Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Kutoa huduma za kijamii ni kuinjilisha

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi akibariki jiwe la msingi la shule ya Parokia ya Bikira Maria Mama wa Rozari Takatifu - Makongo Juu, baada ya Adhimisho la Misa Takatifu ya Dominika ya Nne ya Kwaresma. Pembeni kwa Askofu ni Paroko wa Parokia hiyo, Padri Joseph Massenge. (Picha na Mathayo Kijazi). Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi akibariki jiwe la msingi la shule ya Parokia ya Bikira Maria Mama wa Rozari Takatifu - Makongo Juu, baada ya Adhimisho la Misa Takatifu ya Dominika ya Nne ya Kwaresma. Pembeni kwa Askofu ni Paroko wa Parokia hiyo, Padri Joseph Massenge. (Picha na Mathayo Kijazi).

DAR ES SALAAM

Na Mathayo Kijazi

Utoaji wa huduma za Kijamii zikiwemo Elimu, Afya, na huduma zingine katika kustawisha ustawi na maendeleo ya mwanadamu, ni njia mojawapo za uinjilishaji katika kumtangaza Yesu Kristo.
Hayo yalisemwa hivi karibuni na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Dominika ya Nne ya Kwaresma, iliyokwenda sanjari na kuweka jiwe la msingi katika Shule ya Parokia ya Bikira Maria Mama wa Rozari Takatifu - Makongo Juu, jijini Dar es Salaam.
“Hamkuishia hapo, mmepania kujikita katika huduma za kijamii. Huduma za Kijamii ni namna mojawapo ya uinjilishaji. Tunainjilisha kwa kutoa elimu, tunainjilisha kwa kutoa huduma za afya, tunainjilisha kwa kutoa huduma nyingine zozote zinazochangia ustawi na maendeleo ya mwanadamu;
“Basi, kwa kuwa na mikakati hiyo, nawatambua kama Parokia hai. Muendelee kuwa na umoja, muendelee kuwa na mwamko wa kichungaji, muendelee kuinjilisha na kumtangaza Kristo kwa hali na mali. Leo mnapoweka jiwe la msingi la shule ya Parokia hii, nawaombea shughuli hii iendelee vizuri ili ipate kufikia upeo unaotakiwa,” alisema Askofu Ruwa’ichi.
Awali katika homilia yake, Askofu Mkuu Ruwa’ichi aliwataka Wakristo kusikia furaha kutambulika kama watoto wa Mungu, na kama watu waliokombolewa katika maisha yao.
Aliwasihi kuendelea kumwomba Mungu awazidshie neema yake ili wazidi kukua katika fadhila, katika imani, na katika ushuhuda wa Kikristo.
Aidha, aliwaalika Waamini kutambua kwamba wao siyo Wakristo kwa sababu ya mastahili yao wala kutokana na wema wao, bali wako Wakristo kwa sababu Mungu anawapenda na kuwahurumia.
“Mungu alilichagua Taifa la Israel liwe Taifa lake Takatifu, siyo kwa sababu walikuwa Taifa kubwa kuliko Mataifa yote, na wala siyo kwa sababu walikuwa wazuri kuliko watu wote, bali Mungu aliwateua kutokana na huruma na upendo wake,” alisema Askofu Mkuu, na kuongeza,
“Na ukweli huo unaweza kuusema pia kuhusu sisi Wakristo. Sisi tuko Wakristo, siyo kwa sababu ya mastahili yetu, tuko Wakristo, siyo kwa sababu ya wema wetu, tuko Wakristo kwa sababu Mungu anatupenda.”
Kwa upande wake Paroko wa Parokia hiyo, Padri Joseph Massenge, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Tumaini Media, alimshukuru Askofu Mkuu Ruwa’ichi kwa kufika parokiani hapo na kudhimisha Misa hiyo Takatifu, pamoja na kuweka jiwe la msingi la shule ya Parokia hiyo.
Padri Massenge alisema kuwa lengo la kujenga shule hiyo, ni kuwapunguzia changamoto wazazi na walezi ambao mara kwa mara hutumia muda wao kuwapeleka watoto wao katika shule za mbali na eneo hilo.
“Shule hii tungependa iwe na mtindo wa shule kama ile ya St. Joseph kule mjini, kwa sababu watu wengi kutoka huku Makongo wanaamka usiku usiku kuwapeleka watoto wao kule St. Joseph,” alisema Padri Massenge.
Aidha, Padri Massenge alitumia nafasi hiyo kuwaomba Waamini kuchangia ujenzi wa shule hiyo, ili baadaye wapewe kipaumbele pindi wanapokwenda kuandikisha watoto wao kujiunga na shule hiyo.
“Lakini niwakumbushe ninyi vijana mnaozaa, nawaambia tena, hata kama Baba Askofu atanihamisha, nitarudi kuja kukagua siku ya kuandikisha watoto, kama majina yako hayapo kwenye vitabu vya kuchangia shule, kupata nafasi utapata tabu sana. Kwa hiyo mjitahidi mchangie,” alisema Padri Massenge.
Vile vile, Padri huyo alithibitisha kwamba shule hiyo haitakuwa na gharama kubwa katika utoaji wa huduma ya elimu, bali itakwenda katika mfumo wa kawaida, kwani ni Waamini wenyewe ndio wamechangia ujenzi huo.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.