Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Waaswa kuwakumbuka wanyonge

DAR ES SALAAM

Na John Kimweri
Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Jude Thaddeus Ruwa’ichi, amewataka waamini kutoa kipaumbele na kuwakumbuka wanyonge na watu wasiojiweza katika karamu mbalimbali wanazoziandaa.
Wito huo aliutoa hivi karibuni wakati akitoa homilia yake katika Adhimisho la Misa ya kutoa Sakramenti Takatifu ya Kipaimara, iliyokwenda sanjari na uchangiaji wa ujenzi wa nyumba ya Mapadri, iliyofanyika katika Parokia ya Mtakatifu Dominiko Savio, Mikoroshini Tandika, jimboni humo.
Alisema Wakristo hawawezi kumlipa Kristo kwa kazi kubwa ya ukombozi aliyoifanya, lakini kwa njia ya kuwasaidia wengine, wanaweza kufanya utume na kazi ya kumpendeza Mungu.
“Yesu anatuambia kwamba tunapofanya karamu, tuwakumbuke wanyonge kama maskini, viwete, na wale wasio na cha kutulipa, wale ambao hutegemei nao waandae sherehe wakualike,” alisema Askofu Ruwa’ichi.
Askofu Ruwa’ichi alieleza kuwa katika Pentekoste, Roho Mtakatifu aliwashukia mitume na kuwapa nguvu, uthubutu na msukumo wa kwenda kuitangaza Injili, bila kuogopa.
Alisema kijana anayeimarishwa akimpokea Roho Mtakatifu, anakamilishwa katika neema ya ubatizo, kwa kuwa katika ubatizo huzaliwa mara ya pili, na kufanywa kuwa mtoto wa Mungu na ndugu wa Kristo.
“Katika Pentekoste, Roho Mtakatifu aliwashukia Mitume na kuwapa nguvu na uthubutu na msukumo wa kwenda kuitangaza Injili. Hawa watoto leo kwao ni Pentekoste, na watampokea tena Roho Mtakatifu, kwasababu tayari walishampokea” alisema Askofu Ruwa’ichi.
Katika hatua nyingine, Padri Canisius Hali, wa Parokia hiyo amewaalika waamini na watu wote wenye mapenzi mema kushirikiana nao katika kazi hiyo ya ujenzi wa nyumba ya mapadri.
Kwa mujibu wa Padri Hali, alibainisha kuwa kwa sasa ujenzi huo upo katika hatua za mwisho, na kumshukuru Baba Askofu kwa ushauri na kuwa pamoja nao katika shughuli hiyo.
“Tunajenga nyumba ya mapadri ambayo ipo katika hatua za mwisho, na Baba Askofu amekuwa karibu nasi katika hatu zote, ninawaalika waamini kutoka maeneo mbalimbali ili kushirikiana nasi katika kazi hii” alisema Padri Hali.
Katibu wa Halmashauri ya Walei Parokia hiyo, Pankrasia Heri, alifafanua kuwa kwa sasa Paroko wa Parokia hiyo anaishi nje ya nyumba hiyo, na hivyo kumshukuru mmoja wa waamini ambaye ndiye aliyejitolea nyumba hiyo.
Alisema pia kuwa kukosekana kwa nyumba hiyo, na wasaidizi wengine ndani ya Parokia kama Mafrateri na mashemasi, kumesababisha utendaji kazi wa Paroko uwe mgumu.

 

Rate this item
(0 votes)
Last modified on Friday, 02 September 2022 09:25
Super User

Selfies labore, leggings cupidatat sunt taxidermy umami fanny pack typewriter hoodie art party voluptate. Listicle meditation paleo, drinking vinegar sint direct trade.

www.themewinter.com

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.