Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Utume wa Kiaskofu ni Baraka

Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi akiwauliza maswali waimarishwa katika Parokia ya Mtakatifu Josephina Bakhita, Mtoni-Mtongani, wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Dominika ya Kwanza ya Kwaresma iliyokwenda sanjari na utoaji wa Sakramenti ya Kipaimara. (Picha na Yohana Kasosi) Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi akiwauliza maswali waimarishwa katika Parokia ya Mtakatifu Josephina Bakhita, Mtoni-Mtongani, wakati wa Adhimisho la Misa Takatifu ya Dominika ya Kwanza ya Kwaresma iliyokwenda sanjari na utoaji wa Sakramenti ya Kipaimara. (Picha na Yohana Kasosi)

DAR ES SALAAM

Na Mwandishi wetu

Miaka ya Utume wa Uaskofu inatajwa kuwa ni Baraka na huruma ya Mungu, kwani ni kuteuliwa na Kristo, na si kwa mastahili ya mtu binafsi.
Hayo yalisemwa hivi karibuni na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Jude Thaddaeus Ruwa’ichi, wakati akizungumzia kuhusu Jubilei ya Miaka 25 ya Uaskofu wake inayotarajiwa kuadhimishwa Mei mwaka huu.
“Kuhusu Miaka 25 ya Uaskofu wangu, naitazama kama ni miaka ya baraka na huruma ya Mungu, kwa sababu siyo kwa mastahili yangu, bali ni kwa kuteuliwa na Kristo Mwenyewe,” alisema Askofu Ruwa’ichi.
Aidha, Askofu Ruwa’ichi alisema kuwa kila Askofu anapowekwa mahali, anawekwa ili kukita mizizi ya kuliimarisha Kanisa, pamoja na Waamini wake.
Wakati huo huo aliongeza kuwa licha ya kwamba katika kipindi cha Uaskofu wake amehudumu katika Majimbo matano tofauti, bali alitii kila uhamisho wake, kwani hali hiyo ilimjenga kuwa imara katika Uchungaji wake, huku akishukuru mapokezi ya kila Jimbo alikotumwa.
Alisema kwamba wazazi wake walipomwita jina Ruwa’ichi, yaani ‘Mungu anajua’, yeye hakufahamu walimaanisha nini, bali limekuwa jina lenye baraka kwake.
Katika mazungumzo yake, Askofu Mkuu Ruwa’ichi alisema kuwa kazi alizozifanya kwenye Shirika lake akiwa kama Mkuu wa Shirika hilo, zimemwonyesha namna anavyoweza kuwa Mchungaji.
Akizungumzia kuhusu vijana, Askofu Ruwa’ichi alisema kuwa Kanisa nchini Tanzania lina utajiri mkubwa wa vijana, ila lina kazi kubwa ya kuendelea kuwajenga katika imani thabiti.
Aidha, alisema kuwa katika Majimbo yote aliyowahi kuhudumu kama Askofu, kumekuwa na changamoto tofauti tofauti kutokana na mazingira yaliyopo
Aliongeza kuwa alijitahidi kukabiliana na kila changamoto zilizokuwepo, bila kuwapendelea Waamini wala kuwakimbiza, yaani kuwapelekesha.
Akizungumzia juu ya familia yao, Askofu Ruwa’ichi alisema kuwa wamezaliwa watoto tisa, ambapo yeye ni wa kwanza, akiongeza kwamba licha ya familia yao kutokuwa ya kitajiri, bali walilelewa na kusomeshwa vizuri.
Askofu Mkuu alitumia nafasi hiyo kutoa pole kwa Askofu wa Zanzibar pamoja na Kanisa Visiwani humo kutokana na mtu mmoja ambaye aliingia kanisani na kufanya uharibifu, ukiwemo wa vitu vitakatifu.
Alisema kwamba ana imani kuwa vyombo vinavyohusika vitachukua hatua juu ya hilo, pamoja na kulikomesha, kwani kufanya hivyo ni tabia ya kutokuziheshimu imani za wengine.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.