza wa jimbo hilo.
Kabla ya uteuzi huo Mhashamu Musomba alikuwa Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, aliyekuwa akisimamia Mawasiliano jimboni humo.

DAR ES SALAAM

Na Mathayo Kijazi

Waamini wameonywa kuepuka kukata tamaa kutokana na majaribu wanayokutana nayo, kwani hayo ni sehemu ya maisha yao.
Kauli hiyo ilitolewa na Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Rita wa Kashia – Goba, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Padri Musa Kihoo wakati wa homilia yake katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Dominika ya Kwanza ya Kwaresima iliyofanyika parokiani hapo.

MBEYA

Na Angela Kibwana

Mhashamu Godfrey Jackson Mwasekaga, Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu la Mbeya, amesema malengo ya Kwaresima ni kufanya toba, wongofu wa ndani na uaminifu kwa neno la Mungu.
Aidha, amesema kuwa Neno la Mungu ni chakula cha kiroho, na ni taa ya kuwaongoza waamini kwenye njia ya Ukristo wao.
Askofu Mwasekaga alisema hayo wakati akitoa homilia yake katika Adhimisho la Misa Takatifu, aliyoadhimisha katika Parokia ya Mtakatifu Clara wa Asizi- Shewa Jimbo Kuu Katoliki Mbeya.

Waamini wa Parokia ya Mtakatifu Yakobo Mkuu Mtume – Kijitonyama, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam wakiwa katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Dominika iliyoadhimishwa parokiani hapo hivi karibuni.

Mapadri na Viongozi wa Halmashauri ya Walei kutoka Parokia mbalimbali za Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, wakifurahia jambo wakati wa mkutano wao, uliofanyika katika viwanja vya Kituo cha Msimbazi, jimboni humo hivi karibuni.

Paroko wa Parokia ya Bikira Maria Mlima wa Karmeli – Bunju, Jimbo Katoliki Teule la Bagamoyo, Padri Dominic akiwaombea Wakatekumeni wapya wanaojiandaa kubatizwa katika Mkesha wa Pasaka wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Dominika ya Kwanza ya Kwaresima iliyoadhimishwa parokiani hapo. (Picha zote na Yohana Kasosi)

DAR ES SALAAM

Na Joseph Mihangwa

Ghafla, Afrika imenyamaza kupiga kelele juu ya paa kutangaza sera zake za maendeleo zenye sura ya ubinadamu; sera zilizojaa kurasa za Vyombo vya Habari enzi za uhuru na zama za mageuzi ya uchumi kufuatia uhuru, kwa maandishi makubwa makubwa na kwa wino wa kuangaza:
“Ujamaa” kwa Tanzania; “Zambian Humanism” kwa Zambia; The Common Man’s Charter” – Uganda na “The Guinean Revolution” kwa Guinea ya Rais Ahmed Sekou Toure.