Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Askofu Kibira aonya kuchomoza ubaguzi

Sista Jacinta na Sista Restetuta wakiwa katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Shukrani iliyoongozwa na Askofu Francis Aquirinus Kibira Kambale wa Jimbo Katoliki la Kasese (hayumo pichani), nchini Uganda. Sista Jacinta na Sista Restetuta wakiwa katika Adhimisho la Misa Takatifu ya Shukrani iliyoongozwa na Askofu Francis Aquirinus Kibira Kambale wa Jimbo Katoliki la Kasese (hayumo pichani), nchini Uganda.

KASESE, Uganda

Askofu Francis Aquirinus Kibira Kambale wa Jimbo Katoliki la Kasese nchini Uganda, amewatahadharisha Wakristo dhidi ya ubaguzi kwa misingi ya Dini na kabila.
Aidha, amewasihi waamini hao kuhakikisha wanazingatia maendeleo na elimu kwa manufaa ya jamii husika, badala ya kuendekeza ubaguzi miongoni mwao.
Askofu Kibira alitoa onyo hilo katika hotuba yake baada ya kuadhimisha Misa Takatifu ya Shukrani ya Mchungaji Restetuta Biira Katusabe, binti wa Mtakatifu Theresia wa Mtoto Yesu “Madada wa Banyateresa”, iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Nyabirongo, jimboni humo.
Katika hotuba yake, Askofu Kibira anayehusishwa na kusaka maendeleo, kuchukia umaskini na chuki miongoni mwa jamii kwa Wakristo waliopoteza ubinadamu kati yao, aliwataka waishi pamoja kwa amani.
Askofu Kibira alirejelea onyo lake la awali kwa wakuu wa familia dhidi ya kugawanya vipande vya ardhi miongoni mwa watoto, lakini kutumia ardhi iliyopo kwa tija ambayo itasaidia kuongeza mapato, ikiwemo karo ya shule kwa watoto wao.
Katika Misa hiyo, Askofu Kibira Kambale alimteua na kumtuma Padri Leosio Masereka kwenda kufanya utume katika Seminari Kuu ya Kitaifa ya Mtakatifu Paulo-Kinyamasika, baada ya kuhitimu Shahada yake ya Uzamivu (PhD) ya Liturjia kutoka Roma.
Askofu Kibira aliwaomba wazazi kuwatoa watoto wao ili wafanye kazi za Kanisa na kuwasaidia hasa katika elimu rasmi na isiyo rasmi, na kutaja familia kuwa shule ya kwanza, na wazazi ndio waalimu wa kwanza.
Akiongoza hotuba wakati wa Jubilei ya Fedha katika maisha ya Kidini ya shukrani ya Misa ya Mchungaji Jacinta Mbambu pamoja na kuadhimisha viwango tofauti vya elimu katika familia ya Padri Leosio, Askofu Kibira alibainisha kuwa kasisi huyo alimaliza PhD yake huko Roma, kabla ya kumteua kuwa Mhadhiri wa Seminari Kuu ya Kitaifa ya Mtakatifu Paulo.
Katika Homilia yake, Askofu Kibira aliwataka wazazi na walezi kufanya kazi ya kuwajenga watoto wao ili kuendana na huduma ya Kanisa na kuwekeza katika malezi ya watoto, huku akiwakumbusha kuendeleza upendo, msamaha na uvumilivu miongoni mwa mambo mengine.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.