Login to your account

Username *
Password *
Remember Me

Create an account

Fields marked with an asterisk (*) are required.
Name *
Username *
Password *
Verify password *
Email *
Verify email *
Captcha *
Reload Captcha

Utakaso unahitaji uvumilivu - Padri

Baadhi ya wazee wanaolelewa katika Kijiji cha Wazee kilichopo Msimbazi Centre, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, wakisubiri kupokea matoleo kutoka kwa Shirika la Wazee na Wastaafu Katoliki Jimbo, waliokwenda kufanya matendo ya huruma katika kijiji hicho hivi karibuni. (Picha na Yohana Kasosi) Baadhi ya wazee wanaolelewa katika Kijiji cha Wazee kilichopo Msimbazi Centre, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, wakisubiri kupokea matoleo kutoka kwa Shirika la Wazee na Wastaafu Katoliki Jimbo, waliokwenda kufanya matendo ya huruma katika kijiji hicho hivi karibuni. (Picha na Yohana Kasosi)

DAR ES SALAAM

Na Mwandishi wetu

Mlezi wa Shirika la Wazee na Wastaafu Katoliki, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, ambaye pia ni Paroko wa Parokia ya Moyo Mtakatifu wa Yesu, Manzese, jimboni humo, Padri Benedict Shayo, amesema kuwa safari ya utakaso inahitaji uvumilivu.
Padri Shayo alisema hayo wakati akizungumza na Tumaini Letu katika mahojiano maalumu baada ya Shirika hilo kufanya matendo ya huruma katika Kituo cha Kulelea Watoto Wadogo, na Kijiji cha Wazee katika Kituo cha Msimbazi, jijini Dar es Salaam.
Alisema kuwa wazee wastaafu wameamua kujitoa kwa kile kidogo walichonacho kusaidia wahitaji, hasa katika kipindi hiki cha Kwaresma, kwani ni kipindi cha kujikatalia, kujinyima na kujitoa kwa ajili ya wengine.
Alisema kuwa hatua hiyo imefikiwa katika kutimiza nia ya Misa yao ya Shukrani iliyofanyika parokiani Manzese.
Alsiema kuwa wanapotambua na kutathmini upendo wa Mungu wa kuwafikisha tena katika nyakati hizi, ni vyema wakatoa majitoleo yao, kwa kutoa vipawa walivyonavyo ili waweze kutimiza nia hiyo.
Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa Shirika la Wazee na Wastaafu Wakatoliki, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Profesa Alphonce Kyessi, alisema kuwa hatua hiyo ni katika kutimiza azma yao ya kufanya matendo ya huruma kwa kutoa sukari, mchele na mafuta kwa Wazee wa Kijiji cha Wazee, Msimbazi, ili nao waweze kujikimu.
“Tumewaona wazee wa hapa na tumetoa majitoleo yetu na tutaendelea kutekeleza wajibu huu …ni utaratibu wetu wa kila mwaka lakini mwaka huu tumeonelea vema tuje hapa Kijiji cha Wazee lakini pia tumetoa kwa Kituo cha kulelewa Watoto wadogo hapa Msimbazi,” alisema Proresa Kessy.
Aidha, Profesa Kessy amewasihi waamini na wote wenye mapenzi mema vijana UWAKA, WAWATa wanaendelea kufanya matendo ya huruma, si kwa wazee tu, lakini pia hata katika Hospitali kwa wagonjwa.
Naye Sista Rosina Isaya Ngukuyawene, Mlezi Mkuu wa Kijiji cha Wazee, Msimbazi, alisema kuwa changamoto kubwa ni bima ya afya, kwani waliyopewa na Ustawi wa Jamii ni ndogo na haiwasaidii sana wazee, na hivyo kulazimika kutoa fedha za ziada ili watibiwe.
Alisema kuwa changamoto nyingine ni uchakavu wa majengo ya nyumba za kuishi wazee hao, kwani nyingi hali yake ni mbaya na zinahitaji kufanyiwa ukarabati mkubwa kusudi wazee waishi katika mazingira bora zaidi.

Rate this item
(0 votes)

Leave a comment

Make sure you enter all the required information, indicated by an asterisk (*). HTML code is not allowed.