Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Maadhimisho Miaka 30 Redio Tumaini yafana

Paroko wa Parokia ya Familia Takatifu – Mburahati, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Padri Vitalis Kassembo, akipokea zawadi ya ‘T-shirt’ kutoka wawakilishi wa Tumaini Media wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Shukrani kwa kutimiza Miaka 30 ya Redio Tumaini, iliyoadhimishwa parokiani hapo. (Picha na Mathayo Kijazi) Paroko wa Parokia ya Familia Takatifu – Mburahati, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Padri Vitalis Kassembo, akipokea zawadi ya ‘T-shirt’ kutoka wawakilishi wa Tumaini Media wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Shukrani kwa kutimiza Miaka 30 ya Redio Tumaini, iliyoadhimishwa parokiani hapo. (Picha na Mathayo Kijazi)

NA MATHAYO KIJAZI

Wakati Redio Tumaini ikiadhimisha Jubilei ya Miaka 30 tangu kuanzishwa kwake maadhimisho ambayo yameonekana kufana, imeelezwa kuwa mtu anayetunza afya ya akili, ataweza kuamua na kutenda mambo mema maishani  mwake.
Paroko wa Parokia ya Familia Takatifu- Mburahati, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Padri Vitalis Kassembo, alisema hayo wakati akitoa homilia yake katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Shukrani kwa Mungu kwa Redio Tumaini kutimiza miaka 30, tangu kuanzishwa kwake Februai 3, mwaka 1994.
Aliwasisitiza Waamini kuitunza afya ya akili na roho, wakiitunza miili yao ili waendelee kuunda utakatifu katika maisha yao.
“Katika maisha, wengi wetu mara nyingi tunajikuta tunaumwa afya ya akili. Afya ya akili imetusababishia miili yetu isiwe na afya njema. Hata hivyo, magonjwa hayo yametufanya tuteseke mno, kwa sababu wakati mwingine unaweza kupewa habari ya msiba wa kifo cha mtu wako wa karibu, unjikuta unashikwa na ‘presha’ kwa kuwa akili yako haikuwa tayari kupokea habari hiyo,” alisema Padri Kassembo.
Padri Kassembo aliwaasa Waamini kuwa na utayari wa kumtumikia Mungu, kwani anayefanya mambo ya Mungu, na Mungu naye hufanya mambo ya mtu huyo.
“Tunakumbushana kufanya Tafakari ndugu zangu. Tuwe na utayari wa kumtumikia Mungu…kumbuka kwamba unapoamua kufanya mambo ya Mungu, na Mungu naye anafanya mambo yako,” alisema Padri Kassembo.
Ka mujibu wa Padri Kassembo Waamini wanatakiwa kujenga utamaduni wa kusameheana, wanapokoseana, kwani hiyo itawafanya wazidi kupokea baraka za Mungu katika maisha yao.
Aidha, Padri huyo aliipongeza      Tumaini Media, hasa Redio Tumaini kwa kutimiza miaka 30 tangu ilipoanzishwa, akisema chombo hicho cha habari kina mchango mkubwa katika kuinjilisha na kuhabarisha.
Alibainisha kwamba wapo wagonjwa ambao hawawezi kwenda popote, ila wanafarijika wanaposikiliza Redio Tumaini, kutazama Tumaini Tv, na kusoma taarifa mbalimbali zinazoandikwa katika gazeti la Tumaini Letu.
Kwa upande wake Mratibu wa Matukio ya Kanisa Tumaini Media, Gaudence Hyera, alimshukuru Padri Kassembo kwa kukubali Sherehe za Miaka 30 ya Redio Tumaini zifanyike parokiani hapo.
Hyera alisema kuwa Familia Takatifu ndiyo chanzo cha yote yanayoendelea kutendwa na Kanisa, hivyo Misa hiyo kuadhimishwa katika Parokia ya Familia Takatifu, ni kumshukuru Mungu aliyeamua Familia hiyo iwepo.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.