Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Waamini legelege kiimani kusakwa

NDOLA, Zambia

Askofu wa Jimbo Katoliki la Ndola, nchini Zambia Mhashamu Benjamin Phiri amezitaka Jumuiya Ndogo Ndogo za Kikristo nchini humo kuwafikia Wakatoliki wasiotenda, na kuwahimiza kurejea Kanisani.
Askofu Phiri (pichani) alitoa wito huo wakati wa ziara yake ya kichungaji katika Parokia ya Mtakatifu Anthony - Mikomfwa Luanshya, na kusisitiza kuhusu umuhimu wa Jumuiya Ndogo Ndogo za Kikristo (SCCs) kuwafikia Wakatoliki ambao hawatendi tena imani yao na wameacha kuhudhuria kanisani.
Alisema kuwa jumuia kazi yake siyo tu kushirikiana na washiriki hai, bali pia kuwatafuta Waamini waliolala, kwani ni muhimu kuelewa sababu za kutokuwepo kwao, na hivyo kuwahimiza kwa bidii kuungana tena na Kanisa.
“Tunapokaribia kuhitimisha Jubilei kwa Jumuiya Ndogo Ndogo za Kikristo, naziomba SCCs kuunda ratiba ya kuwatembelea Wakatoliki ambao hawaendi tena kanisani,” alisema Askofu Phiri.
Alisisitiza kuwa SCCs, zikiwa na uhusiano wa karibu na jamii, zimejipanga vyema kushughulikia masuala mbalimbali ndani ya familia na jamii, huku zikitoa msaada na kutia moyo kwa ajili ya kuendelea kuomba.
SCCs, zenye sifa za vikundi vilivyotengwa kijiografia, hutumika kama majukwaa ya kushiriki Neno la Mungu na uzoefu wa maisha, kukuza uhusiano wa kina wa Kikristo.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.