Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Dk. Biteko ataka kipaumbele manunuzi ya Serikali

Hafla ya utiaji saini hati ya makubaliano kati ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC). Hafla ya utiaji saini hati ya makubaliano kati ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC).

DODOMA

Na Mwandishi wetu

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko ameiagiza Taasisi zote za ununuzi nchini (Serikali na Binafsi) kuhakikisha zinatoa kipaumbele katika manunuzi ya bidhaa na huduma zinazozalishwa ndani ya nchi ili kukuza uchumi wa Watanzania, na wazingatie kutoa kipaumbele kwa wafanyabiashara wadogo na makundi maalum.
Dk. Biteko alisema hayo Jijini Dodoma katika hafla ya utiaji saini hati ya makubaliano kati ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (Public Procurement Regulatory Authority: PPRA) na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (National Economic Empowerment Council: NEEC) ili kujenga ushirikiano unaolenga kuchochea ushiriki wa Wafanyabishara Wadogo, wa kati na Makundi Maalum, katika masuala ya ununuzi wa umma.
“Kusainiwa kwa hati hii leo, kunazidi kuboresha mazingira ya Watanzania kushiriki kwenye uchumi wa nchi yao, hasa watu kutoka makundi maalum. Haya ni  maelekezo ya Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha Watanzania wote wanashiriki kwenye shughuli za kiuchumi, hivyo NEEC, PPRA, Taasisi nyingine za Serikali na Binafsi, wawezesheni Watanzania kushika uchumi wa nchi na muone fahari katika hili,” alisema Dk. Biteko.
Kupitia hafla hiyo, Dk. Biteko aliitaka PPRA kuzidi kuboresha huduma zake kwa Watanzania, ikiwa ni pamoja na kuharakisha mchakato wa rufaa zinazowasilishwa kwenye mamlaka hiyo, hususan zile zinazohusisha waombaji wa zabuni kutoka makundi maalum ili kuchochea kasi ya ukuaji wa Uchumi wa mtu mmoja mmoja, na hatimaye Uchumi wa Taifa.
Alizitaka mamlaka hizo kujikita zaidi katika uwezeshaji wa wananchi kwa kutoa elimu, badala ya kubaki kuwa wadhibiti pekee.
Dk. BIteko aliongeza kusema kwamba NEEC na PPRA kufanya tathmini na kutoa tuzo kwa watoa huduma wanaofanya vizuri katika uwezeshaji wa makundi maalum suala litakalochagiza ushindani miongoni mwa watoa huduma, na hatmaye kukuza uchumi.
Alisema kuwa makubaliano hayo yatatumika kama jukwaa la kuwahamasisha watu wa kundi hilo kushiriki na kuimarisha uchumi wa mtu mmoja mmoja, kuimarisha wigo wa walipa kodi, na hivyo kukuza uchumi wa nchi.
Aliipongeza PPRA kwa kuweka kanuni ya ushirikishaji makundi maalum kwenye manunuzi ambayo imeelekeza kuwa asilimia 30 ya zabuni zote zitolewe kwa washiriki kutoka makundi maalum, ambao ni wanawake,vijana, wazee na wenye mahitaji maalum.
Kwa upande wake, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), Jenista Mhagama, alisema kusainiwa kwa hati ya makubaliano kati ya PPRA na NEEC ni ushahidi wa namna Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan alivyoamua kwa dhati kushikirisha makundi ya watu maalum kwenye uchumi na ujenzi wa Taifa.
Alisema kuwa makubalinao hayo yataongeza ushiriki wa makundi maalum kwenye manunuzi ya umma, na hii itaongeza uwezo wa Watanzania katika uzalishaji malighafi na bidhaa pamoja na utoaji wa huduma ndani ya nchi.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.