Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Pondamali ‘aponda’ makipa wa kigeni

DAR ES SALAAM

Na Nicolaus Kilowoko

Aliyekuwa kocha wa makipa wa zamani wa timu ya soka ya Yanga, Juma Pondamali ameelezea kukerwa na ufalme wanaopewa makipa wa kigeni ndani ya Ligi ya Tanzania.
Pondamali alisema kuwa haikubaliki kwa makipa wa kigeni kutawala soka la Tanzania wakati kuna makipa wengi wenyeji wenye uwezo mkubwa ambao bado hawajapewa nafasi ya kuonyesha vipaji vyao.
Alisema kuwa nchi kama Misri wamefanikiwa kuweka utaratibu ambao unawasaidia hata sasa kuwa na wachezaji wengi wazawa kuliko wale wakigeni, na hiyo imewasaidia sana kufanya vyema katika soka lao.
“Never never’, haikubaliki wachezaji wa kigeni kuja kutawala soka la Kitanzania wakati sisi tuna vijana wengi sana ambao wana uwezo mkubwa wa kufanya vizuri katika vipaji vyao”, alisema Pondamali.
Alisema kuwa yeye anashauri hata Tanzania kuweka utaratibu wa kutokuwapa sana nafasi wachezaji wa kigeni ambao kwa wakati mwingine, ni sawa tu na wachezaji wenyeji.
Pondamali ambaye alidumu ndani ya klabu ya soka ya Yanga kwa miaka minne kama kocha wa makipa, alikuwa na wakati mzuri tangu alipokuwa akicheza, mpaka kuwa kocha.
Mbali na kuishauri mamlaka husika kuweka utaratibu wa wachezaji wa kigeni, lakini aliwashauri wachezaji vijana wazawa kuhakikisha kwamba wanajitahidi kufanya mazoezi na kutafuta mafunzo kwenye vituo mbalimbali ili kujinoa zaidi.
Pondamali alisema kuwa wao wamekuwa wakiwasaidia wachezaji wengi katika kituo chao kilichopo Mkwajuni wakati ligi inaposimama kwa muda, na wamekuwa wakifanya vyema kwenye timu zao, hivyo akaendelea kuwaomba wachezaji vijana kutafuta uzoefu kwenye kazi zao.
Ikumbukwe pia kuwa Pondamali aliwahi kuwa kipa wa Taifa Stars miaka ya zamani, ambapo mwaka 1980 alishiriki fainali za AFCON zilizofanyika nchini Nigeria, ambazo ndizo fainali za kwanza Tanzania kushiriki.
Mbali na hilo, aliidakia timu ya Yanga akiwa pamoja na wachezaji kama Fred Minziro (sasa kocha), Leodgar Tenga (Rais wa zamani wa TFF), na wengineo wengi.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.