Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Baba Mtakatifu awakingia kifua wahamiaji, wakimbizi

Baba Mtakatifu Fransisko akimbariki mmoja wa watoto wahamiaji katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, wakati Kumbukumbu ya Siku ya Wahamiaji na Wakimbizi, mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana mjini Vatican. Baba Mtakatifu Fransisko akimbariki mmoja wa watoto wahamiaji katika Uwanja wa Mtakatifu Petro, wakati Kumbukumbu ya Siku ya Wahamiaji na Wakimbizi, mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana mjini Vatican.

VATICAN CITY, Vatican

Baba Mtakatifu Fransisko amesema kwamba wakimbizi na wahamiaji wanapaswa kuombewa na kupewa hifadhi wanapoomba hifadhi.
Kauli hiyo ya Baba Mtakatifu imo katika tafakari yake kwa waamini waliofurika kwenye Uwanja wa Mtakatifu Petro, wakati Baba Mtakatifu akikumbushia Siku ya Wahamiaji na Wakimbizi, mara baada ya Sala ya Malaika wa Bwana.
Alisema kwamba kuna umuhimu wa kuwa na uhuru wa kukaa au kuondoka katika nchi, pamoja na ule wa kukaribishwa popote mtu anapokwenda.
Baba Mtakatifu akiwageukia waamini na mahujaji kutoka pande zote za Dunia waliounganika katika Uwanja wa Mtakatifu Petro akisema, “Leo (Jumalipi ya Septemba 24) ni Siku ya Wahamiaji na Wakimbizi Duniani, yenye kaulimbiu: ‘Huru kuchagua kuhama au kubaki,’ ili kukumbusha kwamba kuhama kunapaswa kuwa chaguo huru, na kamwe, si jambo pekee lisilowezekana.
Alisema kuwa haki ya kuhama sasa imekuwa wajibu kwa wengi, na hasa mahali ambapo panapaswa kuwepo haki ya kutohama, ni kubaki katika nchi ya mtu mwenyewe.
Baba Mtakatifu alisema kuwa ni lazima kwa kila mwanaume na mwanamke kuhakikishiwa haki ya kuishi maisha yenye heshima katika jamii anamojikuta.
Aliongeza kusema kuwa kwa bahati mbaya, umaskini, vita na mgogoro wa tabianchi, huwalazimisha watu wengi kukimbia nchi zao.
“Sote tunatakiwa kuunda jumuiya ambazo ziko tayari na wazi kukaribisha, kukuza, kusindikiza na kuunganisha wale wanaobisha hodi kwenye milango yetu,” alisema Baba Mtakatifu Fransisko.
Baba Mtakatifu aliikumbuka ziara iliyompeleka Kusini mwa Ufaransa ambapo alisema, “Changamoto hii ilikuwa katikati ya Rencontres Méditerranéennes, yaani Mikutano ya Mediteranea ambayo ilifanyika katika siku za hivi karibuni huko Marsiglia, na katika kikao chake cha kuhitimisha, nilishiriki jana, nikisafiri hadi jiji, njia panda ya watu na tamaduni.”

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.